Wanaume mmepitwa mapenzi na mahaba na Jogoo

Najua haiwahusu ila nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji sasa basi nina majike wanne na jogoo moja, nimeshtushwa sana jinsi jogoo anavyowajali wake zake,
Kwanza, jogoo hali mpaka majike wale, anawaitia chakula yeye anasimama pembeni,
Pili, anawapeleka sehemu ya kutagia yaani anatengeneza sehemu ya jike wake kua comfy wakitaga hadi kulalia,
Tatu, anaishi nao wote kwa upendo mkubwa, hawabagui, hawapigi
Nne, anawalinda dhidi ya maadui ukimsogolea jike wake anatishia kukurukia, na kwa watoto wakiwa wanawafukuza majike wake hata awe mbali vipi atakuja mbio na kutaka kupigana,

Sasa kilichonifanya nilete huu uzi ni baada ya kuona Jogoo anawashinda akili, maarifa na mapenzi wanaume wengi kwa wake zao,
Imagine janaume zima limejaza misuli kwenye mikono yake linampiga mwanamke kama linakanda maandazi,
Janaume zima linakataa kumpeleka mwanamke wake clinic wakati mimba waliitafuta wote, janaume zima lipo radhi kwenda kula mapocho pocho peke yake au na michepuko yake huku mke na watoto wanashindia andazi moja moja, yaani wanaume wa kitanzania wengi wenu mna ubinafsi sana, mwanamke aliyekutoa kwenye ukoko enzi hizo unavaa kandambili ukishazipata unaanza kumuona mluga luga hana hadhi hata ya kuongozana na wewe, mwanamke wako amekuzalia watoto wazuri, ameharibu shape yake mwisho wa siku unamuona mzee, kiroba ananuka maziwa, shame!

Kuna siku tumeenda clinic ya mtoto, akaja mwanamke mjamzito ameongozana na mwanaume wake basi lile janaume eti linajishtukia kuonekana kama yupo nae, muda wote kainama kwenye simu huku anatupiga kijicho cha pembeni, mwanamke wa watu anamsemesha jamaa hamjibu na akijibu anajibu kama anakereka, ikafika muda wakaitwa waingie kwa nurse khe jamaa asigome nini yule dada akamwambia kwa sauti ya chini lakini wakuda tukainasa, "baba T mbona unanitia aibu lakini sio vizuri" basi likageuka tena kutuangalia akatukuta tumemkodolea macho kama yote likamwambia "tangulia si nakuja bhana" baadae kwa kujivuta vuta sana likaingia, alivyoona warembo tumekaa tumetulia akaona mkewe anamchoresha duh! na limgongo lake lililopinda kama chura mzee, mxiiiiiiiiue

Kuna hawa wasiosaidia wake zao mizigo yaan unakuta wametoka shopping janaume lipo busy linachat mwanamke kaelemewa na mizigo, hua wananikera sana wakati mwingine huwaomba wawasaidie wakati mwingine naishia kusonya tu,

Haya nyie wanaume suruali ujumbe wenu ndio huo mjirekebishe, heshimuni wake zenu, wapendeni, wajalini, walindeni kama Jogoo anavyofanya kwa mke wake, mnaweza kufuga kuku pia ili mjifunze kwa jogoo 🤣🤣🤣

Tchaao.
Hii ni mimba sio wewe mamdogo
 
Anaogopa kusema kuwa hakutuliza akili akakosa upendo kama huyo jogoo anaoutoa, akadakwa na wa kufanana naye jinsia; na sasa ametamani upendo wa jogoo na mitetea 4
Hahahahaha upendo na mahaba ninayoyapata huku siwezi kutamani upande wa jogoo hata kwa mtutu wa bunduki, weeeeeeh au basi
 
Kuna msemo rafiki yangu mkongomani alikuwa anawaambia watu "usiwe kama jogooo, kazi yake kuzalisha lakini hawajibiki kutunza watoto wake wala mwanamke wake".
Unataka binadamu tuige tabia za jogoo?
Pale anapoitia chakula ndiyo utongozaji wake, akishampanda Mara kadhaa hana habari naye anatafuta mwingine.
Jogoo hana pesa wala mali anaokota vya bure. Binadamu lazima apambane Sana kuvipata vya kuongea hivyo haongi kizembe au hovyo hovyo.
Jogoo hamuachi jike wake hata iweje, umeona sasa hadi jogoo anajua ili kumpata mwanamke sharti utoe chochote kitu ila nyie mkiombwa buku tu mnafungulia nyuzi mia mbili kwa saa
 
Kuna mwanamke anapenda mwanaume anayefanya Kama jogoo?; Yupo????
Mbona mnakimbilia kwenye sex? hapa yanazungumzwa mapenzi na mahaba, wanawake zenu wataka muwajali na muwapende, muwalinde na muwatetee,
Kajifunzeni kwenye maisha ya jogoo na wake zake
 
Najua haiwahusu ila nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji sasa basi nina majike wanne na jogoo moja, nimeshtushwa sana jinsi jogoo anavyowajali wake zake,
Kwanza, jogoo hali mpaka majike wale, anawaitia chakula yeye anasimama pembeni,
Pili, anawapeleka sehemu ya kutagia yaani anatengeneza sehemu ya jike wake kua comfy wakitaga hadi kulalia,
Tatu, anaishi nao wote kwa upendo mkubwa, hawabagui, hawapigi
Nne, anawalinda dhidi ya maadui ukimsogolea jike wake anatishia kukurukia, na kwa watoto wakiwa wanawafukuza majike wake hata awe mbali vipi atakuja mbio na kutaka kupigana,

Sasa kilichonifanya nilete huu uzi ni baada ya kuona Jogoo anawashinda akili, maarifa na mapenzi wanaume wengi kwa wake zao,
Imagine janaume zima limejaza misuli kwenye mikono yake linampiga mwanamke kama linakanda maandazi,
Janaume zima linakataa kumpeleka mwanamke wake clinic wakati mimba waliitafuta wote, janaume zima lipo radhi kwenda kula mapocho pocho peke yake au na michepuko yake huku mke na watoto wanashindia andazi moja moja, yaani wanaume wa kitanzania wengi wenu mna ubinafsi sana, mwanamke aliyekutoa kwenye ukoko enzi hizo unavaa kandambili ukishazipata unaanza kumuona mluga luga hana hadhi hata ya kuongozana na wewe, mwanamke wako amekuzalia watoto wazuri, ameharibu shape yake mwisho wa siku unamuona mzee, kiroba ananuka maziwa, shame!

Kuna siku tumeenda clinic ya mtoto, akaja mwanamke mjamzito ameongozana na mwanaume wake basi lile janaume eti linajishtukia kuonekana kama yupo nae, muda wote kainama kwenye simu huku anatupiga kijicho cha pembeni, mwanamke wa watu anamsemesha jamaa hamjibu na akijibu anajibu kama anakereka, ikafika muda wakaitwa waingie kwa nurse khe jamaa asigome nini yule dada akamwambia kwa sauti ya chini lakini wakuda tukainasa, "baba T mbona unanitia aibu lakini sio vizuri" basi likageuka tena kutuangalia akatukuta tumemkodolea macho kama yote likamwambia "tangulia si nakuja bhana" baadae kwa kujivuta vuta sana likaingia, alivyoona warembo tumekaa tumetulia akaona mkewe anamchoresha duh! na limgongo lake lililopinda kama chura mzee, mxiiiiiiiiue

Kuna hawa wasiosaidia wake zao mizigo yaan unakuta wametoka shopping janaume lipo busy linachat mwanamke kaelemewa na mizigo, hua wananikera sana wakati mwingine huwaomba wawasaidie wakati mwingine naishia kusonya tu,

Haya nyie wanaume suruali ujumbe wenu ndio huo mjirekebishe, heshimuni wake zenu, wapendeni, wajalini, walindeni kama Jogoo anavyofanya kwa mke wake, mnaweza kufuga kuku pia ili mjifunze kwa jogoo 🤣🤣🤣

Tchaao.
Mambo yasiwe mengi oleweni na jogoo wala hatuna baya
 
We Dr. Mariposa hayo mambo ya wanaume umeyajuaje? Na wewe unamfanyia hivyo mwenzio?? Au na wewe unafata mfano wa jogoo??
Ni rahisi, naishi kwenye jamii ya wanawake na wanaume nayaona, nayasikia pia,
Sie huku full kudekezana, kwetu ni furaha tu🥳🥳
 
Umeona hiyo profile pic yako?
Ndio mapenzi ya jogoo hayo
Ungeweka mfano wa njiwa ningekuelewa sana lakini jogoo? umeingia chaka.
Ukitaka ujue subili hao majike wawe na vifaranga atahamia hadi kwa jirani hapo au wakiatamia tu anarudi kwa jirani hata kwa kupambana na jogoo wa hapo hayo ni machache tu. Jogoo huua hadi vifaranga
 
Kuna sehemu siwezi kuongozana na wife. Clinic, sokoni, duka la vipodozi au saluni ya kike aisee uko siendi mimi
NAUNGA MKONO HOJA

Mwanaume yeyote mwenye akili timamu na ambaye hajapandwa kichwani hawezi fanya ufala huu.
Hadi unafkia hatua hiyo basi mkeo ndo kashika remote ya familia kabisa.
 
Ila ujue dakika moja ni nyingi kwa jogoo! Mnataka wanaume waige kwa jogoo? Mtaridhika?
 
Kwa hyo unataka tuwe tunawapanda hadharani
 
Wanaume wanapenda kuonekana single siku zote

Kuna couple nmekaa nayo kanisani leo
Mama amebeba mtoto mwanzo mwisho, baba hana habari, mtoto anasumbua mama ndo anahangaika, baba anhaaaaa amekaa kifalme...tabia mbaya
 
Sisi tunajua kwamba mnataka pesa tu !kumbe na mapenzi mnataka!?

*Kuolewa na KAZI Fulani kazi sana,hawana Hela hao" mwanamke analopoka mbele ya wenzake,Sasa unajiuliza mnataka pesa au mapenzi!!?

Chagueni kimoja,sio pesa mnataka na mapenzi mnataka mtakosa vyote nyie!!

Kwasasa Kila mwanamke ana bei yake sisi tufanyaje zaidi ya kuwanunua!!?

Majike ya jogoo hayajui pesa Wala jogoo hawazi pesa ndio maana anatoa mapenzi Kwa wakeze!!
 
Kwa hiyo una maanisha tuwe na mahaba kama jogoo lakini tusifanye mapenzi kama jogoo?

Maana kuna mtu nae alituchamba tusifanye mapenzi kama jogoo tushike lipi tuache lipi. Mnatuchanganya wajameni 😇😇
 
Duh mna muda hadi wa kuchunguza majogoo ili kuhalalisha ufeminism..have never seen this kind of rubbish in my gad damn life ..
 
Sasa huyo huyo jogoo ana matetea wanne, na nyie wanawake mtakubali kuolewa mitala kama kuku? Pia mtalubali kupigwa bao la sekunde moja kama la jogoo?

Back
Top Bottom