Wanasayansi Wafichua Dalili za Mwisho wa Dunia!

Wanasayansi Wafichua Dalili za Mwisho wa Dunia!

Kama NASA wameanza kunusa dalili za mwisho wa Dunia, na wao wanaspend bilions kwenye utafiti wa mambo ya anga, kuna possibility mwisho upo. Lisemwalo lipo, kama halipo, laja.
Mwambie kwa HERUFI KUBWA labda atakuelewa
 
Nadharia kama Big Rip zipo, but ni predictions za mbali sana inaweza kuchukua mabilioni ya miaka.

Anyways mimi pia ni muamini kama wewe, naamini mwisho utafika, but the end is not anytime soon.
 
Nmesoma lakini nlipoona umechanganya na biblia basi nikaishia hapo
Nisamehe ndugu yangu, kumbe nimekuchanganyia pilipili kwenye mboga na wewe hupendi?

Sogeza sikio lako nikuambie jambo muhimu: nakuomba jambo hili: usiihukumu Biblia kabla hujaichunguza wewe mwenyewe.

Biblia Takatifu sio kitabu cha kawaida. Kimekuwa kikisomwa kwa maelfu ya miaka, na kimewabadilisha watu wa aina zote, hata wanasayansi wakubwa kabisa katika historia.

Kwa mfano: Isaac Newton alitumia muda mwingi kusoma Biblia kuliko hata sayansi yenyewe.

Galileo Galilei alisema Biblia inaonyesha njia ya kwenda mbinguni, sio jinsi mbingu zinavyokwenda, akithibitisha kuwa haipingani na sayansi bali ina lengo tofauti.

Johannes Kepler aliona kazi yake ya sayansi kama njia ya “kufikiri mawazo ya Mungu baada yake.”

Hao hawakuwa watu wajinga. Walikuwa watu wenye IQ kubwa sana, lakini bado waliona thamani ya kusoma Biblia.

Jaribu hata kusoma sehemu ndogo tu, mfano Injili ya Luka sura ya 1, bila presha yoyote. Soma huku ukijiuliza: “Hiki kitabu kinasema nini hasa?”

Unaweza kushangaa utakachogundua.
 
Nadharia kama Big Rip zipo, but ni predictions za mbali sana inaweza kuchukua mabilioni ya miaka.
Anyways mimi pia ni muamini kama wewe, naamini mwisho utafika, but the end is not anytime soon.
Nimekupata vizuri sana. Ni kweli kabisa, kisayansi hizo nadharia kama Big Rip ni predictions za mabilioni ya miaka. Lakini point ya kiroho haiko kwenye timeline, iko kwenye uhakika wa tukio lenyewe na kutokujulikana kwa muda wake.

Katika Biblia Takatifu, Yesu Kristo alisema wazi kwamba: Siku hiyo inakuja kama mwizi ajavyo (Mathayo 24:36,44), yaani haitatangazwa mapema wala kufuata ratiba tunazozijua.

So, hata kama kisayansi inaonekana “far away,” kiroho inaweza kuwa karibu mno kuliko tunavyodhani, kwa sababu: kwanza hatujui exact time; pili, dalili alizosema Yesu za kuja kwake na za mwisho wa dunia, tayari zimeonekana.

So kusema “not anytime soon” ni very risky kiroho.

Better stance ni hii:
Yes, inaweza kuwa mbali kisayansi, but spiritually we stay ready anytime. Kwa sababu Yesu mwenyewe anasema: Behold, I am coming soon, bringing my recompense with me, to repay each one for what he has done (Rev 22:12).

Au wewe neno "soon" unalielewaje?
 
Amen
Kama huna habari, wanasayansi wamekuwa wakichunguza mwenendo wa ulimwengu (universe), na matokeo ya tafiti zao yamefichua jambo la kushangaza: ulimwengu hauko tuli, bali unapanuka kwa kasi kubwa sana.

Kupitia uchunguzi wa kina wa anga (astronomy), wamegundua kuwa kuna nguvu ya ajabu inayoitwa dark energy, ambayo ndiyo inachochea upanuzi huu wa ulimwengu. Nguvu hii inaonekana kuwa kubwa kuliko nguvu ya uvutano (gravity), na inaendelea kusukuma galaksi mbali mbali ziachane kwa kasi inayoongezeka kila siku.

Wanasayansi wametoa nadharia kadhaa kuhusu mwisho wa ulimwengu, mojawapo ni ile inayojulikana kama Big Rip. Nadharia hii inaeleza kuwa, kama hii nguvu ya upanuzi itaendelea kuongezeka, itafika mahali ambapo itashinda nguvu zote zinazoshikilia vitu pamoja, kuanzia galaksi, nyota, sayari, hadi atoms zenyewe. Hatimaye, kila kitu kitavunjika na kusambaratika kabisa.

Ajabu ni kwamba, nadharia hizo zinashabihiana sana na yale yaliyoandikwa katika Biblia Takatifu miaka mingi iliyopita. Maandiko yanatueleza kwamba siku ya mwisho inakuja. Siku hiyo mbingu zitateketezwa kwa moto na kutoweka, na viumbe vya asili vitayeyushwa.

Hivyo ni dhahiri mwisho wa ulimwengu unakuja, na utakuwa wa kutisha na wa ghafla.

Yesu Kristo alipokuwa duniani, kabla hajapaa mbinguni, alieleza dalili zitakazotangulia kurudi kwake na za mwisho wa dunia. Dalili hizo ni pamoja na kuongezeka kwa vita na machafuko, matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali, magonjwa hatari na yasiyo ya kawaida, kuongezeka kwa uovu na maasi, upendo wa watu wengi kupoa, watu kupenda fedha kuliko Mungu, kuibuka kwa manabii wa uongo nk.

Tukiangalia dunia ya leo, dalili hizo zinaonekana wazi mbele ya macho yetu. Hata mambo ya kusikitisha yanayoendelea huko Mashariki ya Kati, yalitabiriwa zamani kwamba yatatokea.

Inawezekana kabisa kwamba Mungu, kwa huruma zake, ameruhusu sayansi ithibitishe kwa njia hiyo kwamba mwisho upo ili hata wale wasiopenda kusikia Neno lake waujue ukweli huo.

Ndugu zangu, huu sio wakati wa kubeza wala kupuuza. Ufalme wa mbinguni umekaribia. Huu ni wakati wa kutubu dhambi, kumrudia Mungu kwa moyo wa dhati, kumwamini Yesu Kristo na kumpokea kwa imani mioyoni mwetu awe Bwana na Mwokozi wetu.

Tukifanya hivyo, siku ya mwisho itakapofika, hatutakuwa miongoni mwao watakaolia na kusaga meno, bali tutanyakuliwa hadi mbinguni na kupokea uzima wa milele.

Sources:
  • BBC – Theories about the end of the universe (Big Rip, Big Freeze, Big Crunch)
  • NASA – Research on expanding universe and dark energy
  • Biblia Takatifu – 2 Petro 3:12; Mathayo 24
View attachment 3561406
Amen
 
Mbona niliaga kwamba naenda katika maeneo mengine kupiga gospel.
Usiniambie hukusoma "farewell" yangu.
Nimeingia jana hapa sijakuona. Wewe ulikuwa wapi?
Jana nilitekwa my..
Ila nipo sasa aiseee nilikumiss sana sana jamn unajua mpaka nikahisi mybe umehama nchi.

Kiukweli moyo wangu leo unatirirka machozi ya furaha kwa uwepo wako set free..

Karibu sana sana sana ...
 
Mnalazimisha sana Sayansi iseme kama dini zenu,
Hii ni Kama vile tu Waislamu wanavyosema Quran yao inazungumzia Big bang
Naelewa unachomaanisha. Hata hivyo mimi siilazimishi sayansi “ikubaliane” na dini. Kila moja ina eneo lake: Sayansi inaeleza "How" (jinsi mambo yanavyotokea)na Biblia inaeleza "Why" (kwa nini yapo na yanaelekea wapi).

Nilichofanya ni kuonesha tu kwamba kuna kushabihiana kwa mawazo, sio kusema sayansi inaithibitisha moja kwa moja Biblia Takatifu, bali inaweza kueleza yaliyoandikwa kwenye Biblia kwa njia tofauti.

Kwa mfano, sayansi inasema ulimwengu una mwanzo na unaweza kuwa na mwisho, na Biblia pia inazungumzia mwanzo na mwisho wa ulimwengu. Hapo kuna convergence, sio “kulazimisha.”

Kwenye Sayansi kuna nadharia nyingi zinazobadilika kadri muda unavyokwenda. Lakini ukweli wa Biblia unabaki kuwa thabiti kwa waamini.
 
Ukitaka kujua tupo nyakati gani na tunaelekea wapi, tafuta unabii wa tatu na wa mwisho wa Bikira Maria wa Fatma alipowatokea Lucia, Francis na Yasinta, mwaka ule wa 1917.
Biblia ninayoiamini mimi haina unabii wa Bikira Maria wa Fatma.
 
Kiukweli moyo wangu leo unatirirka machozi ya furaha kwa uwepo wako set free..
Ukitubu dhambi zako na kukubali Yesu akuokoe, mimi nami moyo wangu utatiririka machozi ya furaha. Lakini kwa sasa moyo wangu una huzuni kwa kuwa umekataa kuokoka.
 
Kuna watu hawapendi kusikia habari za mwisho wa dunia. Dawa ni kuokoka tu. Ukiokoka unakuwa na amani tele, hata ukiambiwa mwisho wa dunia ni leo.
 
Hakuna mwisho wa Dunia ila Kuna mwisho wako
Shetani anatupofusha macho ya rohoni ili tuyaamini tunayoyaona kwa macho ya mwilini tu.Na kwa sababu hii,binadamu wengi hatuna imani kwamba asili yetu inatokana na Mungu baba mwenyewe.Lakini ukweli ni kwamba mwisho wa dunia umesababishwa na binadamu kumwasi Mungu.Binadamu tunapasa kuisikiliza sauti ya Mungu ili tujijengee imani na kumtumikia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom