Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,555
- 41,067
Sifa mojawapo ya mtu mwenye kiwango kikubwa cha akili (High IQ), ni kuyaona mambo kabla hayajatokea.
Katika viongozi ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kuyaona mambo kabla hayajatokea, kwa Tanzania na Afrika ni Mwalimu Nyerere. Huyu mengi aliyasema ambayo wakati wake hayakuwepo lakini yalikuja kushuhudiwa baadaye.
1) Alizungumzia juu ya umuhimu wa kuweka taratibu ngumu za kumfukuza kazi mfanyakazi ili kuwazuia watawala au waajiri wababe, wanaoweza kukufukuza wakati wowote iwe kwa haki au uonevu, kwa vile tu wana madaraka. Kwa maneno yake Mwalimu alisema, "mkubwa anaamka tu kumwambia mfanyakazi, kuanzia leo huna kazi. Bwana mkubwa, nina watoto, nina familia, wataishije". Tukaja kushuhudia wakati wa utawala wa Magufuli, watu wanafukuzwa kwenye mikutano wa hadhara. Sasa hivi tunashuhudia Samia anavyowafukuza kazi kila kukicha maDC na maDED. Yaani mtu yawezekana ana ajira yake, anaondolewa toka kwenye ajira yake, anateuliwa kuwa DC au DED, baada ya miezi michache anafukuzwa. Hivi vyeo vya kuteuliwa vimekuwa vya kumpa utukufu mteuaji hata wakati asipostahili. Wateuliwa wanaishi kama watumwa au mateka wake. Rais alistahilk kupewa idadi ndogo sana ya watu wa kuwateua, wengine wote walistahili kuwa waajiriwa wanaolindwa na kuwajibishwa kwa sheria za ajira.
2) Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kuwa kuna "wanasiasa malaya. Wananunulika kama bidhaa, wanauza utu wao". Wakati wa awamu ya 5 tulishuhudia biashara kubwa ya manunuzi ya wanasiasa iliyosimamiwa na Polepole.
Wanasiasa malaya aliowaona mwalimu miaka mingi iliyopita, tukaja kuwaona dhahiri zaidi wakati wa awamu ya 5, awamu ya Marehemu Magufuli na Samia.
Orodha ya wanasiasa hawa malaya ni ndefu sana, wanasiasa walinunuliwa kama madafu au migebuka, na mpaka leo wametapakaa Serikalini, na hivyo kudhihirisha kuwa nchi kwa kiasi kikubwa inaongozwa na wanasiasa malaya, wanasiasa wanaonunulika, wanasiasa wasio na heshima ya utu. Baadhi nilioweza kuwakumbuka:
Godwin Mollel alikuwa CHADEMA
Julius Kalanga alikuwa CHADEMA
Pauline Gekul alikuwa CHADEMA
Joseph Mkundi alikuwa CHADEMA
Maulid Mtulia alikuwa CUF
Zuberi Kachauka alikuwa CUF
Abdala Mtolea alikuwa CUF
James Millya alikuwa CHADEMA
Kalist Lazaro alikuwa CHADEMA
Cecil Mwambe alikuwa CHADEMA
Vincent Mashinji alikuwa CHADEMA
Chacha Ryoba alikuwa CHADEMA
Waitara alikuwa CHADEMA
Kitila Mkumbo alikuwa ACT
Lulandala alikuwa CHADEMA
Bashiru alikuwa CUF
Patrobas Katambi alikuwa CHADEMA.
Lakini kwa sasa, nchi inanyemelewa na wanasiasa fisi. Hawa hawanunuliwi lakini wananyemelea uongozi kwa mbinu chafu. Sifa kubwa za wanasiasa fisi:
1. Kuwatukuza watawala kwa kutumia unafiki mkubwa, na rushwa ya sifa kwa watawala. Hawawezi kukosoa chochote.
2. Kila kitu wanakigeuza kuwa ni mali ya Rais. Ikijengwa daraja, barabara, wanachuo wakipewa mkopo, n.k. lugha yao utasikia, "Rais amevunja rekodi, amejenga darasa au amechimba kisima, n.k". Wakati ni dhahiri isiyoshaka kuwa Rais hana pesa, tena hata yeye mwenyewe anafadhiliwa na kodi zetu. Hatoi pesa bali tunampa pesa. Lakini wanaongea huo ujinga ili Rais awaone na kuwasikia, na baadaye awape ulaji, siyo awape kazi.
3. Hawa hata Rais ikitokea bahati mbaya akateleza akaanguka, wao watasema, "Rais aonesha maajabu, apiga sarakasi mpaka chini kwa kiwango ambacho hakijwahi kufanywa na Rais yeyote Duniani"
Na bahati mbaya sana uwanasiasa fisi kwa baadhi ya watu umeweza kulipa, ndiyo maana WANASIASA FISI WANAONGEZEKA KWA KASI SANA. Wapo ndani ya Serikali na nje ya serikali. Wanasiasa fisi waliopo ndani ya Serikali wanataka waendelee kubakia kwenye nafasi zao na wengine wanataka wapande zaidi. Hawana uwezo wowote wa maana zaidi ya ufisi, yaani kutoa sifa za kinafiki.
Kafulila alipoondolewa kwenye uRC, ilikuwa kila siku makala ndefu za kumsifia Rais. Ufisi mwishowe ukalipa, angalao akaweza kutulia. Wapo wanafisi waliopo nje ya serikali, kama akina Mwamshamvwa ambao bado hawajaonwa, hawa wapo mitandaoni wakikesha, kusifu, kutukuza na kuwaabudu watawala mpaka wanafamilia wa Rais, wameamua kuwa wanasiasa fisi, ili kungojelea kurushiwa chochote, kuyafanya maisha yao yaliyododa angalao yabadilike na kuwa katika mwanga.
MWISHO
Wanasiasa malaya na wanasiasa fisi, hata siku moja, kamwe hawataweza kuipeleka nchi mahali popote, maana malengo yao siyo kutoa mchango wa maendeleo kwa Taifa, bali kuyapa uhakika wa kushiba matumbo yao.
Tuwaepuke na kuwakimbia wanasiasa malaya na wanasiasa fisi, na watawala wanaopalilia uwepo wa wanasiasa malaya na wanasiasa fisi, kwa namna yoyote inayowezekana.