Wanaume mmepitwa mapenzi na mahaba na Jogoo

Najua haiwahusu ila nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji sasa basi nina majike wanne na jogoo moja, nimeshtushwa sana jinsi jogoo anavyowajali wake zake,
Kwanza, jogoo hali mpaka majike wale, anawaitia chakula yeye anasimama pembeni,
Pili, anawapeleka sehemu ya kutagia yaani anatengeneza sehemu ya jike wake kua comfy wakitaga hadi kulalia,
Tatu, anaishi nao wote kwa upendo mkubwa, hawabagui, hawapigi
Nne, anawalinda dhidi ya maadui ukimsogolea jike wake anatishia kukurukia, na kwa watoto wakiwa wanawafukuza majike wake hata awe mbali vipi atakuja mbio na kutaka kupigana,

Sasa kilichonifanya nilete huu uzi ni baada ya kuona Jogoo anawashinda akili, maarifa na mapenzi wanaume wengi kwa wake zao,
Imagine janaume zima limejaza misuli kwenye mikono yake linampiga mwanamke kama linakanda maandazi,
Janaume zima linakataa kumpeleka mwanamke wake clinic wakati mimba waliitafuta wote, janaume zima lipo radhi kwenda kula mapocho pocho peke yake au na michepuko yake huku mke na watoto wanashindia andazi moja moja, yaani wanaume wa kitanzania wengi wenu mna ubinafsi sana, mwanamke aliyekutoa kwenye ukoko enzi hizo unavaa kandambili ukishazipata unaanza kumuona mluga luga hana hadhi hata ya kuongozana na wewe, mwanamke wako amekuzalia watoto wazuri, ameharibu shape yake mwisho wa siku unamuona mzee, kiroba ananuka maziwa, shame!

Kuna siku tumeenda clinic ya mtoto, akaja mwanamke mjamzito ameongozana na mwanaume wake basi lile janaume eti linajishtukia kuonekana kama yupo nae, muda wote kainama kwenye simu huku anatupiga kijicho cha pembeni, mwanamke wa watu anamsemesha jamaa hamjibu na akijibu anajibu kama anakereka, ikafika muda wakaitwa waingie kwa nurse khe jamaa asigome nini yule dada akamwambia kwa sauti ya chini lakini wakuda tukainasa, "baba T mbona unanitia aibu lakini sio vizuri" basi likageuka tena kutuangalia akatukuta tumemkodolea macho kama yote likamwambia "tangulia si nakuja bhana" baadae kwa kujivuta vuta sana likaingia, alivyoona warembo tumekaa tumetulia akaona mkewe anamchoresha duh! na limgongo lake lililopinda kama chura mzee, mxiiiiiiiiue

Kuna hawa wasiosaidia wake zao mizigo yaan unakuta wametoka shopping janaume lipo busy linachat mwanamke kaelemewa na mizigo, hua wananikera sana wakati mwingine huwaomba wawasaidie wakati mwingine naishia kusonya tu,

Haya nyie wanaume suruali ujumbe wenu ndio huo mjirekebishe, heshimuni wake zenu, wapendeni, wajalini, walindeni kama Jogoo anavyofanya kwa mke wake, mnaweza kufuga kuku pia ili mjifunze kwa jogoo 🤣🤣🤣

Tchaao.
Wamekudinya pabaya siyo?,au bado hujapata show ya kibabe upunguze hizo story za kuponda ponda miamba
 
Kuna sehemu siwezi kuongozana na wife. Clinic, sokoni, duka la vipodozi au saluni ya kike aisee uko siendi mimi
Clinic kwa mara ya kwanza ni mandatory kwa mwanaume kumsindikiza mkewe ili wote mpimwe magonjwa, na kupata ushauri wa mwanzo kwa pamoja.
 
Kuna sehemu siwezi kuongozana na wife. Clinic, sokoni, duka la vipodozi au saluni ya kike aisee uko siendi mimi
We kwaio wanapo itaga baba mtoto yupo wapi ww umechill ulipo ivyo vingine ni sawa ila hospital utaki
 
Kuna sehemu siwezi kuongozana na wife. Clinic, sokoni, duka la vipodozi au saluni ya kike aisee uko siendi mimi
Unaona sasa, clinic hasa kipindi cha ujauzito ni muhimu muende nyote mkapimwe afya zenu na kupewa shauri mbali mbali,
Sokoni tena wewe ndio unapaswa kwenda na sio mkeo, wewe mwanaume ndie inafaa ununue manunuzi yote ya nyumbani huko masokoni kuna ushawishi mkubwa sana kwa wake zenu
 
Wanaume wanapenda kuonekana single siku zote

Kuna couple nmekaa nayo kanisani leo
Mama amebeba mtoto mwanzo mwisho, baba hana habari, mtoto anasumbua mama ndo anahangaika, baba anhaaaaa amekaa kifalme...tabia mbaya
Sahihi kabisa wanaume wanapenda kuonekana single and free, wanaona kuonekana wanajali wake zao jamii itawaona ni dhaifu na waliopotea
 
Jogoo hamuachi jike wake hata iweje, umeona sasa hadi jogoo anajua ili kumpata mwanamke sharti utoe chochote kitu ila nyie mkiombwa buku tu mnafungulia nyuzi mia mbili kwa saa
Shida unaeza toa hela nyingi kwa mwanamke na usipate chochote hata busu unaeza usiambulie, ila mwanaume ambae hajawahi toa hata 100, anapewa mahaba yote kisa ana muonekano mzuri, wanaume ndo tunaogopa hiyo Dr. Mariposa
 
Mbona mnakimbilia kwenye sex? hapa yanazungumzwa mapenzi na mahaba, wanawake zenu wataka muwajali na muwapende, muwalinde na muwatetee,
Kajifunzeni kwenye maisha ya jogoo na wake zake
Jogoo na wake zake, uko tayari mwanaume awe na wake zake Kama jogoo?
 
Huu uzi utakua na vawulensi sana, ngoja nikae na 🍿 nisome comments. Lol
20250228_173346.jpg

😀😃😃😃
 
Jogoo hamuachi jike wake hata iweje, umeona sasa hadi jogoo anajua ili kumpata mwanamke sharti utoe chochote kitu ila nyie mkiombwa buku tu mnafungulia nyuzi mia mbili kwa saa
Jogoo ana mahitaji mengi mfano wa binadamu?
Anajitafutia mwenyewe? E.g. Tiba, mavazi, na makazi(shelter),elimu, n.k?
It sleeps and rest on it's shit, that's why it can spend it's entire resources for the sake of having 3secs of mating with a hen. Why worry if you aren't responsible even for yourself?
 
Shida unaeza toa hela nyingi kwa mwanamke na usipate chochote hata busu unaeza usiambulie, ila mwanaume ambae hajawahi toa hata 100, anapewa mahaba yote kisa ana muonekano mzuri, wanaume ndo tunaogopa hiyo Dr. Mariposa
Pesa iendane na swaga jamani usipooze sana, be a bad boy wanawake wanapenda sana bad boys 😂
 
Jogoo ana mahitaji mengi mfano wa binadamu?
Anajitafutia mwenyewe? E.g. Tiba, mavazi, na makazi(shelter),elimu, n.k?
It sleeps and rest on it's shit, that's why it can spend it's entire resources for the sake of having 3secs of mating with a hen. Why worry if you aren't responsible even for yourself?
Dooh! Yote hayo kwa jogoo jamani mimi wito wangu ni mfate matendo yake mema anayowafanyia wake zake na nyie muyafanye kwa wake zenu
 
Najua haiwahusu ila nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji sasa basi nina majike wanne na jogoo moja, nimeshtushwa sana jinsi jogoo anavyowajali wake zake,
Kwanza, jogoo hali mpaka majike wale, anawaitia chakula yeye anasimama pembeni,
Pili, anawapeleka sehemu ya kutagia yaani anatengeneza sehemu ya jike wake kua comfy wakitaga hadi kulalia,
Tatu, anaishi nao wote kwa upendo mkubwa, hawabagui, hawapigi
Nne, anawalinda dhidi ya maadui ukimsogolea jike wake anatishia kukurukia, na kwa watoto wakiwa wanawafukuza majike wake hata awe mbali vipi atakuja mbio na kutaka kupigana,

Sasa kilichonifanya nilete huu uzi ni baada ya kuona Jogoo anawashinda akili, maarifa na mapenzi wanaume wengi kwa wake zao,
Imagine janaume zima limejaza misuli kwenye mikono yake linampiga mwanamke kama linakanda maandazi,
Janaume zima linakataa kumpeleka mwanamke wake clinic wakati mimba waliitafuta wote, janaume zima lipo radhi kwenda kula mapocho pocho peke yake au na michepuko yake huku mke na watoto wanashindia andazi moja moja, yaani wanaume wa kitanzania wengi wenu mna ubinafsi sana, mwanamke aliyekutoa kwenye ukoko enzi hizo unavaa kandambili ukishazipata unaanza kumuona mluga luga hana hadhi hata ya kuongozana na wewe, mwanamke wako amekuzalia watoto wazuri, ameharibu shape yake mwisho wa siku unamuona mzee, kiroba ananuka maziwa, shame!

Kuna siku tumeenda clinic ya mtoto, akaja mwanamke mjamzito ameongozana na mwanaume wake basi lile janaume eti linajishtukia kuonekana kama yupo nae, muda wote kainama kwenye simu huku anatupiga kijicho cha pembeni, mwanamke wa watu anamsemesha jamaa hamjibu na akijibu anajibu kama anakereka, ikafika muda wakaitwa waingie kwa nurse khe jamaa asigome nini yule dada akamwambia kwa sauti ya chini lakini wakuda tukainasa, "baba T mbona unanitia aibu lakini sio vizuri" basi likageuka tena kutuangalia akatukuta tumemkodolea macho kama yote likamwambia "tangulia si nakuja bhana" baadae kwa kujivuta vuta sana likaingia, alivyoona warembo tumekaa tumetulia akaona mkewe anamchoresha duh! na limgongo lake lililopinda kama chura mzee, mxiiiiiiiiue

Kuna hawa wasiosaidia wake zao mizigo yaan unakuta wametoka shopping janaume lipo busy linachat mwanamke kaelemewa na mizigo, hua wananikera sana wakati mwingine huwaomba wawasaidie wakati mwingine naishia kusonya tu,

Haya nyie wanaume suruali ujumbe wenu ndio huo mjirekebishe, heshimuni wake zenu, wapendeni, wajalini, walindeni kama Jogoo anavyofanya kwa mke wake, mnaweza kufuga kuku pia ili mjifunze kwa jogoo 🤣🤣🤣

Tchaao.
Simnasema 50/50....imekuwaje tena!
 
Back
Top Bottom