Wanaume, huu si uungwana hata kidogo

Wanaume, huu si uungwana hata kidogo

Habari za asubuhi....
Naomba niende moja kwa moja kwenye lengo langu....
Kuna baadhi ya wanaume wana tabia ambayo mimi binafsi sipendezwi nayo kwa hakika. Mwanaume anakuwa anathamini watoto kuliko mke wake aliyemzalia hao watoto..... Sisemi msiwapende watoto wenu ila mjitahidi kubalansi.
Utaona mtu yuko bize na watoto tu...weekend anachukua watoto anawatoa out,kama ni zawadi wanapata watoto tu. Hata akiweka picha facebook ni kuweka watoto mwanzo mwisho.....huoni hata siku moja kaweka picha ya mkewe au walau aweke wanae pamoja na mama yao. Niliwahi kuona mtu ameweka picha facebook eti 'bon voyage my daughter' nikajiuliza hivi huyu mtoto wa mwaka mmoja anasafiri hadi Mwanza peke yake? Hata ukiangalia kwenye visimu vyao vya tochi huoni picha ya mkewe hata moja.
Hivi kuna sababu zozote za msingi zinazowafanya muwe hivyo? Huyo mwanamke ndiye aliyewaweka tumboni miezi tisa hao watoto unaojivunia....akaenda leba na hatimaye na wewe ukapata cha kujisifia mbele ya wanaume wenzio. Hivi bado hamjui kuwa kuna wanawake wanatoa mimba? Au hamjui kuwa kuna watu walichezea ujana wao hadi leo hawana uwezo wa kushika mimba? (siwazungumzii wale wenye matatizo ya uzazi yaliyotokea kwa bahati mbaya)
Sasa kinachokufanya usimthamini huyu mwanamke ni nini?
Huyo ndo mkeo...ulimchagua kati ya maelfu uliowaona...na hayo matunda unayoringia umeyapata kupitia yeye. Mthamini mkeo...be proud of her.
Ni hayo tu

Sasa huu wivuuuuu amaaaaa?
 
Mh..akili yangu ya ki-teamB ikawaza wewe ni mchepuko wa watu flan flan ivi...

then akili ikarudi sawa nikajiuliza, hapo siku za nyuma niliwahi kusikia malalamiko haya, 'Mke wangu toka ajifungue, attention yote kahamishia kwa mtoto'

Hii ya leo ni mpya..ngoja niifanyie uchunguzi.
 
Mkuki kwa nguruwe eehe, mbona hata ninyi hamtuweki kwenye whatsApp profile zenu au any social media halafu muda mwingi unautumia kukaa na watoto kuliko mimi Baba.
 
we nawe mbn unajiingiza kwenye team ya watokwa povuu!!... hii yote ni nini hasa, kuwekwa kwenye profile pic. au? sasa watoto wako mwenyewe halafu unawaonea wivu kweli!! ..kawabemende basi ili wachukize mbele za watu....nyie ndo mnamwagia wanawake wenzenu uji usoni kwa wivu uliopitiliza kamu huu wako.
 
Mchepuko wa watu gani? Hem jibu kwanza hilo ndo tuendelee
 
Mkuki kwa nguruwe eehe, mbona hata ninyi hamtuweki kwenye whatsApp profile zenu au any social media halafu muda mwingi unautumia kukaa na watoto kuliko mimi Baba.

Mbona watu mmekomalia profile? Kuna mahali nimesema muwaweke kwenye profile?
 
Mazoea kwamba umesahau kuwa una mke au?
Nadhani hata akinamama huamua kuinvest kwa watoto. Kuinvest kwa mke kunakuwa na risk kubwa kuliko watoto maana ni damu yako, hawezi kukuangusha jumla.
 
we nawe mbn unajiingiza kwenye team ya watokwa povuu!!... hii yote ni nini hasa, kuwekwa kwenye profile pic. au? sasa watoto wako mwenyewe halafu unawaonea wivu kweli!! ..kawabemende basi ili wachukize mbele za watu....nyie ndo mnamwagia wanawake wenzenu uji usoni kwa wivu uliopitiliza kamu huu wako.

Duuuh haya bwana....hujaelewa au unajilazimisha kutoelewa? Kuna mahali nimetaja profile hapo? Mi sijawaonea wivu maana sijaexperience hicho kitu.... Nimeona jinsi kaka zangu wajomba na rafiki zangu wanavyofanya nikaona sio vizuri
 
Mbona watu mmekomalia profile? Kuna mahali nimesema muwaweke kwenye profile?

Kamwulize mmeo kwa nini hakufanyii hicho unacholalamika, maana wengine tunawafanyia wake zetu. Wewe ulipokwishaolewa ukadhni ndo umefika unathani mume atakuwa na hamu na wewe tena, halafu lisura lenywe ndilo hilo, wacha ahamishie mapenzi kwa watoto.
 
Lakini nionavo mimi wanawake ndo wanaoongoza kuwapenda watoto kuliko waume zao. Utakuta mwanamke kabla hajazaa alikuwa anampenda sana mume wake lakini akishazaa tu idadi ya watoto anayojua inamtosha ujue basi hana habari na tena na kumjali mumewe na anatamani aachane naye ili abaki na watoto. Na endapo ataachwa kubaki na watoto, basi uje atawajaza sumu watoto ili wamchukie baba yao ili hapo baadaye afaidi matunda ya watoto peke yake. Wanaume wengi wanawajali watoto wao kwa kuweka picha zao fb tu, lkn ukichuguza au kufuatilia sana utakuta wababa hao hata matunzo hawatoi kwa watoto hao. Na ndio maana ni rahisi kwa mwanaume kumtelekeza mke na watoto wake lkn akampenda mwanamke mwingine ambaye mwenye watoto wasio wake.
 
Nadhani hata akinamama huamua kuinvest kwa watoto. Kuinvest kwa mke kunakuwa na risk kubwa kuliko watoto maana ni damu yako, hawezi kukuangusha jumla.

Hivi kuinvest kwa mke uliyefunga nae ndoa bado unaona ni risk taking? Kaaz kwelikweli
 
Back
Top Bottom