Wanaume, huu si uungwana hata kidogo

Wanaume, huu si uungwana hata kidogo

Habari za asubuhi.

Naomba niende moja kwa moja kwenye lengo langu.

Kuna baadhi ya wanaume wana tabia ambayo mimi binafsi sipendezwi nayo kwa hakika. Mwanaume anakuwa anathamini watoto kuliko mke wake aliyemzalia hao watoto. Sisemi msiwapende watoto wenu ila mjitahidi kubalansi.

Utaona mtu yuko bize na watoto tu, weekend anachukua watoto anawatoa out,kama ni zawadi wanapata watoto tu.

Hata akiweka picha facebook ni kuweka watoto mwanzo mwisho, huoni hata siku moja kaweka picha ya mkewe au walau aweke wanae pamoja na mama yao. Niliwahi kuona mtu ameweka picha facebook eti 'bon voyage my daughter' nikajiuliza hivi huyu mtoto wa mwaka mmoja anasafiri hadi
Mwanza peke yake? Hata ukiangalia kwenye visimu vyao vya tochi huoni picha ya mkewe hata moja.

Hivi kuna sababu zozote za msingi zinazowafanya muwe hivyo? Huyo mwanamke ndiye aliyewaweka tumboni miezi tisa hao watoto unaojivunia, akaenda leba na hatimaye na wewe ukapata cha kujisifia mbele ya wanaume wenzio.

Hivi bado hamjui kuwa kuna wanawake wanatoa mimba? Au hamjui kuwa kuna watu walichezea ujana wao hadi leo hawana uwezo wa kushika mimba? (siwazungumzii wale wenye matatizo ya uzazi yaliyotokea kwa bahati mbaya)

Sasa kinachokufanya usimthamini huyu mwanamke ni nini?

Huyo ndo mkeo...ulimchagua kati ya maelfu uliowaona...na hayo matunda unayoringia umeyapata kupitia yeye. Mthamini mkeo.

Be proud of her.
Ni hayo tu
NB:
Sisemi muweke picha zao ziwe profile picture.....ile kuonekana mnajali uwepo wao japo mara mojamoja inapendeza

Mchepuko bhana. Mbona hujanambia umeanzisha sredi nije kuchakachua????

Nikuambie kitu? Tunawapa zawadi watoto, tunawatoa out, tunawaweka kwenye profile..... kwa sababu kuna sehemu tunataka tuwaweke lakini nafasi imejaa. Mama yao kajaza nafasi kwenye moyo....

vyote navyopata kwa mama yao siwezi pata toka kwao... and vis versa.

btw hii inatokea kwa wababa tu? You sure?

İ love you.
 
Mh..akili yangu ya ki-teamB ikawaza wewe ni mchepuko wa watu flan flan ivi...

then akili ikarudi sawa nikajiuliza, hapo siku za nyuma niliwahi kusikia malalamiko haya, 'Mke wangu toka ajifungue, attention yote kahamishia kwa mtoto'

Hii ya leo ni mpya..ngoja niifanyie uchunguzi.

Kwa kifupi kabisa ungeandika "mkuki kwa nguruwe"
 
Mchepuko bhana. Mbona hujanambia umeanzisha sredi nije kuchakachua????

Nikuambie kitu? Tunawapa zawadi watoto, tunawatoa out, tunawaweka kwenye profile..... kwa sababu kuna sehemu tunataka tuwaweke lakini nafasi imejaa. Mama yao kajaza nafasi kwenye moyo....

vyote navyopata kwa mama yao siwezi pata toka kwao... and vis versa.

btw hii inatokea kwa wababa tu? You sure?

İ love you.

I love u too......nimeona hapo mwisho tu teh...
 
[Hata akiweka picha facebook ni kuweka watoto mwanzo mwisho, huoni hata siku moja kaweka picha ya mkewe au walau aweke wanae pamoja na mama yao. Niliwahi kuona mtu ameweka picha facebook eti 'bon voyage my daughter' nikajiuliza hivi huyu mtoto wa mwaka mmoja anasafiri hadi Mwanza peke yake?]...............Mmmmh mkuu hapa sasa unamsema pastor Peter Mitimingi.
 
Ndo nani huyo
 
Wanaume wengi ni wachepukaji hivyo hawapendi mahawara zao waone kama wanawapenda na kuwajali wake zao.maana wakiwa huko ughaibuni(nyumba ndogo) humwaga sifa mbaya za mke ili hawara aone anasababu ya kuwa nae kumbe wizi mtupu.

Haya ni ukweli uongo.
 
Sidhani kama mtoa mada ana wivu ulopitiliza, anachojaribu kuelezea ni kwamba haya mambo yawe na kiasi( too much is harm full).

Kama baba, anatakiwa kumjali mkewe na watoto pia, na si kuhamishia mapenzi yote kwa watoto.
ukiona mtu yupo hivyo basi ujue ndivyo alivyoumbwa na huo ndio utofauti wetu binadamu aidha mke ndani ya nyumba hasomeki/haeleweki ndo maana penzi linahama.....sasa si bora huyu anayehamishia penzi kwa watoto kulliko anayeamua kuchepukia pembeni.
 
Duuuh haya bwana....hujaelewa au unajilazimisha kutoelewa? Kuna mahali nimetaja profile hapo? Mi sijawaonea wivu maana sijaexperience hicho kitu.... Nimeona jinsi kaka zangu wajomba na rafiki zangu wanavyofanya nikaona sio vizuri
aaaah! kumbe hujaolewa bado?....what a miracle...lazima nikutafute.
 
Back
Top Bottom