Usithubutu kufanya haya unapokuwa ugenini/ ukweni

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,891
Haya Ni Baadhi Ya Mambo Ambayo Mgeni Ukiyafanya Ugenini Unachokwa Haraka Na Unaweza Kufukuwazwa Mapema👇🏼

1: Mgeni Kutozingatia Ratiba Ya Kula Yaani Chakula Kinaiva Haupo Hii inampa Shida Mpishi Kugawa-Gawa Yaani Amkatie Anayetafuta (mme) na akukatie Nawewe Usiye na Faida Hapo.

2: Mgeni Wakati Wa Kula Unakula Mpaka Unaachwa, Mgeni inabidi Uwe wa kwanza kushiba kabla ya wenyeji Hata Kama Hujashiba.

3: Mgeni Kuomba kijiko ili ukwangue mpaka ukoko Pale utakapobakishwa Kwenye kula na pengine ukaunywa kabisa na mchuzi uliyobakia

4: Mgeni Kukosoa Mapishi Mfano Chumvi ndogo, haitoshi au hakuna kabisa halafu ukasema Chumvi haitoshi, Mgeni inabidi unyamaze na ule Hivyohivyo Hata Kama Chumvi haitoshi.

5: Mgeni kumega matonge makubwa, kukomba mboga au kula harakaharaka kwa kufakamia

6: Mgeni kutojiongeza kufanya kazi ndogo ndogo za hapo Ambazo zipo ndani ya uwezo wako mfano.. kuchota Maji, kufagia Uwanja, kudeki, kupika..n.k...

7: Mgeni Kukoloma Usiku Ukilala

8: Mgeni Usiku Wakati Mmelala Usingizi ukikukolea Kutotulia Upande wako Wa Kitanda unajigeuza geuza mwanzo mpaka Mwisho wa kitanda, sometime mpaka Unakuwa unarusha guu lako Unawakandamizia kwa juu mpaka shingoni ulolala nao Kama Ni watoto wanaamka Migongo inawauma Wanakandwa mpaka Maji ya Moto Yaani unajisahau Kama uko Ugenini na umelala na wenzako

8: Mgeni Kuchelewa Kuamka Wenyeji wanaamka Saa 1 tu Asubuhi Wewe unalala mpaka saa nne wenzako mpaka wanamaliza kufanya kazi ndogo ndogo ndo unakuja Kuamka.

9: Mgeni Kukojoa Kitandani.

10: Mgeni Kutongoza au kedeshideshiana na Mtu wa hapo eidha Binti, Kijana, mme, Mke.n.k.

11: Mgeni Kudakia Dakia Ugomvi Mme na Mke Wanapogombana Mfano mke alitaka aende Sehemu sasa mme anamsema na anamkataza mke wake kuwa👉 hakuna Kwenda,, Halafu nawewe Mgeni unadakia Yaani anadhurula Huyu👉.

12: Mgeni Kuchukiwa na Mama Mwenye Mji kutokana eidha hafurahishwi na Mambo yako, kumbuka Ugenini Bora uchukiwe na baba mwenye mji, au Watoto wa hapo Ila usiombe uchukiwe na Mama Mwenye Mji kumbuka huyo ndo Mpishi Baba Yuko Kazini Mgeni Utalazwa njaa mpaka ukome,
👇🏼
Tena mama wa mji anaweza kumshawishi mmewe au akakutengenezea tukio ukafukuzwa, Mgeni inabidi jitahidi akupende Mama Mwenye Mji hapo Uta,Enjoy

12.

13.

14.
 
  • Mgeni anagombea vipande vya nyama na watoto wa mwenyeji wake.
  • Mgeni anajinunisha ugenini.
  • Mgeni anatoa vijiamri kwa wenyeji k.m apelekewe maji bafuni au sauti ya teevee iongezwe/ipunguzwe kadiri ya matakwa yake.
  • Mgeni anakuwa bosi ugenini hadi anawapiga watoto wa mwenyeji wakipotoka ...
 
Mnaendaje kusalimia kwa watu mkafikia kwao?

Ivi na umri huu naenda kumsalimia mtu halafu nalala huko..!!?

Hapa huwa tunagombana sana, huwa naonekana kwa namna fulani. Sehemu pekee ambapo nikienda kusalimia nafikia hapo hapo ni nyumbani nilipozaliwa na kijijini, kwenye asili yetu. Sehemu nyingine zote, huwa nafikia malazi ya mfukoni halafu nakwenda kusalimia nimtakae na kurudi nilipofikia.

Kwenye utu uzima ni ngumu sana kublend in kwenye taratibu zote za nyumba ya watu, utakwazika au utakwaza.
 
Cha msingi tujitahidi tuwe na pesa hayo yote mgeni mwenye mkwanja hana haja ya kuzingatia. Na utapewa uangalizi mzuri siku ulizopo ugenini
La muhimu si mgeni kuwa na mapesa.Hayo ni yake.Anapaswa kuwa mtulivu,muangalifu,achague maneno ya kuongea na kujibu bila kusahau kutii mamlaka ya "nchi" aliyofikia ugenini.
 
Back
Top Bottom