Nataka nikupe kisa kimoja
Kuna jamaa alikua na wake wawili, mmoja ana mtoto na yule mwengine ambae ni mke mdogo hana mtoto. Si unajua mambo ya kijijini? Wake wote wanakaa nyumba moja,
Yule jamaa akienda kwa mke mkubwa anakua anacheka sana tena kwa sauti hadi mke mdogo anasikia, ila akija kwa mke mdogo anakua kawaida tu kile kicheko hamna
Hali hii ikawa ni kila siku hadi mke mdogo akaanza kuumia, ikapelekea kuanza kumuuliza kwanini ukienda kule unakua na furaha sana unacheka hadi huku nasikia?
Jamaa kajibu sicheki na mke mkubwa ninnakua bize na yule mtoto wangu, nikiwa nae nikiona mapengo yake yasio na meno hua nafurahi sana
Mke mdogo akaona isiwe shida, si kaenda kutoa meno? Kama shida yako mtu asiwe na meno sasa cheka na mimi