WANAUME mkilogwa na WANAWAKE mtasema mmeonewa?

WANAUME mkilogwa na WANAWAKE mtasema mmeonewa?

Ndo vile.......kwani kazaliwa nae.......hiyo ndio mitihani ya kujiandaa na necta......sio kila uhusiano lazima uzae ndoa........asimame......ajikung'ute.......aendelee na safari......achunge tu.....kilichomwangusha kisimwangushe tena........

we mrombo unamawazo hadimu
 
Jamani naombeni ushauri wenu kwa huyu rafiki yangu ni mrembo wa haja kweli kama mnavyojua wahaya figure namba nane black beauty, tataizo lake anahitaji sana kuolewa na umri umeenda sana ana 28yrs old, wanaume wamekuwa wakimrubuni kwa mapenzi wakisikia habari ya ndoa wanakimbia nayeye haitaji boyfriend kilio chake ni kuolewa.
Nikama miezi 6 sasa hivi imeshapita alimpata kijana mmoja mtanashati wakapendana sana, baada ya muda mfupi Yule kijana akamwambia ahame alipokuwa amepanga chumba ahamie kwake waanze maisha ya mume na mke , dada akashukuru akajua ndio kuolewa huko, akaachia chumba huko alikokuwa amepanga akahamia kwa kijana huku maisha yakiendelea, kijana akawaanamshawishi abebe mimba, basi kwakua dada hakua na mtoto aliona ni sawa akabeba mimba baada ya mimba kufikisha kama mwezi na nusu kijana akamchenchia akamwambia atoe hiyo mimba hayuko tayari kuwa na mtoto kwa kipindi hicho na dawa za kutoa hiyo mimba akamletea ikabidi bidada azinywe ili maelewanao ya wepo, baada ya mimba kutoka mapenzi yakaendelea motomoto nakijana akamwambia bidada mwezi dec nitakupeleka kwetu kukutambulisha nawewe unipeleke kwenu ili tuanze process za ndoa, basi wakakubaliana maisha yakaendelea.
Hivi majuzi rafikiyangu kaja kunilalamikia mwanaume amebadilika sana wakipata mgeni kama ni mwanaume,kijana anaenda kulala na mgeni sebuleni anamuacha rafiki yangu chumbani peke yake hatakama mgeni atakaa wiki mbili hali itaendelea hivyo hadi mgeni aondoke, kingine nikwamba mwanaume anapigiwa simu hadi saa nane za usiku na xgirl wake, ikabidi rafiki yangu achukue hiyo namba ya simu ili apate ukweli, kupiga hiyo simu akapokea msichana alivyojaribu kumuuliza huyo kijana ninani kwake akamwambia ni mchumba wake nahapo alipo anaujauzito wa miezi 3 na wanategemea kufunga ndoa mapema mwakani na December anampeleka kijijini kwao kumtambulisha ikabidi shost wangu ashtuke kwa maneno ya huyo dada, ikabidi amuulize mwanaume nini kinaendelea jibu mwanaume alilomjibu nikwamba kwenye ukoo wao walishakatazwa kuoa wahaya kwahiyo aamue atakaloamua, sasa rafiki yangu alichoamua kasema bora anywe sumu kuliko kumuacha jamaa kwasababu kaachia chumba chake buree kumbe mwaume ana mdanganya, nilichomshauri asithubutu kunywa sumu kwajili ya mwanaume kwani haitamsaidia chochote.

Naombeni ushauri wenu rafiki yangu afanyeje kwahili wakubwa zangu
kwa kifupi ajipange upya hana jinsi akubaliane na matokeo kwakua aking'ang'ania hapo bado anatafuta shida zaidi na kupoteza mda.
 
mimba alitoa na saiv anataka ajiue??
wkati anazaliwa alijua atakutana na huyo mwanaume?
mapenzi yanauma sana,sawa,lakini si sababu ya kujitoa uhai
nyie marafiki zake kaeni nae karibu,mumfariji..katika kipindi hiki kigumu anawahitaji sana yani
 
Akome kujipeleka kwa mwanaume bila hatua za muhimu kuchukuliwa na hatimaye ndoa.Hata kama umempenda mwanaume kuna baadhi ya vitu ukifanya unaonekana wa bei rahis,sasa we k kaitimbaaaa weeeee na mimba kuchomoa juu!!!!Hakuna ndoa hapo,atulize moyo ila ndo ajipange maisha yenyewe vita toshaaa.
 
Marufuku kuhamia kwa mwanaume, lazima mwanaume ahamie kwangu hutaki sepa
Ukihamia kwangu siku ukinikoroga nakutimua na nguo ya mwilini tu
 
Aaaaanh nimekumbuka kitu!!!!!

Amwambie huyo mwanaume waende kwa baba wa mwanaume wakasuluhishwe na iwe asubuhi na mapema ndio suluhu zinapatikanaga!!!!!!!

Cc Kongosho Ennie Heaven on earth
 
Ukioa mhaya ni majanga!Wanaona wao kwa wao hao.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Jamaa anaonekana awali alimpenda kweli huyo dada ila kuna uwezekano kapata ushauri kutoka kwa ndugu kuhusu wahaya na ndomana akawahi haraka kumwambia atoe ule ujauzito ili kusiwe na uunganishi tena!ndugu tuangalie sana mashauri yetu kwa ndugu zetu.
 
Ndo vile.......kwani kazaliwa nae.......hiyo ndio mitihani ya kujiandaa na necta......sio kila uhusiano lazima uzae ndoa........asimame......ajikung'ute.......aendelee na safari......achunge tu.....kilichomwangusha kisimwangushe tena........

Neno la hekima hili,ajipange na aendelee,huyo mvulana(si mwanaume) hajielewi he is so low and stupid,how come anacheza na hisia za watu kirahisi hivyo?
 
Duuh So sad kwakwel! Baadhi ya nyie wanaume mna matatizo gn lkn???? Mtachomwa moto nyie kwa hayo makusud yenu,oohooooo!!
 
too much expectation ya ndoa kwa akina dada inawaumiza sana,hasa pale muda unapoenda ushauri wangu ahamie sehemu ambapo atakuwa mgeni eneo hilo then akianzisha mahusiano mengine basi asikubali kutoa papuchi aweke wazi lengo lake ndoa na hapendi kuchezewa asiyeweza sharti hilo amtapike itherwise atalia kila siku,mwanaume kumtangazia ndo girl kunahusisha vitu vingi sio tu kwa sababu una k basi unaweza kuolewa.
 
Aaaaanh nimekumbuka kitu!!!!!

Amwambie huyo mwanaume waende kwa baba wa mwanaume wakasuluhishwe na iwe asubuhi na mapema ndio suluhu zinapatikanaga!!!!!!!

Cc Kongosho Ennie Heaven on earth

Akikubali huu ushauri wako aje nimuazime cha moto! Huku kwetu zinauzwa kwa mafungu.
 
Na mimi hili ndio limekuwa swali langu ka kwanza; Mbona vyumba vingi hapa mjini?

Tatizo letu wengi wetu wanawake/wasichana mwalimu wetu kipofu...ukiamua kuishi na mwanaume bila ndoa tegemea yote kuolewa au kutemwa. sababu hakuna mkataba wowote baina yenu at the same time umeshusha thamani yako katika jamii inayoamini mwanamke anakuwa cheap akijipeleka kuishi na mwanaume kinyemela.

Kuishi na mtu hakubadili status ya kuwa wewe ni girlfriend tu


Kwa hiyo anataka kujiua sababu ya chumba alichoachia zaidi ya kukosa ndoa? Hii story sijaielewa kabisa.

Kulala sebuleni na mwanamme na kumwacha yeye chumbani, je akija mgeni mwanamke inakuwaje?
 
Hata mimi si ndio nashangaa...asije akawa ana apply theory za MMU....mimi nimeolewa na 29 na wala sikuwa na pressure ya kunifanya nijimuvuzishe kwenye geto la mtu


miaka 28 ndo umri umeenda? Mbona sie wengine tumeolewa 36 hata presha hatukuwa naO???
 
Back
Top Bottom