Wanaume huwa mnaangalia nini mtafutapo mke?

Wanaume huwa mnaangalia nini mtafutapo mke?

ila sometimes sisi wanaume ni wapumbavu kweli yan unapata demu anayekupenda kwa dhati halafu,unamkataa kwa sababu za kishenzishenzi tu,,,et mshamba!!!!!!! halafu unataka mjanja anayekuchuna then unakuja kulalamika ooh sijui anapenda hela.....

samahani kama nimewakwaza wanaume wenzangu lakini tunaambizana ukweli tu.
Asee dem nikiona mshamba ndio nampenda zaid
[emoji28]
 
At least atakua mama fresh, at least tutasikilizana.
Napenda mtu a play role ile ya mama naturaly
Hata akiwa msomi ataiplay tu naturally.
Mbona wapo ambao hadi wanaacha kazi kwa muda ili alee.
 
Labda kuna sababu zinazomfanya mume aende nje. Mie nimechoka leo sijisikii nataka kulala mapema. We unataka kila siku mie nachoka sana. Mke kukosa utundu kwenye sita kwa sita. Usiniulize definition ya utundu. Akienda nje kwa bidada asiyefikia uzuri wa mkewe hata kwa 5% anasuuzika roho yake na kujisemea kimoyo moyo, "Natamani mke wangu kwenye sita kwa sita angekuwa kama huyu."
Ndio umfundishe, we si ulivutiwa na umbo tu na vingine ukadai utamfundisha?
Ndio umvumilie hivyo hivyo maana ndio chaguo lako.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wengine hawafundishiki weye Mume huyooo anajiendea nje kujirusha. Mtu kishakwambia kachoka kuna darasa tena hapo!? Mtandao umeyaanika mengi ya ndani ya ndoa ambayo zamani yalikuwa siri na baadhi wakiamua kufunguka wanafunguka hasa unabaki kutoa macho tu.

Ndio umfundishe, we si ulivutiwa na umbo tu na vingine ukadai utamfundisha?
Ndio umvumilie hivyo hivyo maana ndio chaguo lako.
 
Uzuri wa mke si sura ni tabia.
Kama wewe kweli ni Mwanamke nyamaza usiwasemee wanaume,, mwanamme Aliyekamilika hahitaji tabia pekee,, mwanamme anahitaji mwanamke mwenye vigezo vyote vitabu 3 (1)Mzuri wa sura na shape na mzuri 6×6 (2)Tabia njema (3)mwenye hofu ya MUNGU yaani mwanamke mwenye kuweza kujishusha,, ukikosa kimojawapo ya hivyo hapo juu lazima mwanamme atakusaliti tu siyo kuwa Hakupendi hapana Bali atataka kuwa na wewe na muda huo huo akitafuta usichokuwa nacho
 
Habari wana jf.

Leo nimepewa story ambayo imenifurahisha na kunisikitisha kidogo.
Kuna jamaa alikuwa na mpenzi wake waliedumu kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa, baadae jamaa akaanza visa tu na kumuacha binti bila sababu za msingi.

Alikuwa akiulizwa na marafiki zake kwanini amemuacha yule binti wakati ni boonge la wife material,jamaa alikuwa akisema eti binti ni mshamba mshamba yeye anahitaji binti mjanja, kweli akampata boonge la duu na akawa anajiona amefika haswaaa.

Baada ya muda jamaa alipata ajali mbaya iliyopelekea kuhitaji huduma hadi za kuogeshwa na ndugu zake walikuwa mbali, marafiki walimuhudumia japo sio kivile na wakati mwingine alipitisha hata siku tatu bila kuoga, inshort alihitaji huduma ya karibu sanaaa.

Mpenzi wake mpya hakumjali na wala hakujishughulisha nae, yule binti wa kwanza alipopata habari kuwa jamaa anapata taabu sana alikwenda kumuona na kuamua kumhudumia vizuri sana hadi jamaa alipopata nafuu, na binti alijitolea kweli hata kifedha.

Jamaa sasa akili ndio zikamrudi na akamuomba binti msamaha na kumuomba warudianae, ila binti alikataa katakata na kumwambia kuwa amemuhudumia tu kama ambavyo angeweza kumhudumia binadamu yeyote aliyepatwa na shida ila hawezi kurudiana nae. Jamaa alijitahidi kila njia ila binti aligoma kurudiana nae.

Baada ya mwaka binti aliolewa na mwanaume mwingine. Na jamaa kabaki hadi sasa anahangaika tu na kulaani wanawake anasahau kuwa yeye pia aliwahi kuvurunda huko nyuma.

Hapo ndipo nikawaza "ama kweli wanaume hawajui nini wanataka kwakweli".
Practical guidelines to evaluate a potential wife
Angalia sifa zifuatazo wakati unachagua mke mtarajiwa
Nitaeleza kwa kifupi kama ifuatavyo...
Kumbuka herufi hizi...
A B C D E F

Age=Of about your age
Gape lisizidi miaka 10...
B=Beauty anayekuvutia
C=Character Tabia unazozikubali
D=Dignity anayejiheshimu
E=Education .....of about the same level of education.
F= Family ....Of about the same level of family status

Baada ya ku evaluate hizo sifa on a piece of paper ....l insist uwe very honest!!..mkweli na nafsi yako....
Mpe maksi....mfano labda umempa maksi 65%....sasa angalia udhaifu wake uko wapi?? Wapi amepoteza maksi 35??
Kumbuka huwezi kumpata mwanamke ambaye utampa 100%
Utakuwa unajidanganya.......
MASWALI mawili ya kujiuliza
1.Je nitaweza Kuishi na madhaifu yake??
2.Kama siwezi nitayarekebishaje??

NB: kama hayarekebishiki na huwezi kuishi na madhaifu yake...achana naye!!!!! Tafuta mwingine......WAKE WA KUOA WENYE SIFA WAPO...
Nakaribisha MASWALI.. .nitajibu kadri ya uwezo wangu.....lengo ni kuwasaidia wale walio ktk hatua ya kutafuta wake watakao dumu ktk ndoa zao....
 
Back
Top Bottom