Wanasayansi Wafichua Dalili za Mwisho wa Dunia!

Wanasayansi Wafichua Dalili za Mwisho wa Dunia!

Haya mambo yanajielezea yenyewe , hayahitaji ufafanuzi wako bwashee.
Una heri kama unayaona yanajieleza. Mimi nimewafafanulia wale ambao wana macho lakini hawaoni.
By the way, wewe umeokoka? Yesu akija leo, unao uhakika wa kunyakuliwa na Yesu?
 
Kataa kudanganywa na shetani.
Biblia sio ya wakoloni, ni ujumbe wa Mungu uliokuwepo kabla yao.
Yesu Kristo alizitaja dalili za mwisho wa dunia zamani sana kabla ya hao wakoloni kuja kukutawala.
Ukichagua kupuuza, ukweli hautabadilika kwa sababu umeukataa.
Ila nakusikitikia utajuta siku ya mwisho itakapofika na hautapata nafasi ya kutubu wala kumwamini Yesu. Neema itakuwa imefungwa.
Mkuu bila hao wakoloni hiyo biblia ungeijuwa wapi?
 
Walokole wote wanautamani huo mwisho wa Dunia kwelikweli dah! Mmechoka maisha eh? Tangu nimepata akili nusu karne sasa nasikia mwisho wa dunia umekaribia sana nawajua watu hadi wamekufa hawana kitu na maisha duni sana kwa kuwa mwisho upo karibu sana na ni zaidi ya miaka 20 sasa dah!
 
Mkuu bila hao wakoloni hiyo biblia ungeijuwa wapi?
Rafiki, usichanganye masomo. Kuna tofauti kati ya wakoloni na wamisionari. Biblia ililetwa Afrika na wamisionari Wakristo, sio wakoloni wenyewe. Wamisionari wengi walitoka Ulaya na walikuja kufundisha injili, kutafsiri Biblia, na kuanzisha makanisa.

Kama ulisoma Historia, kumbuka kuwa Ukristo haukuanza Afrika wakati wa ukoloni. Ukoloni ulipoingia Afrika tayari Ukristo ulikuwa upo Afrika mapema sana, hasa maeneo ya Misri na Ethiopia.

Yule towashi wa Ethiopia katika Matendo 8:26–39 aliamini kabla ya ukoloni.

Hata Kanisa la Koptiki (Coptic Church), mojawapo ya makanisa ya kale kabisa Afrika, lilikuwepo muda mrefu sana kabla ya ukoloni.

Wakoloni walikuja kutawala, kutwaa ardhi, madini, na kujinufaisha wao, lakini Wamisionari walikuja kuleta Injili na hata kusaidia watu kwa kujenga shule na hospitali. Mpaka leo bado kuna Wamisionari kutoka Ulaya, Amerika na Asia wanaokuja Afrika kuleta habari njema za Yesu Kristo anayeokoa na kuponya. Kama hao unawaita wakoloni, nakushauri ukabukue tena kamusi ya TUKI 😎

Cc: Bushmamy
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom