Wanasiasa Vibaraka wana cha kujifunza kwa Mobutu Ssese Seko

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,907
2,769
Asalamalakum,

Nchi yetu imebarikiwa kuwa na resources nyingi sana ikiwemo dhahabu, gas, ardhi, strategic location na amani, hivi ni vitu muhimu sana kwa watu wanaotaka kujiendeleza kiuchumi, unfortunately kumekuwa na "scandals" kadhaa za wanasiasa kuuza rasilimali za taifa kwa wawekezaji bila kuzingatia maslahi mapana ya taifa. Mgogoro uliokuwepo na makampuni ya kuchimba dhahabu ni kielelezo tosha cha aina ya wanasiasa tuliona. Mikataba waliyoingia haikuzingatia maslahi mapana ya taifa bali maslahi yao binafsi.

Nchi yetu inaongezeka idadi ya watu na vijana wengi hawana ajira sababu ya uchumi kushindwa kutengeneza ajira za kutosha. Resources kama gas ingeweza kusaidia sana uchumi wa taifa lakini nayo kwa maneno yaliyopo na yanayosema tena na baadhi ya wanasiasa "gas" sio yetu. Swali ambalo mtu timamu unajiuliza, inakuwaje karne ya sasa tunakuwa na wanasiasa wa namna hii "WAHUJUMU"wa maslahi ya taifa? Mobutu kila mtu anajua alitumiwa na mataifa ya magharibi kuhujumu Congo, hadi leo resources za Congo zinaporwa huku yeye akiendelea "kuoza" huko kaburini.

Wanasiasa wanatakiwa kutambua hao wazungu wanaowatumia kuhujumu mataifa yao wanafanya hivyo kwa maslahi mapana ya mataifa yao, makampuni yao na vizazi vyao. Hatuwezi kamwe kujenga taifa endelevu kwa kuwa na wanasiasa vibaraka, Afrika inaachwa nyuma kwa kasi sana na mabara mengine, ni bara pekee lipo nyuma kwenye kila kitu sababu ya kukosa wanasiasa wenye maono. Hata wakiiba na kuhujumu itawasaidia nini zaidi ya ubatili? Watambue tu hizi resources ziliwekwa na Mungu kwa sababu maalum sio kusaidiwa wao pekee na familia zao, hata kama hawaamini Mungu yupo, ipo siku watajibu.

Pia ifikie sehemu vyombo vya dola viweze kutetea maslahi mapana ya taifa na sio kukaa na kuangalia wanasiasa wakigawa resources za taifa. Kila kilichopo iwe dhahabu, gas, ardhi, mbuga za wanyama ni mali za watanzania wote na sio kikundi cha wanasiasa waosisitiza tulipe kodi huku resources za nyingi hazitumiki ipasavyo kusaidia taifa kuondokana na umasikini.

Ni aibu kama taifa miaka 60 ya uhuru bado tunapewa misaada ya chakula mashuleni, tunachimbiwa matundu ya choo..miaka 60 ni mingi sana kuwa na matatizo ya namna hii.

Niliangalia video ya Jeffery Sachs akiuliza "what's wrong with you people" kwa lugha nyingine vichwa vyetu vina matatizo gani, alikuwa akiwauliza viongozi wa Congo, actually kwenye hiyo video ame admit CIA walihusika kumuuwa Patrice Lumumba, ni namna wazungu wanatuchukulia kama video dhaifu na tusiojielewa. Yote haya yanaletwa na vibaraka wa hao hao wazungu.
 
wana mema pia ya kujifunza,mfano Congo madini yanachimbwa na kampuni ya Taifa Gecami, Mobutu aliwafukuza wazungu kwenye madini akaweka wazaire na profit ilikuwa kubwa sana ingawa baadae mwishoni mwa miaka ya 90 wizi ulisababisha kushuka profit
 
Back
Top Bottom