Wanasheria na watafsiri sheria msaada wenu

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,659
6,910
Nawiwa kuombwa msaada wa kutafsiriwa kifungu hiki Cha 84 (2) Cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhusu namna ya kumpata spika wa bunge.

Ni sahihi kusema kuwa nafasi ya naibu spika haijatajwa kwenye ibara hiyo Kama alivyosema Tulia?

Ni sahihi Kwa naibu spika kugombea nafasi ya spika bila kujiuzulu nafasi anayoishikilia?

Ukada marufuku kwani nitakuwasha nipate ban ya maisha!
 
Nawiwa kuombwa msaada wa kutafsiriwa kifungu hiki Cha 84 (2) Cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhusu namna ya kumpata spika wa bunge...
Sina hakika lakini kwa kuwa amechukua form ndan ya chama kuomba kuteuliwa,

pengine atajiuzuru akiteuliwa na chama.
 
Kikatiba Tulia yupo sahihi, haupaswi kujiuzulu kazi unayofanya ili uchukue form ya kugombea uspika Ila utakapoteuliwa na chama na ukifanikiwa kupita kwenye kura basi ndipo utajiuzulu kazi unayofanya ili uanze kazi mpya ya uspika Ila ukikosa unarudi kwenye kazi yako.

Hii tumeona kwenye kuchukua form na kugombea ubunge, mtu anachujua likizo anaingia huko kwenye mchakato Ila akikosa anarudi kazini Ila akipata ndio anaacha kazi anaingia kwenye kazi mpya which is okay kabisa.

Hata hivyo kwa nafasi aliyopo na kwa sababu Katiba imekaa kimya kuhusu Naibu spika kuweza kugombea uspika endapo itatokea mazingira Kama haya basi ingekuwa ni busara kwake kujiuzulu kwanza ili ufanyike uchaguzi wa nafasi zote kwa wakati mmoja ili kuepuka kuchelewesha shughuli za Bunge pamoja na gharama zisizo na msingi wowote.

Hautarajii Naibu Spika aendelee kuwepo mpaka atakapochaguliwa kugombea na uchaguzi unaofanyika ni wa spika then akipata ndio sasa ajiuzulu unaibu spika na Tena uitishwe uchaguzi mpya Tena wa Naibu Spika.

Kwakweli hii pamoja haijawekwa wazi kwenye Katiba Tena imetusaidia kuona hili eneo lakini busara ya kiongozi ichukue mkondo.
 
Nawiwa kuombwa msaada wa kutafsiriwa kifungu hiki Cha 84 (2) Cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhusu namna ya kumpata spika wa bunge...
Mkuu Mnasihi, japo Naibu Spika , Dr. Tulia Akson ni mwanasheria, ila uwezo wake kutafsiri katiba ni limited.
Naibu Spika ni kiongozi wa utumishi wa umma kama Waziri na Naibu Waziri, alipaswa kujiuzulu kwanza unaibu Spika ndipo agombee uspika.

Hili nimelifafanua hapa

P
 
Kikatiba Tulia yupo sahihi, haupaswi kujiuzulu kazi unayofanya ili uchukue form ya kugombea uspika Ila utakapoteuliwa na chama na ukifanikiwa kupita kwenye kura basi ndipo utajiuzulu kazi unayofanya ili uanze kazi mpya ya uspika Ila ukikosa unarudi kwenye kazi yako...
Ndivyo Katiba inavyosema au hii umeitoa kichwani?
 
Back
Top Bottom