Ni kweli anayedaiwa kuwa Mshauri wa karibu wa Hayati Mobutu Sese Seko ni ombaomba Kinshasa?

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka sintofahamu baada ya mtu mmoja aliyetambulishwa kama msaidizi wa karibu sana wa Hayati Rais Mobutu Sese Seko aliyekuwa mtawala wa Zaire (Congo DR), akiishi maisha ya dhiki sana mitaa ya Kinshasa huku akiendesha maisha yake kwa kuombaomba.

Kigogo huyo wa zamani ametambulishwa na baadhi ya mitandao/watu kwa majina ya Mutombo Kalombo na alikuwa na cheo cha Mshauri Maalum wa Rais Mobutu Sese Seko.

Moja ya mtandao wa kijamii umeandika "Picha: Aliyekuwa Mshauri Maalum wa Rais Sasa Amegeukia Ombaomba wa Mtaani."

Mwanamume huyo anayetambulika kuwa mshauri wa zamani wa Rais wa zamani Mobutu Sese Seko ameonekana mtaani Kinshasa akiomba pesa kutoka kwa raia wa kawaida'

Picha chanzo kingine kimepakia habari hiyo kikisema "From Grace to Grass; Nothing is Constant in Life. See The Advisor of A President Who is Now a Beggar"

Binafsi nimejaribu kuchimba makavazi mbalimbali lakini nimeshindwa kupata ukweli kuhusu taarifa hii.

Je, ni kweli huyu mwamba alikuwa mshauri wa Mobutu Sese Seko? Je, ni kweli ana maisha ya dhiki mpaka kuwa ombaomba mitaa ya Kinshasa?

3.png

Mutombo Kalombo kabla na baada


Picha kwa hisani ya mtandao
 
Back
Top Bottom