Wanasheria nisaidieni, Baba Mzazi anazidi kuuza mali

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,929
Habarini za asubuhi, naomba niende moja kwa moja kwenye mada baada ya baba angu kuuza nyumba yake ya kwanza week 3 zilizopita na kubakisha nyumba moja maeneo ya huku Sinza Mori ambayo ndio tunakaa sasa hivi nayo anataka kuuza, wakati bado watoto wake sisi bado tupo hai tena ususani mtoto wake mimi bado kijana mdogo hata umri wa miaka 50 sijafika ndio kwanza nina 42, na cha kushangaza huyu mzee baada ya kuuza nyumba ya kwanza bado hajanipa mgao wowote wa pesa mpaka niliamua kwenda kumshtaki ofisi ya kata na jana nimeenda kufungua kesi polisi na Jumatatu ya tarehe 24 tunaenda mahakamani kwa kesi kusikilizwa.

Cha kushangaza leo ameamka na kuanza kusema anauza nyumba hii pia, jamani wanasheria naombeni mnisaidie maana huyu baba anateketeza mali zote na mimi kama mtoto wake sijaambulia chochote mpaka muda huu, nahisi uenda mzee wangu akawa amechanganyikiwa, nataka nieleze mahakama hiyo jumatatu hoja yangu hii kama huyu mzee wangu huenda amechanganyikiwa ili niweze kupatiwa pesa zake zote nizihifadhi sehemu nzuri na salama.

Haiwezekani mimi mtoto wake nipo na nina elimu nzuri tu na kubwa sana ya degree ya marketing kutoka chuo kikubwa kabisa cha university of dar es salaam, na nina umri wa kijana ninayejitambua kabisa wa miaka 42 ashindwe kunipatia hizo pesa nizihifadhi au kama hataki anipe mgao wangu kabisa nikatafute maisha yangu.

Leo ananiambia kwa jeuri eti kama nimeamua kwenda mahakamani basi nitakuwa nakula na kulala mahakamani ila sio hapa kwake, nikamuambia hapa sio kwako hapa ni kwetu maana wewe ni baba yangu na mahakama inatambua umuhimu wa mtoto kwenye ishu ya urithi wa mali, anasema anaenda kutafuta dalali na muda huu ameondoka

Wanasheria naombeni mshikamane na mimi kwenye ili wakuu ili nipate haki yangu ya mali. Na alivyo na jeuri ananiambia ananipa siku mbili niwe nimeshatoa begi langu la nguo ndani niwe nimeondoka jamani mpaka namshangaa huyu mzee.

Nawasilisha
 
Ukute mzee kawa sponser sasa huyo binti kamfanyia uganga hizo hela zinaweza potea fanya ukaangalie kiasili mahakamani pekee utapoteza muda.Sema miaka 42 kulilia mali za baba sio sahihi ila fatilia kwann imekuwa ghafla sana
za chini chini naskia ameongeza na ela zake nyingine ameenda kununua nyumba Mbweni yenye losheni moja ndio nafatilia, maana haiwezekani anakuwa anafanya mambo bila kunishirikisha nahisi uyu mzee atakuwa ana shida sehemu.
 
Nyie ndio mnafanya wazazi wengine wasisomeshe watoto wao. Umesomeshwa hadi kiwango cha degree na una umri wa miaka 42 bado unapelekana mahakamani na mzazi wako kwa mali zake?

Sio kwamba nahukumu, kwa haya maelezo kidogo unayoyatoa inaonekana kabisa wewe ni mtata na ndio maana mzee anaona bora apangilie mambo yake mwenyewe.

Hadi hapo ulitakiwa uwe umeshajitegemea, hata kama umepanga chumba kimoja ila una kwako, mzee angekuona unajitambua.

Hapo mkuu hawezi kukuamini kwa chochote anaona kama atapoteza mali zake tu akikukabidhi.

Cha kwanza, nenda kafute hiyo kesi mahakamani na muombe radhi mzazi mkayamalize nyumbani. Hata asipokugawia chochote, piga moyo konde utafute chumba akili itakukaa sawa.
 
za chini chini naskia ameongeza na ela zake nyingine ameenda kununua nyumba Mbweni yenye losheni moja ndio nafatilia, maana haiwezekani anakuwa anafanya mambo bila kunishirikisha nahisi uyu mzee atakuwa ana shida sehemu.

Mzee anaweza kuwa anashida lakini usikatae na wewe pia una shida, tena kubwa tu.

Sasa kama amenunua nyumba nyingine tatizo liko wapi?

Wewe kinakuumiza nyumba kuuzwa au kutokupewa pesa?
 
Wewe huna degree kwa uandishi huo na mantiki hii ya ajabu.

Ulijiuliza yeye Baba yako hizo unazosema Mali alipewa na Baba yake au wazazi wake? Una miaka 42 hata ingekuwa na umri wa miaka 24 huna haki ya kudai kitu zaidi ulipaswa kuishi kwako na kutafuta vyakwako hizo mahakama unapoteza muda tu.
 
Back
Top Bottom