nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,398
kuna movie moja nimeona mdada wa college analazimisha kuacha nguo zake kwenye geto la jamaa ili kujihakikishia umiliki...wanawake tuna kazi;
dudu..mende,nzi,au unazungumzia nini hapa
Na mimi hili ndio limekuwa swali langu ka kwanza; Mbona vyumba vingi hapa mjini?
Tatizo letu wengi wetu wanawake/wasichana mwalimu wetu kipofu...ukiamua kuishi na mwanaume bila ndoa tegemea yote kuolewa au kutemwa. sababu hakuna mkataba wowote baina yenu at the same time umeshusha thamani yako katika jamii inayoamini mwanamke anakuwa cheap akijipeleka kuishi na mwanaume kinyemela.
Kuishi na mtu hakubadili status ya kuwa wewe ni girlfriend tu
Tuite dua au utabiri?
kulia alie tetere akilia bundi uchuroooh eeeeeeeeeeee
Mmezidi kututegea fumanizi sikuhizi........yaani siku hizi ukienda kukutana na demu unakua na wasiwasi kama unaenda kunyongwa.
Jamani naombeni ushauri wenu kwa huyu rafiki yangu ni mrembo wa haja kweli kama mnavyojua wahaya figure namba nane black beauty, tataizo lake anahitaji sana kuolewa na umri umeenda sana ana 28yrs old, wanaume wamekuwa wakimrubuni kwa mapenzi wakisikia habari ya ndoa wanakimbia nayeye haitaji boyfriend kilio chake ni kuolewa.
Nikama miezi 6 sasa hivi imeshapita alimpata kijana mmoja mtanashati wakapendana sana, baada ya muda mfupi Yule kijana akamwambia ahame alipokuwa amepanga chumba ahamie kwake waanze maisha ya mume na mke , dada akashukuru akajua ndio kuolewa huko, akaachia chumba huko alikokuwa amepanga akahamia kwa kijana huku maisha yakiendelea, kijana akawaanamshawishi abebe mimba, basi kwakua dada hakua na mtoto aliona ni sawa akabeba mimba baada ya mimba kufikisha kama mwezi na nusu kijana akamchenchia akamwambia atoe hiyo mimba hayuko tayari kuwa na mtoto kwa kipindi hicho na dawa za kutoa hiyo mimba akamletea ikabidi bidada azinywe ili maelewanao ya wepo, baada ya mimba kutoka mapenzi yakaendelea motomoto nakijana akamwambia bidada mwezi dec nitakupeleka kwetu kukutambulisha nawewe unipeleke kwenu ili tuanze process za ndoa, basi wakakubaliana maisha yakaendelea.
Hivi majuzi rafikiyangu kaja kunilalamikia mwanaume amebadilika sana wakipata mgeni kama ni mwanaume,kijana anaenda kulala na mgeni sebuleni anamuacha rafiki yangu chumbani peke yake hatakama mgeni atakaa wiki mbili hali itaendelea hivyo hadi mgeni aondoke, kingine nikwamba mwanaume anapigiwa simu hadi saa nane za usiku na xgirl wake, ikabidi rafiki yangu achukue hiyo namba ya simu ili apate ukweli, kupiga hiyo simu akapokea msichana alivyojaribu kumuuliza huyo kijana ninani kwake akamwambia ni mchumba wake nahapo alipo anaujauzito wa miezi 3 na wanategemea kufunga ndoa mapema mwakani na December anampeleka kijijini kwao kumtambulisha ikabidi shost wangu ashtuke kwa maneno ya huyo dada, ikabidi amuulize mwanaume nini kinaendelea jibu mwanaume alilomjibu nikwamba kwenye ukoo wao walishakatazwa kuoa wahaya kwahiyo aamue atakaloamua, sasa rafiki yangu alichoamua kasema bora anywe sumu kuliko kumuacha jamaa kwasababu kaachia chumba chake buree kumbe mwaume ana mdanganya, nilichomshauri asithubutu kunywa sumu kwajili ya mwanaume kwani haitamsaidia chochote.
Naombeni ushauri wenu rafiki yangu afanyeje kwahili wakubwa zangu