Hii ni kweli imenitokea

fleha

Senior Member
Oct 9, 2014
111
103
Tulikuwa ndo kwanza tumeingia chuo ila tayari nilikuwa nimefanikiwa kupata marafiki kadhaa wapya.
Wengi wa marafiki zangu walikuwa watoto wa kimji na wengi wao walijiona wajanja kuliko mimi. Kitu kilichokuja kunipa heshma ni uwezo wangu darasani hasa katika somo la hesabu ambalo lilikuwa tatizo kwa wengi.
Wiki kama ya tatu hivi baada ya kuwa tumedumu katika masomo ndipo akatokea binti mmoja mrembo sana na kuzuzua wavulana karibu wote pale darasani. Kwangu mimi ilikuwa tofauti kidogo maana nilikuwa nimeyapuuza masuala ya mapenzi baada ya kuwa yameniletea usumbufu kipindi cha hapo nyuma, hivyo sikuwa nikiwaangalia watoto wa kike kwa jicho la kuona.
Baada ya muda mfupi yule binti alikuwa kwenye midomo ya wavulana wote, kila mara alitajwa na kila mmoja alionesha kutamani kupata angalau wasaa wa kujuana naye, ila ilisemekana aliuwa na maringo sana, wachache walijaribu kumsogelea waliishia kuumbuka, hakuonekana kutaka hata urafiki na yeyote kati ya wavulana wale.
Miongoni mwa waliokuwa wametekwa na kumuhitaji binti yule waliuwemo wale rafiki zangu, kila wakati walikuwa wakizungumza kumuhusu huku kila mmoja akijaribu kumuonesha mwenzie kuwa yeye ndiye alikuwa na nafasi kubwa ya kumpata kuliko wengine, ilifikia mahali na mimi wakanifanya kumuangalia kwa karibu binti yule, kweli alikuwa ni mrembo sana, na alionekana anatokea kwenye familia ya kitajiri kutokana na vitu ambavyo alikuwa anamiliki, mwanzo sikuvutiwa naye ingawa niliona kuwa alikuwa mrembo, nadhani ni kutokana na kuokuwa na uhitaji wa masuala ya mapenzi kwa wakati ule (mapenzi yalikuwa yamenifanya vibaya sana).

Siku moja rafiki zangu wale walikuwa wakishawishiana kujaribu kumfuata binti yule kwenda kumuomba namba yake ya simu, lakini hakuna ambaye alikuwa tayari kwenda kupata aibu, kwani alikuwa anajulikana kwa kuumbua. Kila mmoja akawa anajaribu kumshawishi mwenzake aende, ila hakuna ambaye alikuwa akinishawishi mimi kwenda, kila mmoja alikuwa anajua kuwa mimi sikuwemo kwenye mpambano ule.
“hivi kweli mtu akutukane kwaajili ya kumsalimia tu?, nyie waoga tu, hawezi kuwatukana bila kumkosea” kwa mara ya kwanza nilichangi yale mazungumzo yao. Rafiki zangu wale walishangazwa kuona na mimi naongelea swala lile, mmoja wao akaniuliza kama mimi sina uoga kwanini mimi siendi, nikamjibu kuwa siendi kwakua sihitaji namba ya binti yule kwakuwa simuhitaji, wote wakacheka na kusema kuwa sio kweli kuwa simuhitaji bali ninajua fika kuwa siwezi kumpata, yule rafiki yangu ambaye aliuliza kwanini mimi simfuati binti yule aliuwa karibu na mimi zaidi ya wale wengine, na alikuwa anajua mimi simuwa mtu wa kuogopa ninapotaka kufanya jambo, hivyo alioneana kushawishika, akanitaka kwenda kuchukua ile namba kisha nimletee yeye, akaniahidi kunipa kiasi kikubwa cha pesa kama ningefakikisha.
Sikufikiria mara mbili, nikainuka na kwenda moja kwa moja mpaka binti yule aliyekuwa amekaa na mabinti wengine kwenye vimbweta kwakijisomea kwaajili ya mtihani ambao tulikuwa nao siku chache kutoka siku ile. Nilipofika pale niligundua mabinti wote alikuwa wakijadiliana kasoro yule binti ambaye nilimfuata pale, waiponiona tu mabinti wale wakanitaka kuwasaidia swali ambalo lilikuwa limewasumbua kwa muda mrefu, kwangu swali lile lilikuwa rahisi sana, nikalifanya mara moja na kuacha mabinti wale wakinimwagia sifa kedekede, kisha nikaachana nao na kumuendea binti mlengwa ambaye alikuwa amejitenga kidogo, nikamsalimia na akaitikia vizuri tu, nikamuuliza kwanini aliuwa hajadilini na wenzake, akanijibu kuwa wenzie walikuwa wanasoma hesabu, somo ambalo alikuwa haliwezi hata kidogo na alikwishakubali kuwa atalifeli, hivyo ameamua kuutumia muda wake kusoma somo lingine ambalo ana uhakika wa kulifaulu.
“hesabu sio ngumu, ni kutoipa muda wa kutosha ndo kunatuangusha” niljaribu kumshawishi, akaonekana kupata moyo kidogo kisha akasema angetamani kama angempata mtu anayejua kama mimi ili awe anamfundisha, nikamwambia mimi nilikuwa tayari kumfundisha, akanipa simu yake na kunitaka kumuandikia namba yangu, kisha akanibeep na mimi nikapata yake, akaahidi kunipigia baadae ili tukutane kwaajili ya kuanza kumfundisha. Nikaondoka na kuwarudia wale rafiki zangua ambao walikuwa wakiangalia kwa makini kilichokuwa kikiendelea, ingawa hawakuweza kusikia maneno.
Nilipofika nilimpa namba yule rafiki yangu aliyeniagiza, akanipa pesa yangu palepale, tukachana.

Siku ya pili nikiwa nimeshau kuhusu makubaliano yangu na yule binti, akanipigia simu na kuniuliza juu ya ratiba yangu ili kama nitakuwa na muda wa ziada nimfundishe, nikampangia muda ambao tulikutana na nikamfundisha vizuri tu. Kitu cha ajabu ni kuwa hakuwa mjinga kama ambavyo nilimdhania, kila nilipompa swali baada ya kumfundisha alipata. Baada ya kipindi akanishukuru sana na kunitaka niwe namfundisha kila siku, alidai kuwa hakuwahi kupata mwalimu mzuri kama mimi na anatamani angenijua mapema maana hesabu isingekuwa imemtesa namna ile.
Basi ukawa utaratibu wa kawaida, tunakutana namfundisha, tunapiga story, tunacheka na alikuwa mcheshi sanaaaa, nikajikuta namzoea na kufurahia sana kampani yake. Hata wale marafiki zangu wakajikuta wamekuwa karibu naye sana maana tulikuwa pamoja muda mwingi, wakati wote huu wawili kati ya wale rafiki zangu walikuwa wakishindana kumvutia lakini mtu wake wa karibu nilikuwa mimi kwa wakati huo maana alikuwa huru sana kwangu na aliuwa akinipa vizawadi vya hapa na pale, na wakati mwingine alikuwa akishtaki kwangu pale ambapo mmoja wa marafiki zangu alimkera, ila wakati wote nilikuwa nikimsihi kuwavumilia na muwapuuza wanapoongea mambo ambayo aliuwa hayapendi, na mara zote alikuwa ananielewa.
yule rafiki yangu ambaye nilimpa namba alikuwa anapenda sana kumvutia msichana yule kupitia pesa, kwakuwa yeye likuwa akikaa nyumbani (tofauti na sisi ambao tulikuwa tunakaa hostel pale chuo), alikuwa akija na gari jipya kila siku, na alihakikisha binti yule anayaona, alikuwa akimpa pesa mara nyingi sana lakini mara zote binti yule alikuwa anachukua ila tukiwa pekeyetu alikuwa ananipa mimi.

Siku moja baada ya kuwa tumemaliza kusoma na binti yule akaondoka, alinipigia simu akinitaka tuoane, nami nikaitikia wito na kwenda kukaa naye eneo tulivu, akaniambia kuwa alikuwa anataka tupige story tu kwa maana alikuwa anajihisi upweke, nami sikuwa na hiana, nikakaa na kupiga naye story za hapa na pale, mara akaniuliza kama niliuwa tayari kuulizwa maswali ya maisha yangu binafsi nikamwambia anaweza kuuliza tu, akaniluliza kama nilikuwa na mpenzi nami nikmjibu kuwa sikuwa na mpenzi, akaonesha kutoamini, akauliza kwanini sikuwa na mpenzi nikamwambia ni story ndefu sana ila akanitaka kumuhadithia. Nikamuhadithia namna mapenzi yalivyokuwa yamenitesa, akasikitishwa sana na simulizi ile kisha naye akanihadithia jinsi mapenzi yalivyokuwa yamemfanya, naye alikuwa ameumizwa sana na mpenzi wake ambaye bado alikuwa naye kwa mazoea tu ila hakuwa na mapenzi naye tena.
Nilimpa pole na kumtaka kufanya maamuzi ambayo yataupa furaha moyo wake. Ghafla binti yule akanitamkia kuwa ananipenda na anatamani kuishi na mimi maisha yake yote yaliyobakia. Sikushangazwa na suala la yeye kunipenda maana tayari nilikuwa nimelihisi, ila nilishangazwa kuona akitamka kuwa nananipenda, hakuonekana kama binti ambaye anaweza kumtamkia mwanaume kuwa anampenda, nilishikwa na bumbuwazi kwa sekunde kadhaa, sikujua hata nisema nini. “najua nitajutia maisha yangu yote kukutamkia neno kama hilo, ila nimeshindwa kuvumilia, nimengoja sana wewe useme ila nimegundua kuwa mwenzangu huna hisia juu yangu” alijitetea binti yule baada ya kuona sijibu chochote.
“sijawahi kumtamkia mwanaume yoyote kuwa nampenda ila kwako nimeshindwa kuvumilia” alizidi kujieleza binti yule. Kiukweli nilikuwa natamani kumwambia msichana yule kuwa nilikuwa tayari kuanza mahusiano naye ila niliwaza kuhusu yule rafiki yangu ambaye alikuwa akimtaka binti yule kulio nilivyokuwa nikimtaka mimi, nikajizuia na kumwambia msichana yule kuwa tuliongelee siku nyingine swala lile. Msichana yule akakubali, alikuwa anaona aibu sana, akataka tuondoke eneo lile, tukaondoka.

Kesho yake rafiki yangu alipokuja chuo alikuwa tofauti sana, hakuja hosteli kunifuata kama ambavyo alikuwa akifanya siku zote, nilimkuta darasani lakini hakunichangamkia na akawa ananiepuka kila nilipotaka kuwa karibu naye, mpaka siku ikaisha akarudi nyumbani. Jioni nkamtumia ujumbe kutaka kujua kulikuwa na tatizo gani, akanijibu kuwa alikuwa na matatizo ya kifamilia ambayo yalikuwa nayamfanya asichangamke, niakubaliana naye ingawa nilijua haikuwa kweli. Hali ile ikaeendelea siku zilizofuata, baadae nikawaza kuwa huenda binti yule alimwambia kuwa alikuwa akinipenda mimi, hivyo nikamuelezea hali halisi na kumuuliza kama amehusika kwa namna yoyote, binti yule akakili kuwa bwana yule amekuwa akimtongoza ila amekuwa akimkataa laikini hakuwa amemwambia chochote kuhusu mimi.
Baadae mmoja wa marafiki zetu ambaye nilikuwa nikikaa naye pale hostel akaniambia jamaa alikuwa akilalamika kuwa nimempora mpenzi, kumbe kuna mtu alikuwa akimtonya anaponiona nikiwa nimekaa na yule binti pekeyetu, naye akaamua kuhitishisha kuwa tulikuwa wapenzi. Maneno yale yalinikera kwakuwa nilikuwa nimempenda binti yule tayari lakini nilikuwa najizuia kwaajili ya rafiki yangu.
Nikaamua kuwa kesho yake ningemtafuta ili tuongee aweze kujua nini kilikuwa kinaendelea. Kesho yake nikaonana naye darasani ila kama kawaida alikuwa ananiepuka, nikaamua kuwa tukitoka nitaongea naye.
Tulipokuja kutoka, matokeo ya mitihani ambayo tulikuwa tumefanya yaliuwa yametoka, hivyo sote tukaelekea kwenye ubao uangalia tulichokuwa tumefanya.
Wakati nafika kwenye ubao ule nikamuona yule binti alikuwa amefika kabla yangu, baada ya kuona matokeo yake akalipuka kwa furaha, nilipofika akanikumbatia kwa nguvu, hakuweza kuficha furaha yake. Alikuwa amepata B ya hesabu, somo ambalo alitegemea kupata F.
Nilipotoka kwenye kumbatio lile nikamuona yule rafiki yangu ambaye sasa alikuwa ananiona adui, akiwa anatuangalia na niwazi kuwa hakupendezwa na alichokuwa anakiona. Nikaangalia matokeo yangu ambayo yalikuwa mazuri sana, kisha nikajitenga na kumsubiri rafiki yangu yule amalize kuangalia yake ili tuongee.
Alipomaliza akaondoka nami nikamfuata huku nikimuita, “ACHANA NA MIMI” rafiki yangu yule alitoa jibu lile kwa sauti kubwa mpaka walokuwa karibu wakageuza shingo zao kutuangalia. Nilijiona kama nimeahibishwa sana, nikachukia na kuamua kuachana naye, niliona fika kuwa nilikuwa nimempoteza rafiki.
Baada ya kutoka pale binti yule alinitumia ujumbe akinitaka jioni ya siku hiyo tutoke kwaajili ya kujipongeza. Sikuona haja ya kujizuia kwa lolote kwa maana ambaye alinifanya kujizuia sikumuona tena kama mtu mwenye umuhimu kwangu, na tayari moyo wangu ulikuwa umempenda sana binti yule.
Hivyo jioni ya siku hiyo tukatoka, ilikuwa siku nzuri sana, siku ya kukumbukwa, tulijikuta tayari ni wapenzi ningawa sikuwahu kumjibu kuwa niliridhia kuwa mpenzi wake, tulikuwa huru sana kiasi kwamba mara kadhaa tulikiss njiani, mbele ya macho ya watu kama ulaya vile, hata hatukujali. Siku ile tulilala pamoja hukohuko tulikokwenda kutembelea na kwakweli ulikuwa ni usiku wa kupongezana.
Penzi letu likaanzia hapo, tumepitia changamoto nyingi mpaka leo, muda hautoshi kuzielezea ila bado tuko pamoja na tunatarajia kufunga ndoa mwezi wa 8 mwaka huu.
 
mie nikisiaga story kama hizi nakumbuka demu wangu nileyoporwa chuo kipindi hicho...nashukuru yalishapita na maisha yanakwenda kama kawa
 
Sasa Je Mimi nikikupa stori ya demu aliyekosea chumba cha gesti akaja kwangu na nikamuoa patakalika hapa?
 
Back
Top Bottom