GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Wanabodi, Naweza kusema ni mwisho wa enzi. Lengai Ole Sabaya angeomba msamaha mapema na kukubali makosa angeishi kwa amani, Alitegemea nguvu za mwanadamu kumshika mkono wakati hana mkataba na aliyemleta huyo mtu Duniani
Ni ukweli na unaumia pale unapoomba msamaha wa kweli kwa maovu na mabaya ni kama unakubali kushindwa na kujidharau mbele ya jamii
Mimi ni mwana ccm na nimetumika sana kwenye Propaganda chafu na safi, Lakini mwaka 2015 mpaka mwaka 2020 ilihitaji kujitoa ufahamu na kuwa mnafiki kwa kueneza chuki na kuligawa Taifa kwani hiki ndio ilikuwa kigezo cha mafanikio ya uongozi na kubaki madarakani
Hii kauli ya kuligawa Taifa na kibri Bwana Lengai Ole Sabaya alitekeleza kwa vitendo kwa kupora, kutukana, kuharibu, kukwapua na kutisha, Wale wote ambao sio wana ccm Waliitwa sio wazalendo kama sera na itikadi ya mwaka 2015 hadi 2020 ilivyohitaji kukufanya ubaki madarakani
Niliomba msamaha kwa uzi huu na nina amani sana
Wafuatao wameongea kauli za dharau kubwa sana mbele za wananchi lakini bado wanashupaza shingo hawaombi msamaha
Ally Happy -Mkuu wa mkoa wa Iringa, Huyu ni tatizo na sio tatizo dogo ni Janga la Taifa, Bado amejaa dharau kama tulivyokuwa sisi wakati tukila mema ya nchi na kumsifia mwanadamu mwenzetu kama vile Yeye ndie ameshikilia maisha yetu. Ameshupaza shingo hataki kuomba msamaha
Kasesera-Huyu alijisahau akatukana wananchi lakini akaomba msamaha wa kijanja janja lakini hafai anahitaji atubu mbele ya jamii
Humprey Pole Pole na Bashiru Ally, Hawa wanapaswa kuomba msamaha mkuu kwa chuki kubwa na dharau, Wakati wa uongozi wao wameligawa Taifa pande mbili waunga juhudi na wasiounga juhudi, Wasiounga juhudi wote walifunguliwa kesi, kubambikiwa makosa na kudhulumiwa biashara zao. Wameharibu uchaguzi Kwa kivuli cha uzalendo na kukatisha tamaa wananchi kwenye chaguzi zingine, Hawa ni moja ya watu wasiofaa kabisa kubaki madarakani lakini bado ni wabunge, Inasikitisha sana
Ni muda muafaka hawa watu wakubali makosa, Walitumika hovyo na kujiona wao wafalme the kati ya mwaka 2015 hadi mwaka 2020.Historia itabaki hivyo kuwa mwaka 2015 mpaka 2020 katiba, Sheria na taratibu hazikufuatwa na watawala bali ilitumika mikono ya chuma kuzima uhuru na haki za Raia

Naomba msamaha kwa Siasa zangu chafu na Propaganda
Wanabodi, Kuomba msamaha sio ujinga bali ni kujitakasa mbele za Muumba. Napenda kutumia nafasi hii kuomba msamaha kwa wote niliowakosea kwa kujibu hovyo au kutukana Katika thread zangu, Reply Back na Comments zangu. Nimeomba radhi baada ya kujifunza jinsi kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu...
www.jamiiforums.com