Wanaotakiwa kupisha uendelezwaji wa Mto Msimbazi waomba Rais Samia kuingilia kati suala la malipo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Baadhi ya wakazi wa Jangwani, jijini Dar es Salaam wameandamana wakiwa na mabango tarehe 3 Septemba, 2023 wakishinikiza kulipwa fidia inayostahili badala ya ile waliyothaminishwa kwa kulazimishwa huku wakiwa chini ya usimamizi wa askari wenye bunduki.

============= =================

photo_2023-09-05_09-45-31.jpg

Baadhi ya wakazi wanaotakiwa kuhama kupisha mradi wa uedelezaji wa Mto Msimbazi chini wa ufadhili wa Benki ya Dunia wamesema hawana imani na mthamini kiongozi ambapo wamedai katika zoezi la ulipaji fidia limegubikwa na utata.

Akizungumza Septemba 4, 2023, Saleh Seleman Cheyo, ambaye alijitambulisha kama Mwenyekiti wa Kamati Teule ya walioathirika na zoezi la kupisha uendelezwaji wa mto huo amesema zoezi la ulipaji fidia linafanyika bila kuzingatia taratibu ambapo amedai kuna baadhi ya kaya zimelipwa Sh. 27,000/= kama fidia ya makazi na mali nyingine zusizohamishika.

"Kabla ya kuja TAMISEMI alikuja mtu anaitwa Jangwani Holding alifanya uthaminishaji lakini alimaliza miaka sita bila kutulipa, kabla ya kukubaliana na Jangwani Holding, akaja TAMISEMI akawaambia wananchi nitawapa pesa taslimu na mengineyo lakini kinachofanyika kwa sasa ni aibu kuna watu wanalipwa elfu 27,000/= na wanafamilia."
photo_2023-09-05_09-45-37.jpg

Ameongeza kuwa mratibu wa zoezi hilo la malipo "Ameenda huko amekuja na karatasi za mfano wa malipo, tulipoenda kuzingalia kwanza tukagundua sio karatasi za malipo kwa sababu karatasi za malipo itakiwa iwe na maneno na tarakimu lakini zile walizotuletea pale TAMISEMI kama ni elfu mbili imeandikwa tarakimu (2000/=) hakuna maneno.

"Lakini pia wanazichapisha palepale, ukileta malalamiko mfano watu wale wenye nguvu flani wakilalamika wanawaongezea palepale tukaona hii sio haki, hizo pesa za kuongeza zinatoka wapi, tunasema kuna upigaji," amesema Cheyo.

Pia mkazi mwingine wa eneo hilo aliyejitambulisha kuwa ni kati ya wahanga zoezi hilo, Denisi mahanda amedai kuwa wao wanaunga mkono uwekezaji unaokudiwa isipokuwa wanapinga utaratibu unaotumika kuwaondoa, ambapo amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumulika zoezi hilo ambalo amedai kuwa linatekelezwa kinyume na sheria.
photo_2023-09-05_09-45-29.jpg

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakuita kama Mama sisi ni vijana na tuna Wazee wetu tumekuwepo hapa miaka mingi na watu wengi wamekuwa wakiliitaji eneo hili, lakini umeenda umetafuta wawekezaji kwanza tunakupongeza kwa kazi ya kutafuta wawekezaji umetuletea huyu World Bank.

"Lakini watendaji uliowapa kazi ya kutuondoa sisi hawakufuata Sheria na utaratibu wa uthamini, wamekuja wakaturubuni vizuri kwa maneno yao, walisema watatupa vitu vingi tu kwamba watalipa mpaka mimea watatupa ardhi kilometa 25, watatoa pesa taslimu lakini kilichokuja kutokea ni vitu ambavyo havistahili kufanyiwa binadamu kama sisi ambao ni Watanzania."
photo_2023-09-05_09-45-24.jpg

Kufuatia madai hayo amesema "Tunakuomba Rais Samia utusikilize na utusaidie, mthamini mkuu mpaka sasa hivi hatuna imani nae na uongozi wake maana kila tukifikisha kilio chetu kwake majibu yake hayatulizishi."

Aidha, Bi.Len Hamis (Msaidizi wa Mwekazina wa Wahanga) amesisitiza kuwa wanaomba Rais Samia Suluhu kuingilia suala hilo akidai malipo yanatolewa ni kidogo, huku akidai wakati wa zoezi la kusaini nyaraka za malipo kulikuwepo na mazingira ya usiri kuwatia hofu.

"Sisi kilio chetu tunaomba Rais wetu aingilie kati ili zoezi kwa sababu kilichotendeka ni uonevu katika kusaini, kulikuwa na kuitwa chemba ambapo ilituletea sintofahamu ya kuongezewa hela tulikuwa hatujui hela hizo zinatokea wapi, pia tulikuwa tumeshikiwa bunduki kama sisi ni wezi ambao sio watanzania wa Nchi hii.

"Tunamuomba Mh. Rais Samia Mwanamke mwenzangu ukumbuke huku Jangwani kuna wajane, kuna wamama wahanga.., hela tuliyopewa ni ndogo hazitoshi hata kututoa hapa kuweka makazi kwingine inatuumiza sisi Wanawake wenzako Mh. Rais ingilia kati uliowaleta kwetu wakatuahidi hakuna walichotekeleza," ameeleza Mama huyo.

Akifafanua zoezi la kuitwa kusaini nyaraka za malipo amesema: "Siku tulipoitwa kule kusaini tulienda kimakundi tulipofika pale tukajiuliza mbona hapa hukuna pesa lakini kuna ulinzi na bunduki kilitushangaza sana hicho tukaingia ndani tukakuta karatasi hapo unaambiwa usaini ukiangalia pembeni na nyumba kuna bunduki."

Kufuatia madai hayo wakazi hao walipoulizwa kama wamefanya jitihada za kufikisha madai yao kwenye mamlaka husika kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi, wamesema tayari wameandika malalamiko yao tayari yamefika kwa Mkurugenzi wa Jiji (Ilala) na Mkurugenzi wa Kinondoni sambamba na Ofisi Mbunge wa Ilala na Kinondoni pamoja na Mthamini kiongozi ambapo wamedai majibu waliyopewa mpaka sasa hayaridhishi.

Awali, itakumbukwa baada ya kuanza kuwepo taarifa za malalamiko ya Wananchi juu ya viwango vya fidia na mkanganyiko juu ya zoezi la uthamini wa makazi, ili kupisha Mradi wa Uendelezaji huo Serikali ilisema uthamani haukuhusisha ardhi isipokuwa mali zisizohamishika.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa Miradi ya Serikali inayofadhiliwa na Benki ya Dunia Mhandisi, Humphrey Kanyenye wakati akizungumza na Vyombo vya Habari na kuongeza kuwa, viwango vya fidia vimetokana na uhalisia wa mali zisizohamishika zilizokutwa wakati wa uthamini.

Amesema “Kilichofanyiwa uthamini ni kile kilichokutwa kwenye eneo husika, wengi walikuwa na matarajio makubwa lakini hatukuhusisha ardhi tumeangalia kile tulichokikuta kwenye eneo husika.”

Itakumbukuwa hatua za mchakato huo zilikuja baada ya Benki ya Dunia (WB) kukubali kutoa fedha kiasi cha Dola 100 milioni kwa ajili ya upanuzi wa Mto Msimbazi.


Pia soma:
- Serikali itusaidie wakazi wa Kigogo, fedha wanazotaka kutulipa kupisha mradi haziendani na nyumba zetu
 
Kuna wajanja waliongeza vibanda bila kujua wenzao walianza kuchukua picha za nyumba toka angani.
Mswahili ukimgusa atasema umempotezea cheni yake ya dhahabu wakati hajawahi kuivaa!
 
Huo mto unatanuka kwa kasi sana maeneo ya Gongo la mboto hatua zisipochukuliwa kuujengea ukingo soon utabomoa hadi reli zote mbili ya xamani na hii mpya
 
safi sana...tena huko uswailini ndio base ya ccm kwenye uchaguzi..mkihongwa wali na vitisheti na vibia basi mnasifiaga sana ccm..sasa subirin dawa iwaingie...na hakuna kurudi nyuma mdhamin keshapatikana muhame hapo..nenden kalalen kwenye ofisi za ccm zipo Kila Kona ya nchi....
 
Back
Top Bottom