Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Kama huna habari, wanasayansi wamekuwa wakichunguza mwenendo wa ulimwengu (universe), na matokeo ya tafiti zao yamefichua jambo la kushangaza: ulimwengu hauko tuli, bali unapanuka kwa kasi kubwa sana.
Kupitia uchunguzi wa kina wa anga (astronomy), wamegundua kuwa kuna nguvu ya ajabu inayoitwa dark energy, ambayo ndiyo inachochea upanuzi huu wa ulimwengu. Nguvu hii inaonekana kuwa kubwa kuliko nguvu ya uvutano (gravity), na inaendelea kusukuma galaksi mbali mbali ziachane kwa kasi inayoongezeka kila siku.
Wanasayansi wametoa nadharia kadhaa kuhusu mwisho wa ulimwengu, mojawapo ni ile inayojulikana kama Big Rip. Nadharia hii inaeleza kuwa, kama hii nguvu ya upanuzi itaendelea kuongezeka, itafika mahali ambapo itashinda nguvu zote zinazoshikilia vitu pamoja, kuanzia galaksi, nyota, sayari, hadi atoms zenyewe. Hatimaye, kila kitu kitavunjika na kusambaratika kabisa.
Ajabu ni kwamba, nadharia hizo zinashabihiana sana na yale yaliyoandikwa katika Biblia Takatifu miaka mingi iliyopita. Maandiko yanatueleza kwamba siku ya mwisho inakuja. Siku hiyo mbingu zitateketezwa kwa moto na kutoweka, na viumbe vya asili vitayeyushwa.
Hivyo ni dhahiri mwisho wa ulimwengu unakuja, na utakuwa wa kutisha na wa ghafla.
Yesu Kristo alipokuwa duniani, kabla hajapaa mbinguni, alieleza dalili zitakazotangulia kurudi kwake na za mwisho wa dunia. Dalili hizo ni pamoja na kuongezeka kwa vita na machafuko, matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali, magonjwa hatari na yasiyo ya kawaida, kuongezeka kwa uovu na maasi, upendo wa watu wengi kupoa, watu kupenda fedha kuliko Mungu, kuibuka kwa manabii wa uongo nk.
Tukiangalia dunia ya leo, dalili hizo zinaonekana wazi mbele ya macho yetu. Hata mambo ya kusikitisha yanayoendelea huko Mashariki ya Kati, yalitabiriwa zamani kwamba yatatokea.
Inawezekana kabisa kwamba Mungu, kwa huruma zake, ameruhusu sayansi ithibitishe kwa njia hiyo kwamba mwisho upo ili hata wale wasiopenda kusikia Neno lake waujue ukweli huo.
Ndugu zangu, huu sio wakati wa kubeza wala kupuuza. Ufalme wa mbinguni umekaribia. Huu ni wakati wa kutubu dhambi, kumrudia Mungu kwa moyo wa dhati, kumwamini Yesu Kristo na kumpokea kwa imani mioyoni mwetu awe Bwana na Mwokozi wetu.
Tukifanya hivyo, siku ya mwisho itakapofika, hatutakuwa miongoni mwao watakaolia na kusaga meno, bali tutanyakuliwa hadi mbinguni na kupokea uzima wa milele.
Sources:

- BBC – Theories about the end of the universe (Big Rip, Big Freeze, Big Crunch)
- NASA – Research on expanding universe and dark energy
- Biblia Takatifu – 2 Petro 3:12; Mathayo 24