Wanasayansi Wafichua Dalili za Mwisho wa Dunia!

Ko watu waendeleee kula Bata sio. Mpaka hiyo miaka billion 4 ifike ni Leo kweli?????

Asa hapo mpaka aje afufue na watu walokufaga na kuwapa hukumu siutakuta walishaga sahau kama waliwahi kuishi duniani, Kila hukumu watakayopewa watabaki wanashangaa tuu.
Mleta mada hajaleta time frame

Ila ndio hivyo probability ya hilo tukio ni in next 4 Billion years.
 
Duuuh hiyo utakuta tuu Yesu badogi hajarudiuii????? au ndo ikifikia hapo ndo atakuwa kwenye mchakato wa kurudi
 
Hiyo assumption itatokea baada ya miaka
BILIONI 4 IJAYO.
USITUCHOSHE.
siku na saa anajua Mungu pekee.
Kwanza nakushukuru kwa kupita hapa. Wewe ni mtu muhimu sana.
Sasa, kama umeisoma mada yote, utagundua kwamba mimi sijasimamia hizo unazoziita assumption. Nimeziweka hapa kama intro tu.

Mimi imani yangu kwamba hizi ni nyakati za mwisho, nimeijenga kwenye Biblia. Nadharia za wanasayansi huwa zinabadilika, lakini Neno la Mungu halibadiliki.

Sijataja siku wala saa. Nimetaja dalili tu. Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu. Ukiona mawingu meusi usipuuze na kusema mvua haitanyesha. Vivyo hivyo tuonapo dalili alizozitaja Yesu za kuja kwake na za mwisho wa dunia zinatimia, hatupaswi kupuuza. Badala yake tunapaswa kujiandaa kwa tukio hilo muhimu.

Isitoshe, mimi nina Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni Mungu. Anajua yaliyopo na yajayo. Roho Mtakatifu ndiye anayenihimiza nikuambie kuwa mwisho wa dunia umekaribia. Ukiendelea kupuuza itakuwa kwako kama wale waliopuuza wakati wa Nuhu. Gharika ilikuja ghafla ikawakuta unprepared. Wakaangamizwa kwa maji. Tubuni, ufalme wa Mungu umekaribia (Marko 1:15).
 
Hizo dalili ni scientific theories,

Hivyo lazima ziwe supported by evidence, unless otherwise ni porojo tu.

Kisayansi hilo tukio limekuwa calculated in the next 4 billion years to come, so kama msingi wa hoja yako unategemea hapo?

Chill bro.
 
Shetani anatupofusha macho ya rohoni ili tuyaamini tunayoyaona kwa macho ya mwilini tu.Na kwa sababu hii,binadamu wengi hatuna imani kwamba asili yetu inatokana na Mungu baba mwenyewe.Lakini ukweli ni kwamba mwisho wa dunia umesababishwa na binadamu kumwasi Mungu.Binadamu tunapasa kuisikiliza sauti ya Mungu ili tujijengee imani na kumtumikia.
Open your mind
 
Nilitaka useme wazi ulichokisema sasa.
Soma Maandiko yafuatayo aliyoyasema Yesu mwenyewe alipokuwa huko huko Israeli, kisha uniambie kama wanachokifanya Israeli ni sawa au la:
Mathayo 5:38-39
“Mmesikia kwamba ilinenwa: ‘Jicho kwa jicho, jino kwa jino.’ Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.
1 Yohana 3:15
"Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake."
nahisi wewe ni mkristo unaejielewa👏👏 ningekushangaa kama ungesurport kile ambacho Israel anakifanya!
 
Unachosema kina nusu tu ya ukweli. Ni sawa kabisa, kila mtu ana mwisho wake binafsi (kifo), lakini kudai hakuna mwisho wa dunia kabisa ni hitimisho lisilo na ushahidi.

Katika Biblia Takatifu, Mungu ameelezea wazi mambo mawili tofauti: mwisho wa mtu binafsi na mwisho wa ulimwengu. 2 Petro 3:10 inasema: "Siku ya Bwana itakuja kama mwizi; mbingu zitapita kwa mshindo mkubwa, na vitu vyote vitateketezwa."

Hapo hazungumzii mtu mmoja kufa, anaongelea ulimwengu mzima kubadilishwa/kuondolewa.

Pia, Ufunuo wa Yohana 20:11 inasema: "Kisha, nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe, na yule aketiye juu yake. Dunia na mbingu vikatoweka mbele ya macho yake, na havikuonekana tena."

Hii ni lugha ya wazi kabisa ya mwisho wa mfumo mzima wa dunia, sio maisha ya mtu mmoja mmoja tu.

Hata kama wewe ni Atheist na unaikataa Biblia, ziamini basi hizo nadharia za wanasayansi kuhusu uwezekano walioutaja wa mwisho wa ulimwengu. Na kama hutaki kukubaliana na wanasayansi, kubaliana basi hata na Wazee wetu waliotangulia waliosema: "Kila chenye mwanzo kina mwisho" Dunia ilikuwa na mwanzo hivyo lazima itakuwa na mwisho. Ukiendelea kupinga, nakusikitikia kwa sababu utajuta sekunde ya kwanza tu baada ya kuondoka duniani. Na hutakuwa na nafasi tena ya kutubu na kuamini. Soma Luka 16:27–31 ujue yanayotokea mtu akifa.
Sasa Mungu alikuumba ili aje akuuwe?
 
Kama huna habari, wanasayansi wamekuwa wakichunguza mwenendo wa ulimwengu (universe), na matokeo ya tafiti zao yamefichua jambo la kushangaza: ulimwengu hauko tuli, bali unapanuka kwa kasi kubwa sana.

Kupitia uchunguzi wa kina wa anga (astronomy), wamegundua kuwa kuna nguvu ya ajabu inayoitwa dark energy, ambayo ndiyo inachochea upanuzi huu wa ulimwengu. Nguvu hii inaonekana kuwa kubwa kuliko nguvu ya uvutano (gravity), na inaendelea kusukuma galaksi mbali mbali ziachane kwa kasi inayoongezeka kila siku.

Wanasayansi wametoa nadharia kadhaa kuhusu mwisho wa ulimwengu, mojawapo ni ile inayojulikana kama Big Rip. Nadharia hii inaeleza kuwa, kama hii nguvu ya upanuzi itaendelea kuongezeka, itafika mahali ambapo itashinda nguvu zote zinazoshikilia vitu pamoja, kuanzia galaksi, nyota, sayari, hadi atoms zenyewe. Hatimaye, kila kitu kitavunjika na kusambaratika kabisa.

Ajabu ni kwamba, nadharia hizo zinashabihiana sana na yale yaliyoandikwa katika Biblia Takatifu miaka mingi iliyopita. Maandiko yanatueleza kwamba siku ya mwisho inakuja. Siku hiyo mbingu zitateketezwa kwa moto na kutoweka, na viumbe vya asili vitayeyushwa.

Hivyo ni dhahiri mwisho wa ulimwengu unakuja, na utakuwa wa kutisha na wa ghafla.

Yesu Kristo alipokuwa duniani, kabla hajapaa mbinguni, alieleza dalili zitakazotangulia kurudi kwake na za mwisho wa dunia. Dalili hizo ni pamoja na kuongezeka kwa vita na machafuko, matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali, magonjwa hatari na yasiyo ya kawaida, kuongezeka kwa uovu na maasi, upendo wa watu wengi kupoa, watu kupenda fedha kuliko Mungu, kuibuka kwa manabii wa uongo nk.

Tukiangalia dunia ya leo, dalili hizo zinaonekana wazi mbele ya macho yetu. Hata mambo ya kusikitisha yanayoendelea huko Mashariki ya Kati, yalitabiriwa zamani kwamba yatatokea.

Inawezekana kabisa kwamba Mungu, kwa huruma zake, ameruhusu sayansi ithibitishe kwa njia hiyo kwamba mwisho upo ili hata wale wasiopenda kusikia Neno lake waujue ukweli huo.

Ndugu zangu, huu sio wakati wa kubeza wala kupuuza. Ufalme wa mbinguni umekaribia. Huu ni wakati wa kutubu dhambi, kumrudia Mungu kwa moyo wa dhati, kumwamini Yesu Kristo na kumpokea kwa imani mioyoni mwetu awe Bwana na Mwokozi wetu.

Tukifanya hivyo, siku ya mwisho itakapofika, hatutakuwa miongoni mwao watakaolia na kusaga meno, bali tutanyakuliwa hadi mbinguni na kupokea uzima wa milele.

Sources:
  • BBC – Theories about the end of the universe (Big Rip, Big Freeze, Big Crunch)
  • NASA – Research on expanding universe and dark energy
  • Biblia Takatifu – 2 Petro 3:12; Mathayo 24
View attachment 3561406
Wanafichuaje kitu ambacho kishaongelewa/ Kipo ndani ya Quran miaka 1400 iliyopita??

Chapter Adh-Dhaariyat, Verse 47

وَٱلسَّمَآءَ بَنَيْنَـٰهَا بِأَيْي۟دٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ

We built the universe with ˹great˺ might, and We are certainly expanding ˹it˺
"51:47Qur'an"

Cc adriz
 
Naomba kujua mbinguni ni wap?
Mbinguni ni makao ya Mungu, yaani ni mahali ambapo Mungu anakaa katika utukufu wake. Yesu ndiye njia ya kutufikisha katika makao hayo, na atakuja tena kutuchukua sote tunaomwamini na kutupeleka katika makao hayo, ili tuishi pamoja na Mungu. Kulingana na dalili tunazoziona, siku hiyo imekaribia sana. Hivyo usikawie, tubu dhambi zako, mwamini Yesu, umpokee kwa imani moyoni mwako, awe Bwana na Mwokozi wako. Ukifanya hivyo siku hiyo ikifika, utapaona mbinguni physically.
 
Wanafichuaje kitu ambacho kishaongelewa/ Kipo ndani ya Quran miaka 1400 iliyopita??

Chapter Adh-Dhaariyat, Verse 47

وَٱلسَّمَآءَ بَنَيْنَـٰهَا بِأَيْي۟دٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ

We built the universe with ˹great˺ might, and We are certainly expanding ˹it˺
"51:47Qur'an"

Cc adriz
Wanafichua kwa wasiojua. Sio kila mtu anajua kwamba mwisho wa dunia umekaribia
 
Sasa Mungu alikuumba ili aje akuuwe?
Mungu hakutuumba ili aje atuue. Mtu anaangamia si kwa sababu Mungu alimuumba ili afe, bali kwa sababu ya kumkataa Mungu na kuishi katika dhambi. Ukitubu dhambi na kumwamini Yesu utaishi milele mbinguni. Lakini ukimkataa Yesu na kuendelea kutenda dhambi utatupwa katika moto wa milele.
 
Mbinguni ni makao ya Mungu, yaani ni mahali ambapo Mungu anakaa katika utukufu wake. Yesu ndiye njia ya kutufikisha katika makao hayo, na atakuja tena kutuchukua sote tunaomwamini na kutupeleka katika makao hayo, ili tuishi pamoja na Mungu. Kulingana na dalili tunazoziona, siku hiyo imekaribia sana. Hivyo usikawie, tubu dhambi zako, mwamini Yesu, umpokee kwa imani moyoni mwako, awe Bwana na Mwokozi wako. Ukifanya hivyo siku hiyo ikifika, utapaona mbinguni physically.
Ndo nataka kujua hayo makao yake yapo wap?
 
Mungu hakutuumba ili aje atuue. Mtu anaangamia si kwa sababu Mungu alimuumba ili afe, bali kwa sababu ya kumkataa Mungu na kuishi katika dhambi. Ukitubu dhambi na kumwamini Yesu utaishi milele mbinguni. Lakini ukimkataa Yesu na kuendelea kutenda dhambi utatupwa katika moto wa milele.
Acha kuamini mambo ya wakoloni
 
Wana sayansi na mambo ya mwisho wa dunia hakuna uhusiano wowote bwasheee.
Kama huna habari, wanasayansi wamekuwa wakichunguza mwenendo wa ulimwengu (universe), na matokeo ya tafiti zao yamefichua jambo la kushangaza: ulimwengu hauko tuli, bali unapanuka kwa kasi kubwa sana.

Kupitia uchunguzi wa kina wa anga (astronomy), wamegundua kuwa kuna nguvu ya ajabu inayoitwa dark energy, ambayo ndiyo inachochea upanuzi huu wa ulimwengu. Nguvu hii inaonekana kuwa kubwa kuliko nguvu ya uvutano (gravity), na inaendelea kusukuma galaksi mbali mbali ziachane kwa kasi inayoongezeka kila siku.

Wanasayansi wametoa nadharia kadhaa kuhusu mwisho wa ulimwengu, mojawapo ni ile inayojulikana kama Big Rip. Nadharia hii inaeleza kuwa, kama hii nguvu ya upanuzi itaendelea kuongezeka, itafika mahali ambapo itashinda nguvu zote zinazoshikilia vitu pamoja, kuanzia galaksi, nyota, sayari, hadi atoms zenyewe. Hatimaye, kila kitu kitavunjika na kusambaratika kabisa.

Ajabu ni kwamba, nadharia hizo zinashabihiana sana na yale yaliyoandikwa katika Biblia Takatifu miaka mingi iliyopita. Maandiko yanatueleza kwamba siku ya mwisho inakuja. Siku hiyo mbingu zitateketezwa kwa moto na kutoweka, na viumbe vya asili vitayeyushwa.

Hivyo ni dhahiri mwisho wa ulimwengu unakuja, na utakuwa wa kutisha na wa ghafla.

Yesu Kristo alipokuwa duniani, kabla hajapaa mbinguni, alieleza dalili zitakazotangulia kurudi kwake na za mwisho wa dunia. Dalili hizo ni pamoja na kuongezeka kwa vita na machafuko, matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali, magonjwa hatari na yasiyo ya kawaida, kuongezeka kwa uovu na maasi, upendo wa watu wengi kupoa, watu kupenda fedha kuliko Mungu, kuibuka kwa manabii wa uongo nk.

Tukiangalia dunia ya leo, dalili hizo zinaonekana wazi mbele ya macho yetu. Hata mambo ya kusikitisha yanayoendelea huko Mashariki ya Kati, yalitabiriwa zamani kwamba yatatokea.

Inawezekana kabisa kwamba Mungu, kwa huruma zake, ameruhusu sayansi ithibitishe kwa njia hiyo kwamba mwisho upo ili hata wale wasiopenda kusikia Neno lake waujue ukweli huo.

Ndugu zangu, huu sio wakati wa kubeza wala kupuuza. Ufalme wa mbinguni umekaribia. Huu ni wakati wa kutubu dhambi, kumrudia Mungu kwa moyo wa dhati, kumwamini Yesu Kristo na kumpokea kwa imani mioyoni mwetu awe Bwana na Mwokozi wetu.

Tukifanya hivyo, siku ya mwisho itakapofika, hatutakuwa miongoni mwao watakaolia na kusaga meno, bali tutanyakuliwa hadi mbinguni na kupokea uzima wa milele.

Sources:
  • BBC – Theories about the end of the universe (Big Rip, Big Freeze, Big Crunch)
  • NASA – Research on expanding universe and dark energy
  • Biblia Takatifu – 2 Petro 3:12; Mathayo 24
View attachment 3561406
 
Acha kuamini mambo ya wakoloni
Kataa kudanganywa na shetani.
Biblia sio ya wakoloni, ni ujumbe wa Mungu uliokuwepo kabla yao.
Yesu Kristo alizitaja dalili za mwisho wa dunia zamani sana kabla ya hao wakoloni kuja kukutawala.
Ukichagua kupuuza, ukweli hautabadilika kwa sababu umeukataa.
Ila nakusikitikia utajuta siku ya mwisho itakapofika na hautapata nafasi ya kutubu wala kumwamini Yesu. Neema itakuwa imefungwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom