Wanapoua hadharani hawafungwi (Graphic Pictures); Maskini Tanzania

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,997
moz-screenshot-8.png
1.jpg

Kwa mara nyingine tena, kile kinachoelezwa kama 'wananchi wenye hasira, kimefanya kazi yake tena baada ya kumchoma moto wa tairi kijana aliyedhaniwa kuwa kibaka. Jamaa anaonekana kijana mmoja akimsaidia Israel kutoa roho ya kibaka huyo aliyedaiwa kutaka kuiba baiskeli kwenye nyumba ya mkazi mmoja maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam leo alfajiri. Jina la kijana huyo halikuweza kufahamika mara moja.

Kijana aliyedaiwa kuwa kibaka akiteketea kwa moto na kipigo huku akiwa amevishwa tairi.
….Kibaka akiteketea! .Dah!

PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL
 
Oh my goodness me!! If you had any doubts that ours is a lawless society, then look no further than this picture.

Halafu walivyokosa utu, wamesimama hapo wakimwangalia akiishia kuungua. Kwa kweli sisi tuko majitu makatili sana. Hata vibaka, wezi, na majambazi ni binadamu na wanastahili kutendewa kwa heshima na taadhima za ubinadamu.

Waliofanya unyama huu wana uhakika gani kama huyu marehemu ni kibaka? Na hata kama ni kibaka, adhabu waliyompa haiendani na kosa. Na kwa mtazamo wangu, hakuna kosa linalostahili adhabu ya kifo. I just don't believe in the death penalty.

What they did to him is so cruel and inhumane. We all ought to be ashamed and outraged by this.
 
vitendo kama hivi walitakiwa kufanyiwa mafisadi wa nchi hii kama lowassa na rostam, masikini kijana wa watu ameuwawa hivi hivi kutokana na hali ngumu ya maisha iliyoletelezwa na mafisadi wa hapa bongo.
 
Hii inatisha sana.

Hivi kwa Serikali ililiridhia kuondolewa kwa hukumu ya kunyongwa huko mahakamani wakati mitaani watu wanananyongwa na kuwanyonga wenzao kirahisi rahisi.

Serikali inatambua wazi matukio kama haya ni watu kuonyesha wazi hawana imani nayo.

Binafsi sioni tanzania kama tulikuwa sahihi kundoa hukumu ya kunyongwa
 
Oh my goodness me!! If you had any doubts that ours is a lawless society, then look no further than this picture.

Halafu walivyokosa utu, wamesimama hapo wakimwangalia akiishia kuungua. Kwa kweli sisi tuko majitu makatili sana. Hata vibaka, wezi, na majambazi ni binadamu na wanastahili kutendewa kwa heshima na taadhima za ubinadamu.

Waliofanya unyama huu wana uhakika gani kama huyu marehemu ni kibaka? Na hata kama ni kibaka, adhabu waliyompa haiendani na kosa. Na kwa mtazamo wangu, hakuna kosa linalostahili adhabu ya kifo. I just don't believe in the death penalty.

What they did to him is so cruel and inhumane. We all ought to be ashamed and outraged by this.
Ukiishi Manzese kwa mwezi mmoja utabadili kauli yako........hujawahi kutobolewa jicho na kibaka!
 
Ukiishi Manzese kwa mwezi mmoja utabadili kauli yako........hujawahi kutobolewa jicho na kibaka!

Hapana bana, I believe in the sanctity of human life. Kuua kwa namna yoyote ile, iwe kwa adhabu ya kifo, kwa kukusudia, kwa kutoa mimba, ni makosa.
 
Hapana bana, I believe in the sanctity of human life. Kuua kwa namna yoyote ile, iwe kwa adhabu ya kifo, kwa kukusudia, kwa kutoa mimba, ni makosa.
Ingekuwa poa sana kama kila binadamu angefikiri kama wewe. Tatizo we unafikiri hivyo halafu unakuta kuna muhuni fulani ambaye anaona poa tu kukupoteza kwa sababu anataka kuchukua kigari chako au fedha zako. Upo hapo? Sasa ukikutana na mtu kama huyu unafanyaje unamuangalia tu ili akupoteze au unampoteza wewe?
 
In self defence, I have no choice. I'll do what I have to do to protect and defend myself....
 
Oh my goodness me!! If you had any doubts that ours is a lawless society, then look no further than this picture.

Halafu walivyokosa utu, wamesimama hapo wakimwangalia akiishia kuungua. Kwa kweli sisi tuko majitu makatili sana. Hata vibaka, wezi, na majambazi ni binadamu na wanastahili kutendewa kwa heshima na taadhima za ubinadamu.

Waliofanya unyama huu wana uhakika gani kama huyu marehemu ni kibaka? Na hata kama ni kibaka, adhabu waliyompa haiendani na kosa. Na kwa mtazamo wangu, hakuna kosa linalostahili adhabu ya kifo. I just don't believe in the death penalty.

What they did to him is so cruel and inhumane. We all ought to be ashamed and outraged by this.

Well: Well: Well:

Haya maeneo (Tandale/Mabibo/Manzese) mimi binafsi nimeishi takribani miaka mitano! Kuna rafiki zangu wawili waliuawa (kwa kupigwa nondo kichwani) na vibaka na kuporwa simu ya Nokia (ya Tochi): Case ilikuwa reported police na uchunguzi uliendelea na mpaka leo haujaisha! Tulifanya utafiti "underground" kwa kuwatumia makachero binafsi na kuweza kuwafahamu hao vibaka. Of course na kufikia hatua ya kupata kufahamu nani mwenye kutumia simu hizo na aliuziwa na nani

Tulirudi tena police na ku-table "our investigation" - wakawakamata wale waliokuwa wanatumia hizo simu na waliwauzia - the entire chain - baada ya miezi miwili watuhumiwa wote walikuwa huru! na case ikaishia hapo! - Tulikubali yaishe. Police Station inayosimamia usalama wa maeneo yote niliyoyataja hapo ni Magomeni together with Urafiki police post. Kwa wale ambao in one way or another wamefika vituo hivyo vya police wanaweza kukubaliana na mimi kuwa yale ni magulio ya rushwa - If you can not afford to bribe "more" kuliko hata kibaka au jambazi - kesi inaweza kukufunga wewe uliyeibiwa au kufanyiwa ujambazi.

Kwa mantiki hiyo, Wananchi wa maeneo hayo hawaendi vituo vya police - bali wanafanya "uchunguzi binafsi" kama kuna incident yoyote - wizi au ujambazi - then wanaanza ku-trace wahusika : Now, kwa kuwa mwizi/jambazi ni vigumu kuacha, wanaanda "mtego" na akinaswa tu : TAIRI na Petrol huwa viko tayari - to take them to HELL!

Note: Ukifuatilia huyo mtu anayechomwa hapo, trust me and God, lazima atakuwa ameshakuwa reported either Magomeni or Urafiki kwa ujambazi/wizi not less than 20 times!
 
In self defence, I have no choice. I'll do what I have to do to protect and defend myself....
Umeona sasa kinachotokea hapa Bongo ni kuwa watu wana-habour hasira kwa muda mrefu maana kuna wahuni wengi tu wanaua watu na kuchukua mali zao na kupotelea kizani sasa inapotokea wanamdaka mtu yeyote anayetuhumiwa kufanya hivyo ndo wanamaliza hasira zao hao, ofcoz siungi mkono maana kwanza inawezekana siyo kweli kwamba mhusika ni kibaka halafu pia hata kama ni kibaka inawezekana siyo miongoni mwa hao wauaji otherwise kama kungekuwa na njia ya kuestablis on the spot kuwa kweli mtuhumiwa ni miongoni mwa hao wauwaji mi ningeunga mikono na miguu habari ya kuwapoteza lakini siyo kwa moto probably.
 
Hapana bana, I believe in the sanctity of human life. Kuua kwa namna yoyote ile, iwe kwa adhabu ya kifo, kwa kukusudia, kwa kutoa mimba, ni makosa.

Honestly, mi kibaka akinikalia kwenye reli, wont think twice...
 
Mzee Mwanakijiji.... Hivi vibaka, wezi au Majambazi wakiwahi kukutenda au kumtenda mtu wa karibu yako?? these people are ruthless... Mimi ni mtu wa Mungu, nawaombea kwa Mungu awabadilishe na awasamehe dhambi zao, lakini inapokuwa too much na wananchi wakachukua sheria mikononi... then I can only pray for their souls to rest in peace (if they will at all)... Hii inaonyesha kwamba wananchi hawana imani na judicial system tena...
 
Lakini kuua kwa kumvisha tairi shingoni na kulichoma moto....hiyo hapana bana. Bado sikubaliani nanyi. Mmomonyoka wa maadili ktk jamii yetu hii unatisha.
 
Uhalifu na adhabu zake unashangaza siyo tu kwa lay men and women bali hata kwa weledi!
Uhalifu mdogo huadhibiwa kwa adhabu isiyo a mfano - hata kupoteza maisha. Ukifanya uhalifu mkubwa mathalani wizi wa mabilioni... maisha yako yanaweza kuwa laini na hata utakavyochukuliwa ni tofauti, waweza kuonekana ni shujaa! Fundisho gani tunapata hapa? JIBU HATA MIYE SINA.
Bottomline..... uhai, utu vimetoweka. Ni maadili gani tunajenga kwenye jamii?
 
:A S-eek: Kuchomwa mto mpaka kufa??Hiyo adhabu hamna anaestahili......na hao wanaoangalia wana roho ngumu jamani!!LOH!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom