Wanaume hawaoi sura tena bali uelewa…!

Wanaume hawaoi sura tena bali uelewa…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
Lauren-London.jpg

Siku za nyuma, wanaume walijali zaidi uzuri wa sura na mwili wakati walipokuwa wanatafuta mke. Lakini utafiti uliofanywa duniani kote unaonesha kwamba, wanaume hivi sasa wamebadili mitazamo na kuanza kuangalia vitu vilivyo zaidi ya uzuri wa sura na mwili.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Grand Valley kilichopo jimboni Michigan nchini Marekani walioendesha sehemu kubwa ya utafiti huo wamesema, wanaume hivi sasa wameanza kujali uwezo wa wanawake katika kufikiri na kujua namna ya kujenga maisha kuliko kujali sura zao na maumbile.

Tafiti nyingi, ukiwemo huo wa karibuni wa Chuo cha Grand Valley, zinaonesha kwamba, kwenye miaka hadi 1980, wanaume walikuwa wakioa wake ambao wanaume hao wanawazidi kielimu na hata kimapato. Lakini kufikia mwaka 2002, wanaume wengi walikuwa wameoa wanawake ambao wanawazidi kielimu, kimapato au kukaribiana.

Lakini pia imebainika kwamba, hadi kufikia miaka hiyo, wanaume na jamii nyingi zilikuwa zikimtazama mwanamke anayefaa kuolewa kuwa ni yule mzuri sana kwa sura na umbo. Lakini kufikia mwaka 2002, wanaume wengi na jamii walikuwa wanaamini kwamba, mwanamke mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa maisha ndiye anayefaa kuwa mke.

couple5-e1285430787670.png

Kwa miaka ishirini hali imebadilika sana. Maisha yamezidi kuwa magumu na uhitaji wa watu kusaidiana katika kuyakabili umeongezeka. Kwa hiyo mtu anapofikiria kuoa huanza kujiuliza atakavyomudu maisha na mke. Kwa hofu za kushindwa, hujikuta akijiuliza namna atakavyoweza kusaidiana na huyo anayetaka kumwoa katika kufanya mambo yaende.

Siku za nyuma, mwanamke mwenye kipato kizuri alikuwa katika ugumu wa kupata mume, lakini siku hizi, bila kujali sura au sifa nyingine, uhakika wa mwanamke kuwa na njia za kipato unampa, nafasi kubwa zaidi ya kuolewa. Kilichokuwa kinaogopwa huko nyuma na wanaume kwa sasa ndicho kinachokimbiliwa.

Tafiti hizo zinasisitiza kwamba, thamani ya mwanamke kwenye jicho la mwanaume inaanza kuondoka kwenye uzuri wake wa sura na mwili na kuingia kwenye uwezo wake katika kuyakabili maisha. Hii ikiwa na maana kwamba, kwa kadiri siku zinavyoenda, wanawake ambao watakuwa na nafasi kubwa ya kuolewa watakuwa ni wale waliosoma au wale wenye shughuli za kuzalisha.

Black_woman_working_in_home_office_BLD078386.jpg

Wataalamu wengi wanasema, hivi sasa uzuri unaonekana kabisa kubadilishana nafasi na elimu na uwezo wa ‘kutafuta maisha' wa mwanamke. Kwa hiyo, sasa siyo suala la uzuri tena, bali mwanamke anajua kitu gani na ana uwezo kiasi gani wa kufanya maisha yawe bora sana.

Hii pia ina maana kwamba, dhana ya zamani ya mwanamke mzuri kuolewa na mwanaume msomi au mwenye fedha imeanza kukosa mashiko. Siku za nyuma mwanamke mzuri sana, angeolewa na mwanaume mwenye fedha, kama zilivyo bidhaa nzuri kuangukia mikononi mwa wenye uwezo kifedha.

Lakini leo hii, wanaume wanachoweza kufanya ni kuwachezea kimapenzi wanawake wazuri na siyo kuwaoa. Linapokuja suala la kuoa, kisomo na uwezo wa kuyajua maisha huchukua nafasi. Uzuri wa sura hubaki nyuma kwanza.

Copy to: Nivea, Madame B, Asnam, Smile, Lisa, lara 1, farkhina, Purple, Mrembo by Nature, Jeska, vivian, Paloma, amu, marejesho, Preta, Nyamayao, florence, Kaunga, mwaJ, Swts
 
Last edited by a moderator:
huo ni ukweli usiopingika ingawa nakupinga kidogo kwenye uzuri wa mtu wapo wanawake warembo wanaojua nini wanakifanya na nini wanahitaji kwao urembo ni nyongeza,bora umeweka wazi kwamba ni mamtoni ndo wamebadili mwelekeo,hapa kwetu mbado sana zaidi sana ukiwa juu utaambulia kuwa kiburudisho,mfano hapa jf kila kukicha utasikia oooh wanawake wasomi...........ooooh wanawake wenye pesa...........,naomba siku moja unifafanulie ule usemi wenu ''fulani ni wife material,lakini fulani ni wa kutumia then unasepa'' utakuta huyo mtu wanaesema ni wakutumia unasepa ni mrembo kajaaliwa idara zote lakini vijana wanamuona sio wife material,hope you will do so father.
 
kweli lakini loo utakuta ana mchumba very beautiful ila anamwaga anakuja kuoa kituko
na yule beautiful onyinye anabaki anatangatanga

Hahahahaha umenitoa machozi kwa kicheko
 
hiyo picha ya kwanza nilikupa uniwekee kwenye frame we umekuja kuitundika jf,ujue uache sifa zako umeshazeeka baba.
 
huo ni ukweli usiopingika ingawa nakupinga kidogo kwenye uzuri wa mtu wapo wanawake warembo wanaojua nini wanakifanya na nini wanahitaji kwao urembo ni nyongeza,bora umeweka wazi kwamba ni mamtoni ndo wamebadili mwelekeo,hapa kwetu mbado sana zaidi sana ukiwa juu utaambulia kuwa kiburudisho,mfano hapa jf kila kukicha utasikia oooh wanawake wasomi...........ooooh wanawake wenye pesa...........,naomba siku moja unifafanulie ule usemi wenu ''fulani ni wife material,lakini fulani ni wa kutumia then unasepa'' utakuta huyo mtu wanaesema ni wakutumia unasepa ni mrembo kajaaliwa idara zote lakini vijana wanamuona sio wife material,hope you will do so father.

Wewe Asnam hujasoma mada ukaelewa, nadhani umeishia kusoma heading. Hebu rudia tena kusoma kwa utuvu.....
Siku nyingine uki-comment uzi wangu namna hii nakuchapa, sijakupeleka shule kukariri majibu, bali kutafakari na kufanya upembuzi yakinifu.... LOL
 
Last edited by a moderator:
Wahenga walinena ya kwamba (Uzuri wa mwanamke si sura bai ni tabia)

Sisi wa enzi hizi hatuna muda wa kuangaliana kitabia tunapendana ghafla na tunaachana ghafla
 
Wewe Asnam hujasoma mada ukaelewa, nadhani umeishia kusoma heading. Hebu rudia tena kusoma kwa utuvu.....
Siku nyingine uki-comment uzi wangu namna hii nakuchapa, sijakupeleka shule kukariri majibu, bali kutafakari na kufanya upembuzi yakinifu.... LOL

nimeuelewa uzi wako lakini mie nimetuma maombi unisaidie kunitafutia majibu ya maswali niliyokuuliza hapo juu hayahusiani na mada ya leo,usipanic mzee
 
Hahahahahahaha
hakuna kituko uzuri wa mtu machoni mwake!
kweli lakini loo utakuta ana mchumba very beautiful ila anamwaga anakuja kuoa kituko
na yule beautiful onyinye anabaki anatangatanga
 
Hahhaahaa Mpwa umerudi tena eeeeh, haya bhana sitaki kujitia mjuvi kwenye hili Mamaaaa Elli asije akaona akaninyima bureee, naogopa mie kusema
 
Ngoja nitamtizama kwa karibu Mamaaa Elli ikibidi nitaweka picha yake hapa jamvini mtoe maoni yenu, si kwa kumtamani tafadhali (ntapiga mtu BAN)

Unajua tatizo ni kwamba akina dada warembo (sio wote) huringia urembo wao kwa wakati wao (ua likiwa limechanua) wakisahau kuwa umri unawatupa upesi, wakija kushtuka it is too late na wazuri wengine wameshazaliwa...it pains unamuona dada mzuri lakini hana mume kama huyu ninae chat nae huku sasa hivi kwenye Kitabu sura chANGU, ngoja nimkopie hii mada
 
Aaaaaaaaah wapi! Inategemea na level ya uchumi ya huyo mwanaume!

1. Maskini na Malofa mjini hapa awajue nani ndo wanaoa uelewa na hawajali sura out of insecurity ya kuwaza nikifilisika atanikimbia, watanigongea Vicious cycle of Poverty tu inawasumbua.

2.Maskini wasomi wale white collar jobs, na 9-5 hour clock life wanaoa shule na kazi za wife to be, sura sio ishu. Woga tu wa kugeuka Malofa mjini hapa afu ukizingatia wamesoma ni balaa mara 3

3.Matajiri shule less a.k.a Ma Lodi wa Kitumbini na Kkoo laki si pesa millioni deni, mjini mipango shule viboko tu. Hawa wanaoa Vitu vya ukweeee ila shurti visiwe na shule kabisaaaa. Mambo ya mzungu yes yes kalamba makamasi hawayatki kabisaaaa. Ila Mkewe wanataka awe Muke ya Bosi wowowo la haja, na wanapenda zaidi shombe shombe a.k.a Udongo wa Dubai!

4. Big Boys Doin Big Thins in Town. A.k.a Nshomile kashika hela. Wale wenye makampuni yao na shule zao za Haverd nini, Cambridge sijui. Weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Hapo inabidi Mdada awe Kisu cha hatari Sura sura kweli na shepu shepu la show stoppin na Masters tano tano. Sio mutu ya mchezo. Anataka ile akisema this is my wife iwe = F. You all!!! Hakuna anaebisha! Na hawaoi hadi wagonge 40. Mpambano wa kugombea ndoa unamuacha Baby dady wa wadada kibao! Kuna mmoja nilimuweka kwenye kumi na nane zangu Mkinga yule ila kina kirefu nimechemkaaaa! Nimejiweka pembeni kuepusha msongamano.

So transition ya kiuchumi baada ya ndoa ndo zinaleta mtafutano coz mtu anaanza ile kukuona sio size yake flani. He could have done better than you!!!!!!!!!

Na wanawake nao wana grade zao, ila kwa leo tuishie hizi za wanaume.
 
kweli lakini loo utakuta ana mchumba very beautiful ila anamwaga anakuja kuoa kituko
na yule beautiful onyinye anabaki anatangatanga

Kimbembe Genetics hapo inakuja kuogomba! Mitoto sura nzitooo kama Lara1. Sijui wanawazaga nini? Badala angechukua Beauty Onyiye msafishie damu!!!!!!!!!!
 
Interesting......
Kuna mzungu mmoja alisema yeye haoi peace of furniture (mdada mrembo) bali mtu ambaye wataelewana na kuendesha maisha.
 
::
Mtambuzi
Umenikumbusha mbali hata mimi niliwahi kufikiri mwanamke sura,
yaliyonipata hata maiti siwezi kuisimulia.
Thanks
=
 
Last edited by a moderator:
Kwa hapa nchini kwetu mwanamke kipato kikubwa ni asilimia kubwa, kupata mvulana au mwanamme ambaye anataka kulelewa na kudoea huku anaingia kwa gia ya juu ma love love huku pembeni ana mtu anayempenda kwa moyo wake wote.
Kwa hiyo mke anaishia kuwa kama wakuchumwa na kusaidia maisha ya mwanamme nae ajijenge na kusaidia wa kwao.
 
Aaaaaaaaah wapi! Inategemea na level ya uchumi ya huyo mwanaume!

1. Maskini na Malofa mjini hapa awajue nani ndo wanaoa uelewa na hawajali sura out of insecurity ya kuwaza nikifilisika atanikimbia, watanigongea Vicious cycle of Poverty tu inawasumbua.

2.Maskini wasomi wale white collar jobs, na 9-5 hour clock life wanaoa shule na kazi za wife to be, sura sio ishu. Woga tu wa kugeuka Malofa mjini hapa afu ukizingatia wamesoma ni balaa mara 3

3.Matajiri shule less a.k.a Ma Lodi wa Kitumbini na Kkoo laki si pesa millioni deni, mjini mipango shule viboko tu. Hawa wanaoa Vitu vya ukweeee ila shurti visiwe na shule kabisaaaa. Mambo ya mzungu yes yes kalamba makamasi hawayatki kabisaaaa. Ila Mkewe wanataka awe Muke ya Bosi wowowo la haja, na wanapenda zaidi shombe shombe a.k.a Udongo wa Dubai!

4. Big Boys Doin Big Thins in Town. A.k.a Nshomile kashika hela. Wale wenye makampuni yao na shule zao za Haverd nini, Cambridge sijui. Weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Hapo inabidi Mdada awe Kisu cha hatari Sura sura kweli na shepu shepu la show stoppin na Masters tano tano. Sio mutu ya mchezo. Anataka ile akisema this is my wife iwe = F. You all!!! Hakuna anaebisha! Na hawaoi hadi wagonge 40. Mpambano wa kugombea ndoa unamuacha Baby dady wa wadada kibao! Kuna mmoja nilimuweka kwenye kumi na nane zangu Mkinga yule ila kina kirefu nimechemkaaaa! Nimejiweka pembeni kuepusha msongamano.

So transition ya kiuchumi baada ya ndoa ndo zinaleta mtafutano coz mtu anaanza ile kukuona sio size yake flani. He could have done better than you!!!!!!!!!

Na wanawake nao wana grade zao, ila kwa leo tuishie hizi za wanaume.
Beauty is in the eyes of beholder..Ukisema mbaya mwingine ndio amemzimia..Na Kitu kingine watu huwa wana sehemu maalumu wanapenda hasa wanaume..Mtu anaweza kuangalia makalio tu au akampendea mwanya na mengine asiangalie..
 
Back
Top Bottom