Wanaume + Housegirl: Pepo gani limeingia mioyoni mwenu?

Ndo kitu nampenda Aspirin,akishajua kosa anakuwa mkweli,anaomba msamaha na anamuomba mpenzi arudi.....keep that!
mpokee kwa mikono miwili.....................:smile-big::welcome:

Nasubiri uniadapti ujue..........
 
Nilikuwa natafuta cha kuandika, maana huu ni ukweli uaohuzunisha.
Unataka kugongwa nini??

Kwakuwa FL1 kagongwa na hausigeli wake kwahiyo tunakonkludi kuwa hausigeli naye kagongwa na jamaa nikimaanisha kuwa ukichukua velocity ya kugongwa bila kuwasha TV inaangalia ukuta na kuacha AC iko on ikiwa inapulizia TV na ukiwa umekusanya mizigo unajistukia umelala usiku wa manane peke yako basi kiwango cha kugonga na kugongwa sio kikubwa sana
 
Nadhani Mapenzi ni kitu tofauti sana na watu wanavyotafsiri!

1. Mapenzi Huwa Hayadumu!
2. Upendo huwa unadumu
3. Mapenzi huja ghafla na huondoka taratibu na yanaweza kurudi lakini huwa ni kama maua hayabaki na hali ile milele
4. Mapenzi hayana uhusiano na social or economical status yako, unaweza kufanya mapenzi na mwanaume au mwanamke mwenye sura na shape mbaya kuliko lakini duh mashine bomba sio mchezo umeme na msisimko mtindo mmoja upo hapo...

So kuoana ni kupendana sio mapenzi, mapenzi yanakuwa sehemu tu ya package yote, Upendo pekeyake ndo utadumisha ndoa. Na ukimfumania mwenzio sio mwisho wa ndoa, siajabu ndo changamoto ya kuweka mambo sawa...

Muhimu, usikubali HG/HB avunje ndoa yako... tena ikitokea hiyo ishu chuna dili na mwenza wako kimyakimya kama ni kibano au vipi then hakikisha ndoa haivunjiki unamshughulikia huyo mvamiaji fasta maana lazima mmoja wapo atakuwa amemleta, mnamtimua tu then mnajipanga upya...

Unaweza ukawa curious kujua mapigo ya huyo mwizi wako ili na wewe kama vipi unajifua...
 
Kwakuwa FL1 kagongwa na hausigeli wake kwahiyo tunakonkludi kuwa hausigeli naye kagongwa na jamaa nikimaanisha kuwa ukichukua velocity ya kugongwa bila kuwasha TV inaangalia ukuta na kuacha AC iko on ikiwa inapulizia TV na ukiwa umekusanya mizigo unajistukia umelala usiku wa manane peke yako basi kiwango cha kugonga na kugongwa sio kikubwa sana

The Finest hivi ni lugha gani inaongelewa hapa mkwe ..
Naomba tafsiri na si tafsida
 
FL1,.mi sikatai kwamba at times wanawake wanajisahau sana tu,.lakini taking this into a human point of view...Wanaume wangapi that wako soooo busy hata anasahau when was the last time alikua intimate na mkewe?lakini je asilimia ngapi ya wanawake wanaenda kutoka na mahouseboy?(ndogo sana right?)..if only marriage was built in a way that mwnaume atajishusha na mke nae ajishushe that akiona kuna mapungufu anaeza kumwambia mwenzake without kumnyanyasa in any way life could be better..mimi naamini it starts with the mentality kwamba i am a man and can do anything!.wanawake wengi wanavumilia all the lost attention unlike men..hivi najiuliza ukikaa na mke wako kwa ustaarabu ukamwabia what you feel,hatakuelewa kweli?na je ukimchukua hg then nae akaeka hg akajisahau pia..will you be changing hgs?..heshima kitu cha bure kwakweli,.hv imagine mtu unamvisha unamlisha,unamchukulia kama mdogo wako afu anatoka na mumeo?au ndo babaako kafanya hivyo?how will you feel?
 
Juzi nilikuwa katika semina fupi ya mambo ya ndoa ,kila mwanamke aliyekuwa akisimama ana-complain mahusiano mabaya ya mmewe na H/G
Mwisho wa mada yetu wakinamama waliokuwepo wakasema wanaamini 95% ya kina baba wanamahusiano na ma H/G

@ Mama wa kwanza alisimama na kulalamika mie nilishangaa mme wangu alipokinga kifua na kulazimisha msichana wao aongezwe mshahara huku akidai anataka aanze kumsomesha haraka iwezekanavyo na n kitanda kilichopo chumbani kibadilishwe wakati mwanzo mzee alikuwa anamuomba mama amuondoe alipofanya uchunguzi zaidi ndipo bomu lilipolipuka mme ( Mama anakula sahani moja na H/G

@ Mama wa pili alifuma msg za mmewe kwenye simu ya H/G maana binti alikuwa hajui ku-delete akamrudisha kwao baada ya muda akapokea taarifa binti yuko mjini tena kufanya uchunguzi kumbe mme kampangishia H/G mtaa wa pili baada ya kufukuzwa kwake

@ Mama wa tatu yeye aliona binti ana mimba alipomuhoji kwanza akamdanganya ni ya kijana House/Boy wa jirani na kwao ..Mama alipomfata H/B kijana akatoboa siri kuwa ni ya mmewe na kumpa evidence ya mmewe ,Binti kuulizwa akakubali huku analia na kuomba samahani

@Mama wa nne yeye akadai watoto wakitoka kwao wanafundishwa mbinu na wazazi wao kama wakifika wahakikishe wanakuwa na uhusiano na baba mwenye nyumba ili mambo yawe mtelemko katika familia yako na wengine wanasisitizwa wajitahidi kupalilia ili wao wakamate usukani.

Wazazi tunaelekea wapi hata kutoa ushauri huu kwa watoto wetu?

Mie Binafsi nashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya kina baba mnaamua kuwa na uhusiano na M/G wakati mnajua kabisa kitendo hiki kinamdhalilisha sana Firstlady wako hata kumfanya H/G aanzishe dharau na choko choko ndani ya nyumba???

I salute!

Wanawake wamepunguza kuwajibika. Unakuta hg anafanya mazuri (kazi mhimu za nyumbani) kuliko mwanamke. Fikiria house wife anayekaa hapo kibalazani anapakwa rangi kwenye kucha, hana kazi yoyote ila anataka apendwe na kuwekewa hg. Ukumgusa ata hamu hana. Wanawake pia wamepunguza nidhamu.
 
Ni kweli Pearl hata sisi wakati mwingine tunachangakia Lakini je Kama mme umeona mkeo ana mapungufu hayo kwanini msikae chini mkaongea kabla hujaamua kuleta maafa ndani ya nyumba?Kwani kuwa na mahusiano na H/G ndio suluhisho la haya matatizo?

Siyo wanawake wote wakielezwa mapungufu yao wanayakubali na kubadilika, anaweza kuendeleza matatizo.
 
Back
Top Bottom