Wanaume huwa mnaangalia nini mtafutapo mke?

Wanaume huwa mnaangalia nini mtafutapo mke?

17342955_922658744542624_8684626147277408608_n-jpg.483119


Tabia mnabadilisha eti eeh!!
Kuna watu wana wake wazuriiii na bado huko nje wanahangaika hatari, tena anakwenda kutembea na mtu ambae hamfikii mkewe hata robo.
 

Attachments

  • 17342955_922658744542624_8684626147277408608_n.jpg
    17342955_922658744542624_8684626147277408608_n.jpg
    68.9 KB · Views: 195
Wanaangaliaga makalio na huyo jamaa kwenye hii stori yako ndio mwakilishi wetu. Japo kuna washamba baadhi ambao bado wanaangalia tabia na mienendo kama vigezo vikuu.
 
Wanaangaliaga makalio na huyo jamaa kwenye hii stori yako ndio mwakilishi wetu. Japo kuna washamba baadhi ambao bado wanaangalia tabia na mienendo kama vigezo vikuu.
Oooooops!! Kumbe vigezo vingine ni ushamba!!
 
Habari wana JF,

Leo nimepewa story ambayo imenifurahisha na kunisikitisha kidogo.
Kuna jamaa alikuwa na mpenzi wake waliedumu kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa, baadae jamaa akaanza visa tu na kumuacha binti bila sababu za msingi.

Alikuwa akiulizwa na marafiki zake kwanini amemuacha yule binti wakati ni boonge la wife material, jamaa alikuwa akisema eti binti ni mshamba mshamba yeye anahitaji binti mjanja, kweli akampata boonge la duu na akawa anajiona amefika haswaaa.

Baada ya muda jamaa alipata ajali mbaya iliyopelekea kuhitaji huduma hadi za kuogeshwa na ndugu zake walikuwa mbali, marafiki walimuhudumia japo sio kivile na wakati mwingine alipitisha hata siku tatu bila kuoga, inshort alihitaji huduma ya karibu sanaaa.

Mpenzi wake mpya hakumjali na wala hakujishughulisha nae, yule binti wa kwanza alipopata habari kuwa jamaa anapata taabu sana alikwenda kumuona na kuamua kumhudumia vizuri sana hadi jamaa alipopata nafuu, na binti alijitolea kweli hata kifedha.

Jamaa sasa akili ndio zikamrudi na akamuomba binti msamaha na kumuomba warudianae, ila binti alikataa katakata na kumwambia kuwa amemuhudumia tu kama ambavyo angeweza kumhudumia binadamu yeyote aliyepatwa na shida ila hawezi kurudiana nae. Jamaa alijitahidi kila njia ila binti aligoma kurudiana nae.

Baada ya mwaka binti aliolewa na mwanaume mwingine. Na jamaa kabaki hadi sasa anahangaika tu na kulaani wanawake anasahau kuwa yeye pia aliwahi kuvurunda huko nyuma.

Hapo ndipo nikawaza "ama kweli wanaume hawajui nini wanataka kwakweli".
Mke mwema huwa hatafutwi, uletwa na Mungu..
 
Back
Top Bottom