Wakati nipo chuo mwaka wa kwanza, Kuna siku nilipigiwa simu, namba mpya, alikua ni baba yangu mdogo ambae ndio wa mwisho kuzaliwa kwa kina baba, kipindi hicho kiumri alikua early 30's.
Akaniambia Mimi baba yako mdogo nipo Dar kikazi nimefikia hoteli Fulani nataka nikuone tusalimiane nimeambiwa upo chuo dar, Basi nikamwambia sawa nitakuja siku Fulani Sina kipindi.
Nilivyomaliza kuongea nae nikampigia baba simu nikamwambia bamdogo Fulani kanipigia kaniambia yupo dar anataka kuniona siku Fulani.
Baba kwanza alikaa kimya muda mrefu halafu akaniambia usiende, ikifika hiyo siku uliyosema utaenda mwambie upo busy aje hosteli kukusalimia, akikulazimisha uniambie, kwa kipindi kile nilishangaa nikaona mzee mbona kawaza mbali Sana huyu si sawa tu na baba yangu, lakini nilitii ilivyofika siku sikwenda hotelini na bamdogo akasema hawezi kuja hosteli nikamwambia haya tutaonana wakati mwingine.
Huwa najiuliza mzee sijui aliwaza nini.