Wanaume mkoani Shinyanga waangua kilio kwa madai ya kunyimwa unyumba na wake zao

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Baadhi ya wanaume mkoani Shinyanga wamelalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwamo kupigwa na kupigwa na wake zao.

Hayo wameyasema Jumanne Desemba 7, 2021 wakati wakipewa elimu ya ukatili wa kijinsia na dawati la jinsia la polisi katika stendi ya mabasi wilayani Shinyanga.

Peter Makalanga amesema kuwa "Kwa kweli wanaume tumekuwa tukifanyiwa ukatili wa kijinsia tunashukuru kutuletea elimu hii hapa stendi, lakini wanaume tuna nyanyasika sana siku hizi, wake zetu wanatunyima unyumba, lakini akijua unachepuka ndipo mgogoro unapoanzia na kufikia hatua ya kupigana," amesema Makalanga.

Naye, Seni Wiliam amesema kuwa migogoro ikitokea kweneye familia wao wanawake wamekuwa wakikimbilia polisi kushtaki.

"Tunaomba mtusaidie waambieni wake zetu waache kutufanyia ukatili, kwani wao ukiwagusa tu tayari wanakimbilia Polisi kushitaki, hiyo siyo sawa, lakini ukiangalia chanzo cha yote hayo ni yeye mweyewe kuni nyima unyumba," aliongeza.

Kwa upande wake Mkuu wa dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi wilayani Shinyanga, Brightone Rutajama amewataka wanaume kufika kwenye dawati hilo kutoa taarifa za kufanyiwa vitendo vya ukatili na wake zao na siyo kuona aibu.

"Nawaomba wanaume mnapofanyiwa ukatili na wake zenu msisite kuja kwenye dawati la jinsia, kwani tunapokea malalamiko ya watu wote bila ya ubaguzi na kisha kuyatafutia ufumbuzi ikiwamo kutatua migogoro ya ndoa, lakini wanaotoa taarifa za kufanyiwa ukatili wengi hua ni wanawake tu" amesema Rutajama.

"Katika mwaka 2020 walifanyiwa ukatili watu 225 lakin kwa mwaka huu 2021 wamefanyiwa ukatili watu 188, hivyo matukio yamepungua kwa kwa mwaka huu ukilinganisha na
mwaka uliopita, nawaomba muendelee kupiga vita ukatili wa namna yeyote
"amesema Lutajama.

Pia amewataka wafanyabiashara wa standi ya mabasi wilayani Shinyanga kuacha kufanyiana vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwamo kutoleana lugha chafu.

Wakitaja sababu za kuwafanyia vitendo hivyo, baadhi ya wanawake waliohudhuria semina hiyo wamedai wanafanya hivyo kutokana na baadhii ya wanaume kutoka nje ya ndoa.

Mkazi wa kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, Elizabeth Joseph amedai kuwa chanzo cha wanaume wengi kunyimwa unyumba ni wanaume kutoka nje ya ndoa mara kwa mara, ambapa wakati mwingine wanaume wanachati na michepuko hadharani hivyo kusababisha mke kukasilika na kumnyima unyumba mme wake.

images (8).jpeg
 
Ndiyo, ni kweli zimejaa mitaani ila ni ngumu ku approach ukakubaliwa chapchapu ukapewa. Ya nyumbani unajilia muda wowote ukitaka bila gharama yoyote tena bila wasiwasi maana ni yako kihalali na jamii inajua hivyo.
Tuone picha yako na unako ishi, wanawake hawa hawa wanaokufuata wenyewe ushindwe kumla siku moja.
 
Ndiyo, ni kweli zimejaa mitaani ila ni ngumu ku approach ukakubaliwa chapchapu ukapewa. Ya nyumbani unajilia muda wowote ukitaka bila gharama yoyote tena bila wasiwasi maana ni yako kihalali na jamii inajua hivyo.
Pole Sana,wenzio kila siku ni siku ya kutongoza na siwezi kuwa na mwanamke mmja,never ndio maana kamwe siwezi jiliza wala kujibembeleza kwa mwanamke to that extent..
 
Back
Top Bottom