Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Kuna habari kwamba Mengi atakutana na waandishi wa habari leo Jumatatu saa 7 mchana.

1608027843789.png

MALUMBANO kati ya wafanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi na Rostam Aziz, yaliendelea jana kufuatia wanasheria wa Mengi, Michael Ngalo na Agapitus Nguma kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Rostam juzi huku wakiacha kujibu hoja nyingine na kuongeza maswali kadhaa waliyodai yanahitaji majibu.

Katika mkutano na waandishi wa habari mwanasheria wa Mengi, Michael Ngalo wa Ngalo & Company Advocates alijibu baadhi ya tuhuma hizo kwa niaba ya Mengi na kudai kuwa wako mbioni kumfungulia kesi Rostam Aziz kutokana na tuhuma hizo wanazodai kuwa ni za uongo.

Tuhuma zilizojibiwa na wanasheria hao ni kuhusu fedha za Import Support, kampuni ya Anche Mwedu Limited, utajiri wa Mengi, ukwepaji ulipaji kodi, fedha za misaada na kuwekeza katika biashara, uwekezaji wa kampuni ya NICO kwenye kiwanda cha Interchem Pharma Limited na kuwaita wengine ni wauaji.

Tuhuma ambazo hazikujibiwa na Mengi ambazo zilitolewa na Rostam ni kuhusu kuwa na akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi, malipo kwa wafanyakazi wake, kuhusu kuwa na ugomvi na baadhi ya viongozi na kutaka matatizo hayo yawe ya kitaifa na tuhuma nyinginezo.

Kuhusu fedha za Import Support, Ngalo alisema deni la fedha za import support zimeshalipwa tangu mwaka 2008 hivyo Mengi hana deni kama hilo huku wakionyesha kivuli cha hundi walizolipia deni hilo.

Kuhusu kampuni ya Anche Mwedu Limited alisema suala hilo liliamuliwa mahakamani katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupitia hukumu iliyosomwa Septemba 30 mwaka 2008 na dai la NBC kupitia Consolidated Holding Cooperation kwenye kesi hiyo lilikataliwa na mahakama kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kuthibitisha deni hilo.

Kesi hiyo ya madai nambari 197 ya mwaka 1993 ilifunguliwa na Anche Mwedu Limited dhidi ya Benki Kuu, kampuni za Societe General De Surveilanche S.A, SGS India Private Ltd, Consolidated Holding Corporation, Benki ya NBC na kampuni nyingine ya J.G. Vacuum Flasks Ltd.

Kuhusu ukwepaji kodi wanasheria hao walidai kuwa si Mengi wala kampuni yake yoyote ina tuhuma za kukwepa kulipa kodi.

Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo.

Hata hivyo Mengi kupitia mwanasheria wake aitwaye Nguma alimtaka Rostam kujibu maswali manne, la kwanza, likiwa la kutaka kujua anafanya biashara gani nchini na ataje biashara hizo anazoziendesha na pia kama kampuni zake zimesajiliwa BRELA kwa kutumia jina lake.

Pia alimtaka aeleze kama zinalipa kodi, na kuhusu kuwa hana uhusiano na Kagoda aeleze alikuwa akienda benki kujadiliana juu ya akaunti ya Kagoda alikuwa akifanya hivyo kama nani.

Kuhusu Dowans aeleze mipango ya benki kuipatia Dowans fedha za mkopo aliokuwa na aliushughulikia kama nani, na uhusiano na Richmond anawafahamu vipi wahusika wake.

Hatua hiyo ya Mengi kujibu baadhi ya tuhuma, na kutoa maswali hayo imekuja siku mbili baada ya mfanyabiashara Rostam Aziz kumlipua Mengi na kumbatiza jina la "nyangumi wa ufisadi" baada ya Mengi kumwita yeye na wenzake wanne kuwa ni mafisadi papa.

Rostam Aziz, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara watano waliotuhumiwa na Mengi kuwa mapapa wa ufisadi, alitoa mlolongo wa tuhuma za ufisadi dhidi ya mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, na kueleza kuwa atawasilisha vielelezo kwa vyombo husika ndani ya saa 48 ili Mengi aanze kuchunguzwa.

Mapigo ya Rostam, ambayo yanazidi kupandisha joto la vita hiyo ya maneno, yametokana na tuhuma nzito ambazo Mengi alizitoa Aprili 23 wakati alipotaja wafanyabiashara watano akitaka wadhibitiwe mapema, akiwemo mbunge huyo wa Igunga.

Tofauti na Mengi ambaye hakutoa vielelezo hapo mwanzo wakati anawataja mafisadi papa hao na kusema yuko tayari kupandishwa kizimbani ili ukweli udhihirike, Rostam aliorodhesha tuhuma nyingi na kuahidi kuzikabidhi kwenye vyombo vya serikali ili hatua zichukuliwe.
 
Na bado tutayumbishwa mpaka TUKOME, nahisi MWISHO MBAYA HUKO MBELE tunakoelekea. SIRI wanayo wenyewe sie ngoja tu tuicheze hii ngoma kwa viitikio na vigele gele vingiiiiiii.........
You are right... Ninachojua kuna watu watafanyiwa umafia (am not praying for this!) na kama si hivi, basi tutarajie anguko la ajabu katika serikali ya awamu hii kabla ya uchaguzi. Something needs to be done ASAP!
 
Wana JF

Mi naomba kuuliza TUNAENDA WAPI? Tz yetu haina vyombo vya Usalama? Huyi Kiranja wetu Mkuu Hizi habari ahazioni au kusikia..........usikute ananyimwa kuuangalia TV kwenye White House yake a.k.a IKULU............Mbona amekaa kimya tuu?
 
You are right... Ninachojua kuna watu watafanyiwa umafia (am not praying for this!) na kama si hivi, basi tutarajie anguko la ajabu katika serikali ya awamu hii kabla ya uchaguzi. Something needs to be done ASAP!
Anguko ndo suluhu nzurii...............
 
You are right... Ninachojua kuna watu watafanyiwa umafia (am not praying for this!) na kama si hivi, basi tutarajie anguko la ajabu katika serikali ya awamu hii kabla ya uchaguzi. Something needs to be done ASAP!


Yule Mnajimu Mkuu/maarufu keshatabiri hilo.... tusubiri tuone ni nini hasa kitatokea.
 
Kama ni kweli, kuna mlipuko utatokea ktk nchi hii. Labda UWT waambiwe wamzuie. mzee Mengi anahisi serikali inwakingia kifua mafisadi na inawasaidia kuwakandamiza wanaopinga ufisadi. Mh!, tusubiri....
 
Really something need to be DONE, and these people know each other VERY WELL. nahisi pia ni CHAIN ndefu inawezekana kuna makundi yanawakilishwa hapo. it might be beyond vita ya UFISADI as we might be thinking..... kama ulivyosema INVISIBLE, tutegemee ANGUKO KUBWA iff jamaa atakutana na waandishi kwa mujibu wa hii THREAD.... mwili unanisisimuka miye. any way IT IS OUR TIME to sit down and ENJOY tha SHOW, wacha tupate mengi yaliyojificha regardless madhara ya hayo MABOMU.
 
Naomba kuiwakilisha JF ili niweze kuwapa LIVE .Niko njiani naenda town sasa nipeni mikoba .Nitasimama pale Haider Plaza kujua ukweli wa hizi nyeti.
 
Wacha waumbuane tu mpaka kieleweke. Ila Mengi mbona ameharakisha sana? Atulie na kuweka facts zake vizuri kabla ya kuzimwaga kwa wananchi. Ukiwa na hasira kali huwezi kuweka mambo vizuri.

Mafisadi bwana, wanajifanya eti wanatutetea sisi wananchi, kumbe wanataka kutufanya kondoo, tuwaamini na kutulia kabla ya kutushambulia.

JK kashindwa kuendesha nchi na matokeo yake ndio haya. Lakini pia conflicts kama hizi if managed zinaweza kuwa chachu ya maendeleo, bora zisiende out of control, hapo nchi inageuka kuwa Somalia.
 
Wana JF

Mi naomba kuuliza TUNAENDA WAPI? Tz yetu haina vyombo vya Usalama? Huyi Kiranja wetu Mkuu Hizi habari ahazioni au kusikia..........usikute ananyimwa kuuangalia TV kwenye White House yake a.k.a IKULU............Mbona amekaa kimya tuu?

Mkiwapiga mawe mafisadi kila mtakapo waona atajua tu hata kama haangali TV. si watenda vikaoni na nundu ...
 
Wacha waumbuane tu mpaka kieleweke. Ila Mengi mbona ameharakisha sana? Atulie na kuweka facts zake vizuri kabla ya kuzimwaga kwa wananchi. Ukiwa na hasira kali huwezi kuweka mambo vizuri.

Mafisadi bwana, wanajifanya eti wanatutetea sisi wananchi, kumbe wanataka kutufanya kondoo, tuwaamini na kutulia kabla ya kutushambulia.

JK kashindwa kuendesha nchi na matokeo yake ndio haya. Lakini pia conflicts kama hizi if managed zinaweza kuwa chachu ya maendeleo, bora zisiende out of control, hapo nchi inageuka kuwa Somalia.
Mtanzania,

Unajua inafikia wakti nahisi kutokwa machozi kwa namna mambo yanavyoenda ndivyo sivyo!

Unajua iko hivi: Mengi anashauriwa na wana JF wenzetu na hata Rostam alichokiongea jana kaandikiwa na mwana JF mwenzetu. Tunaelekea wapi?

Pls mnaowashauri hivi, jaribu kuwaonea huruma, mnawachanganya kabisa, wanavyofanya sivyo (labda kama mmedhamiria kuwamaliza kabisa!)
 
Nafahamishwa na mwandishi wetu kuwa wameambiwa atafanya Press Conference SI ofisini kwake bali Royal Palm (Movenpic) Hotel.
 
Unajua sasa hv watanzania wameelekeza masikio yao kwenye scandal ya hawa watu wawili,(Mengi na Rostam). Itakwa ni kujibizana tuuuuuuuuu na wandishi wa habari halafu mwisho wa yote hakuna kitakchooendela. Wote hawa ni wezi na kila mmoja wao anastaili zake za wizi. WOTE NI WEZI WAKUBWA.

Wanatupumbaza sisi raia kwa kukaa nakusikiliza uchafu wao.

Mlio nyumbani Tanzania kataeni ushenzi huu. Tatizo nchi yangu Tanzania kuna wanafiki wengi na wengi wanasikilza na kuyapa kipau mbele mambo yasiyo ya msingi. Niko Oslo Norway nahangaika na shule pengine nikirudi nyumbani nitaisaidia nchi yangu.

Ukizaliwa na ukakuta wazazi wako ni watumwa hutajua kama wazazi wako utumwani, mpaka sauti toka nje ikwambie kuwa familia yenu iko utumwani.

Nawahi darasani, ila narudia kusema WOTE HAWA NI WEZI
 
Mtanzania,

Unajua inafikia wakti nahisi kutokwa machozi kwa namna mambo yanavyoenda ndivyo sivyo!

Unajua iko hivi: Mengi anashauriwa na wana JF wenzetu na hata Rostam alichokiongea jana kaandikiwa na mwana JF mwenzetu. Tunaelekea wapi?

Pls mnaowashauri hivi, jaribu kuwaonea huruma, mnawachanganya kabisa, wanavyofanya sivyo (labda kama mmedhamiria kuwamaliza kabisa!)

RA has lost Authority no doubt!!! ukiwa na hela bila authority matokeo ndio hayo Muulize Idd Simba he knows well nini maana ya kuwa na hela ukakosa authority ...

RA's days are numbered!

wataka maelezo zaidi?
 
ra has lost authority no doubt!!! Ukiwa na hela bila authority matokeo ndio hayo muulize idd simba he knows well nini maana ya kuwa na hela ukakosa authority ...

Ra's days are numbered!

Wataka maelezo zaidi?

tunayataka maelezo hayo
 
hapa kuna AGENDA ya SIRI, it might be business conflicts. kwa sababu mengi anajaribu kupandikiza chuki kwa watanzania ili wafikie mahali kuchukua hatua mikononi juu ya hawa wanaoitwa MAFISADI. Hii ni kutokana na kauli yake kwamba hawa jamaa wana pesa nyingi za kuweza kupindisha ukweli, kwa hiyo kwa lolote lile bada atadai ukweli umepindishwa na pesa. Sasa hii sinema ngoja tuone mwisho wake, lakini naamini sterling na adui watasalimika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom