Wanaotaka Muungano Uvunjike watoke kwanza Bungeni na BLW

Nadhani, somo hili la "oath" linahitaji kueleweshwa vizuri.
Lakini kwenye la kiapo nirudie hotuba ya Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere baada ya kuapishwa kama Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Disemba 9, 1962. Alizungumzia hivi kuhusu 'kiapo' maneno ambayo yangeweza kurudiwa kwa kila kizazi:

Yesterday I took an oath. I swore that as President of the Republic of Tanganyika I would to my duty and carry out my work without fear or favor, affection or ill will towards anyone. That was no hollow formula, to be spoken and forgotten. It was a most solemn promise, made before Almighty God, that with His help I shall prove myself worthy of the responsibility which you- the people of Tanganyika - have entrusted me; that I shall strive to fufill the task laid upon me without permitting myself to be of my comfort or convenience. I say "I' sore, but in actual fact it is true say that "we" swore; for I took that oath on your behalf. Every citizen of Tanganyika, whether he be the President, or a politician, a civil servant, a farmer, a teacher, or the lowest -paid worker in the land, every single one of us has an equal duty to give of his best. Every one of us has an equal duty to do the work entrusted to him - whatever that work may be - as if he too had taken a solemn oath to devote himself, without thought for his own advantage, to building our new Republic of Tanganyika".

Mzee Mwanakijiji.

Hiki kiapo, je Mwalimu alikivunja?
Aliapa kuitetea katiba ya Tanganyika na jamhuri ya Tanganyika.

Iko wapi Tanganyika leo? Ipo wapi katiba ya Tanganyika?

Hata kulibakisha jina la Tanganyika(territory ya Tanganyika) hakulibakisha badala yake ameiita Tanzania bara.
Mambo ya Tanganyika aka Tanzania bara yanaongozwa na katiba ipi?

Hivi kweli Mwalimu aliishi na kukitumikia kiapo hiki ulichokiweka hapa?

Kama unaona ni nje ya mada, basi tutaitafutia sehemu yake siku zijazo.
 
lakini kumbuka toka uhuru katiba zilifanyiwa marekebisho na kisha baadae kuwa na katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Anyway KIAPO KINAITAJI MADA MAALUMU.Mwanakijiji ataona mwanzo wake.
 
Ukishasema "argument inayotolewa kuhoji legitimacy yake haina mshiko" maana yake kunaweza kuwa na argument yenye mshiko. Ukishakubali kwamba kunaweza kuwa na argument ya legitimacy yenye mshiko, unakubali kwamba hoja ya legitimacy - whether a valid argument or an invalid one- ipo. Kwamba tunaweza kuhoji uhalali wa kiapo kwa msingi wa legitimacy ya misingi ya kiapo.

This is true; lakini the question here is not the legitimacy of the Union. The MPs hawahoji uhalali wa Muungano, maana wakihoji uhalali wa Muungano ni rahisi sana kuthibitisha kuwa ni Muungano halali. Mtu anaweza kuchukizwa na maisha ya ndoa au na vurugu za ndoa bila kulazimika kuhoji uhalali wa ndoa. Na hata watu wanaoamua kuachana wanaweza kufanya hivyo pasipo kulazimika kuhojia uhalali wa ndoa isipokuwa kama wanataka annullment.

Kama yule mtu anayekwambia "ndoa hii si halali kwa sababu huyu mume tapeli, aliponioa aliniambia hana mke na mimi ni mke pekee" na akadai kwamba kiapo chake cha ndoa si halali, basi na hawa wabunge nao wanaweza kutoa argument kwamba walivyoapa waliapa kwa nia nzuri tu, baadaye wakaja kuona mi document kuhusu muungano wakaona wamepelekwa mkenge kuapa kutetea muungano ambao msingi wake ni deception. Kama mtu ana valid arguments hii ni valid reason ya kubatili kiapo.

Absolutely true, lakini Muungano haukuingiwa pasipo uhalali; hawa hawahoji uhalali wa Muungano based on fraud or deception kwani wakihoji hilo wanaweza kufanya hatua nilizozisema hapo juu. Wao wanachohoji ni kutoridhika na Muungano. Well, kutoridhika na maisha ya ndoa hakuondoa validity ya ndoa. Kwamba, mke akikuudhi leo au watoto wakakikukorofisha huwezi kukimbilia kusema "ndoa haipo". Kiapo cha ndoa hakivunjiki au kuvunjwa kwa sababu mtu kapata hasira leo. Mtu anapofunga ndoa - japo si mfano mzuri sana - anadhaniwa kuwa anakubali majukumu na mambo yote yanayotokana na ndoa. Vinginevyo, watu wanaweza wakasema kuwa "nilipoingia kwenye ndoa sikujua kama mwenzangu ataumwa" na akiambiwa si ulisema "katika shida na raha?" na yeye kusema "yeah, lakini siyo shida hizi".

Inategemea na misingi ya kiapo hapo juu. Mfano wa kiapo cha ndoa una apply. Mke akiapa kudumisha ndoa ya mme/mke mmoja na penzi, kwa maelewano kwamba mume naye atafanya hivyo hivyo, baadaye mume akaenda kuoa mke mwingine, ingawa mke aliapa kudumisha ndoa, kitendo cha mume kuvunja kiapo kinampa mke grounds za kuvunja kiapo chake katika talaka.

Well.. unathibitisha ninachokisema kwamba kiapo alichokula mume cha kuwa na mke mmoja kilidhaniwa kuwa anamaanisha. Kwamba, aliposema atakuwa na Mke mmoja mke wake alitakiwa kuamini na hivyo kuamua kwake kwenda nje ni kinyume na kile alichoapa na hivyo kama ulivyosema "kinampa mke" grounds. Hicho ndicho ninachosema. Hawa watu wametaka tuamini kuwa waliposema kuwa watakuwa "waaminifu kwa Jamhuri ya Muungano" walimaanisha hivyo; hawakuapa kuwa watakuwa waaminifu wa Jamhuri ya Zanzibar au ya Tanganyika! HIcho kiapo kuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano kinaingiwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi kama ilivyo kwa viongozi wengine wa serikali ya Zanzibar akiwemo rais wa Zanzibar. Sasa wanapoamua kukivunja (kwa kutaka kuvunja Muungano) wanatupa haki wananchi kudai kuwa watoke kwanza nje ya hivyo viapo.

Nikitumia mfano wako wa ndoa (siupendi kwenye masuala ya muungano) ni sawasawa na mume na mke kukubaliana kuwa katika ndoa ya mke mmoja na mume mmoja. Sasa wakiwa katika ndoa hiyo waliyoapa kuingia mume anaanza kusema "nataka kuoa mke mwingine". Well thats fine lakini yule mke atamuambia huwezi kufanya hivyo ukiwa umenioa mimi! Ukitaka kufanya hivyo hata kutoa kauli za namna hiyo utoke kwenye ndoa hii kwanza. "Huwezi kutaka kuoa mke wa pili, wakati umekula kiapo cha kuwa na mke mmoja".

Lakini nikifuata mtiririko wa hoja yako unasema paraphrasing you - "haijalishi, viapo vinavunjwa"; unasema "kiapo cha mke mmoja na mume mmoja, kinaweza kuvunjwa pasipo matokeo yake". Hapa ndio tunatofautiana.

Kama mtu ana grounds za kuvunja kiapo anavunja vizuri tu.

Of course, lakini not with impunity! wakitaka kuvunja kiapo au viapo vyao wanaweza - ndicho nilichokisema toka mwanzo, lakini wakivunja wawe tayari kulipa gharama yake. Na gharama yake - kwa maoni yangu dhaifu - ni kuwa watoke kwanza Bungeni ili waishi na kuvunjwa kwa kiapo hicho. Hawawezi kuvunja kiapo halafu wakabakia kwenye Bunge hilo hilo ambalo waliapa ndani yake!
Vivyo hivyo, wanaotaka kuvunja muungano wakiweza kuthibitisha kwamba misingi fulani ya kiapo chao imevunjwa, wanaweza kutumia hilo kama sababu nzuri tu ya kuvunja viapo vyao.

Of course, lakini wakishapata huo msingi wa kuvunja kiapo, na wakiamua kuvunja kiapo watoke. Rais akivunja kiapo chake cha Urais hawezi kubakia kuwa Rais. It is that simple. Daktari akivunja kiapo cha udaktari hawezi kuendelea kana kwamba hakukivunja. Wakili akivunja kiapo cha wakili - na anaweza kuwa na legit reason ya kufanya hivyo - bado atawajibishwa kwa kuvunja kiapo hicho.

Kwanini huamini wanaovunja kiapo cha Ubunge wawe tayari kulipia uamuzi wa kuvunja kiapo hicho?

Si lazima, ukibatilisha msingi wa kiapo, na kama una watu wa kutosha waliokuchagua katika contituency yako wana support kuvunja muungano, utakuwa huna haja ya kujiuzulu ubunge.

Hii hoja tuliipitia the other day, wananchi hawawezi kumuunga mkono mbunge kuvunja sheria na yeye akasimama kuvunja sheria kwa vile kaungwa mkono na wananchi. As a matter of fact, it can even be argued - tukikubali hoja hii kidogo - hao wanaotaka Muuungano uvunjwe walifanya poll ya wananchi wao lini, na wananchi waliwapa hiyo mandate ya kutaka kuvunja Muungano lini?

Na kama ni kweli, kwanini huyo Mbunge alipoingia Bungeni aliapa kuwa "mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano" ambayo yeye alitumwa kuja kuivunja? Well ina maana alidanganya - kitu ambacho kinatosha kumvua madaraka yake au hakumaanisha kitu ambacho bado kinaonesha kuwa hakuwa mkweli.

Mbunge ni mtumishi wa wananchi, si wa serikali. Isitoshe, an argument can be made kwamba wananchi hawatakiwi kukaa bila uwakilishi, hata kama ni uwakilishi katika bunge la serikali batili, if that is the process to go to a more legitimate government.

Very true, lakini ni mtumishi wa wananchi kwenye mambo halali tu; hawi mtumishi wa wananchi katika mambo ya uhalifu. Kwa mfano, mbunge hawezi kwenda Bungeni na kutetea uhalifu kwa sababu baadhi ya wananchi wake ni wahalifu.

Point yako inaweza kuwa valid kwa mtu aliye kwenye baraza la mawaziri. It is absurd kusema unaona serikali ya Muungano haina legitimacy wakati wewe mwenyewe umo katika serikali. Lakini hata huyu, kama anafanya kazi kuivunja serikali hii ili kuje kuwa na a more legitimate government, naye anaweza kupata utetezi katika hili.

Point yangu is valid kwa watu wote wenye kula viapo vya ofisi au majukumu fulani.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Validity ya opposition kwa wabunge hawa ni kama ukisema hawana a registered backing from the people.

Likitokea kundi la watanzania zaidi ya 50% hawataki muungano, wana wa lobby wabunge wavunje muungano, wabunge wakiwakilisha maoni hayo watakuwa wrong?

Swala la muungano dawa yake ni referrendum tu. Hizi nyin gine zote ni roundabouts tu. Pigeni referrendum 2015 tujue moja. South Sudan wameonyesha njia.
 
Wabunge walioapa kuilinda TANGANYIKA mwaka 1961/1962 mbona waliiua mwaka 1964 kwa kuunda TANZANIA, principle hiyohiyo inashindikana vipi kutumika Kuivunja TANZANIA na kubaki na TANGANYIKA na Zanzibar?
 
Haijalishi wana backup ya watu wangapi; as long as wataapa kuwa faithful to the United Republic of Tanzania hawawezi kusimama kutaka kuvunja Muungano. Wakitaka kuwakilisha mawazo hayo ya kuvunja Muungano aidha wasiape kulinda huu Muungano au watoke (kama walishaapa).

Swala la muungano dawa yake ni referrendum tu. Hizi nyin gine zote ni roundabouts tu. Pigeni referrendum 2015 tujue moja. South Sudan wameonyesha njia.

Referendum si suluhisho la Muungano, referendum inakuwa na msingi tu (kama mfano wa South Sudan) ambapo Muungano haukuwa wa hiari. South Sudan ilipounganishwa chini ya Sudan kufuatia Uhuru wa Sudan haikuwa sehemu ya Sudan bali ilikuwa inahusiana na Misri. Hili ni kweli kwenye maeneo mengi yanayotaka referendum.

Tanzania kwa mfano, hakujawahi kuwa na referendum ya kuunganisha watu wa Tanganyika kuwa nchi moja; tuliletwa na Wajerumani na kuunganishwa zaidi na Waingereza. Hata hiyo Tanganyika is not a product of Tanganyikans. Sijui kama Watanganyika wote wangependa kuwa ndani ya Tanganyika hii au nje yake wakiulizwa. Lakini tumekubali kuwa ni nchi moja na tutamshangaa mtu kutoka Kagera akisema kuwa wanataka referendum ya kujitenga kwa sababu ya matatizo mbalimbali.

Ndio maana Ab Lincoln aliwakatalia Southeren States kujitenga na Union japo walikuwa na sababu za msingi zaidi kuliko za Zanzibar. Leo hii miaka nenda baada ya mafanikio ya USA masuala ya kujitenga yamebakia kuwa ni masimulizi. People want the easiest way out kwa sababu hawataki kuongoza kusimamia Muungano. We have weak leaders, weak politicians ambao hawana ujasiri wa kusema kilichowazi - nimeefurahi kuna mtu alimchomekea Mbunge huyo wa CUF leo kuwa "Muungano hauvunjiki"!
 
Wabunge walioapa kuilinda TANGANYIKA mwaka 1961/1962 mbona waliiua mwaka 1964 kwa kuunda TANZANIA, principle hiyohiyo inashindikana vipi kutumika Kuivunja TANZANIA na kubaki na TANGANYIKA na Zanzibar?

take time kidogo kabla hamjauliza maswali jamani. Duh. Vinginevyo mtanipa kazi kubwa kweli ya kufafanua hata vitu ambavyo with unaided reason inaweza kuvifikia.
 
Ni kweli wabunge wana immunity inayowapa haki ya kusema au kutetea uwakilishi wao. Immunity yao sio open kwa kila kauli ndiyo maana kuna kanuni za bunge zinazowaongoza. Endapo mbunge atasema serikali hii ina matatizo tuipindue, sio tu atakuwa amekiuka kanuni bali immunity yake inaweza kuwa revoked na akahitakiwa kwa treason.

Wabunge wameingia kwa sera za vyama vyao na wamekula viapo kuilinda na kuitetea katiba ya JMT. Walizisoma vyema sera ambazo zinatetea muungano(sijui kama kipo chama chenye sera tofauti) na wakakampeni kwa kutumia sera hizo. Katiba yetu inafahamika kwa maudhui yake, na hapa ndipo ninatofautiana na mfano wa Kiranga wa ndoa kuwa inaweza kutokea mtu hakujua jambo na akalazimika kuvunja ndoa.
Wabunge walijua ndani ya ndoa kuna nini kabla ya kuingia mjengoni, sio kuwa sisi ni South Sudan, tuna miaka 50 sasa.

Malecela aliambiwa hapaswi kutetea G55 kwasababu ni kuvunja katiba aliyoapa kuitetea. Tukumbuke alikuwa ni mbunge na alikuwa na immunity kama wengine. Nyerere akawambia G55 hiyo si sera ya chama na kama wanatofautiana nayo watoke ndani ya chama kwanza na kuunda kitu kitakachotetea hoja yao. Kwa ustaarabu ilikuwa na maana kama hawakukubalina na sera za chama tawala na wao kama Maleceala walikuwa wanavunja katiba waliokula kiapo kuitetea.

Hoja ya muungano izungumzwe na wabunge kwa ukamilifu wake, kama yapo mambo yatafutiwe ufumbuzi, lau ni makubwa basi taratibu zitumike kwa majadiliano yasiyo na lengo la uchochezi na zinazoheshimu katiba na kiapo. Tusipozingatia thamani za sera, katiba na viapo tukaacha immunity kwa wabunge itawale, ipo siku tutasikia mbunge anasema tupindue nchi, hapo sijui tutamlaumu!!

Ama wale wasio na uvumilivu au ustaarabu wa kutafuta muafaka kwa njia za amani basi watoke bungeni ili tujue hawana kiapo cha kuetetea kitu wasichokiamini, wajiunge na akina Mtikila waliokataa muungano siku nyingi na wapaze sauti zao kadri wawezavyo kwa sera zao zisozofungwa na katiba au kiapo.

Mimi ni miongoni mwa waliochoshwa na malalamiko yasiyo na msingi wala mashiko ya Wzbar. Ukiniuliza ifanyike nini nitakuambia ima kuwe na Legal challenge au referendum kwa Wzbar.
 
Muungano upo kisheria na unaweza kuvunjwa Kisheria, na itatakiwa wabunge wawemo bungeni ili sheria ya kuuvunja ipite

Technically Muungano unaweza kuvunjwa kwa baraza la wawakilishi kupitisha kifungu cha kuvunja muungano ndani ya katiba yao, kwa kuwa katiba yao ni sehemu ya katiba ya Jamhuri wa Muungano basi iwapo watafanya hivyo kutakuwa na "clause" ya kutokuwepo muungano ndani ya katiba ya Jamhuri ya muungano.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Taasisi, na ni wananchi ndo wenye kauli ya mwisho juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa Taasisi hii, kwa maana hiyo wananchi wanaweza kuamua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ivunjike zibaki nchi za awali, au Iungane na nchi nyingine yoyote, au wanaweza kuamua kuipa Autonomy Kagera ikawa na Shilingi yake, bendera yake n.k, kiufupi katiba ni mtumishi wa watu wakiamua wanaweza kuiondoa hata hiyo katiba iliyopo wakatengeneza nyingine.

Kwa kuwa kuapa kuilinda katiba hakumaanishi kutokuweza kubadirisha vifungu mbalimbali vya katiba, basi kifungu kinachohusu Muungano kinaweza kubadirishwa pia na hivyo kuuvunja au kuunda mwingine na nchi nyinginezo.
hicho kifungu kipya mathalani kinaweza kusomeka hivi, " Kutakuwa na mchakato wa mpito wa kuunda serikali ya Tanganyika na Zanzibar ndani ya miaka 10 tangu kipengele hiki kilipopitishwa na Bunge hili, ndani ya wakati huo Bunge Maalum la Kujadili hatima ya muungano litaketi, baada ya mjadala kufanyika kura zitapigwa, iwapo theluthi mbili ya wajumbe kutoka majimbo ya Tanzania bara na Theluthi mbili kutoka majimbo ya Zanzibar wataunga mkono Kuvunjika basi itatangazwa kuvunjika kwa muungano".

My point is, Njia iliyotumika kuunda huo muungano ndiyo hiyohiyo inayoweza kutumika kuuvunja!
 
Hawajaapa kuilinda Katiba tu; wameapa kuwa waaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Nimesoma hii prospective ya mwanakijiji na ni just opinion na sidhani kwamba wabunge kujadili au kuonyeshwa kwao kutopenda hizi foundations za muungano isiwe kosa. It should be free kuongea jinsi ya kurekebisha haya matatizo tulionayo juu ya muungano na sidhani ni vema kuwaweka wabunge wote au wananchi wanaotaka kubadilishwa kwa baadhi ya joints katika huu muungano wetu kama ni wakosaji. Inawezekana kabisa kuna maswala muhimu ndani ya huu muungano hayakuulizwa wala kujadiliwa kabisa kwa sababu Nyerere kiongozi wetu wakati ule alikuwa anapata only one side prospective na hatuwezi kuendelea na kicking the can down the road, it can bust and cause major major problem. Si kweli kabisa kwamba wote wanaojadili swala la muungano ni fringe people, I personally don't deny that there are fringe people kwenye hizi discussions na lazima tuwaonye wananchi but I am not going to be among those who like to condemn everyone.

Nikianzia kwenye maswala ya land, kuna tatizo hapa na ukweli upo kabisa kuhusu mtanzania bara akienda visiwani hatupewi rights za kununua land kama ipo for sale. Ukisoma hizo sheria za land visiwani utaona wazi zinatetea sana wao huko kama nchi nyingine vile lakini wao wakija bara they get things so easy and fast in exception panapotokea ufisadism. Ukiangalia revenues za muungano hazionyeshi kabisa formula gani inatumika ku-fund programs za visiwani na zipi zina-restrict only utumikaji bara. Maswala ya elimu na huduma za afya kunatofauti sana jinsi gani line imepitishwa kuhusu haya maswala.

Kikubwa kabisa ni constitutional ya muungano. Hii katiba ya muungano inaonekana kabisa ku-cover only sehemu za uchaguzi na hasa kumweka raisi wa visiwani lakini baada ya hapo kuna loop holes nyingi sana jinsi gani wao wanakuwa na katiba yao na sisi bara hatuna ya kwetu. Kwa kifupi ni kwamba sisi wabara tuna-summarize huu muungano kwamba visiwani wanakuwa favour na waovisiwani wana-campaign kubwa ya nationalism kulinda jamii yao away from wabara instead of building one nation. These are facts na hata tukitaka kufuta free and intellectual dialogs lazima zitaendelea ku-pop and one day they will break lose
 
Hakuna wakutoka hapo hawa ni njaa tupu, Mh Sita kamwaga kila kitu na kuwaeleza hizo kelo ambazo hazina msingi badala yake Jusa badalka ya kumjibu Sita bungeni eti kaenda kuitisha mkutano Unguja anamjibu Sita. Huu si uanajike huu mwanaume ankuambieni kama hamtaki tuvunje, sasa si ndo kila siku mnatka sasa mnataka nini? Tulikuwa hatui na kuwa kumbe ni serikali ya mapinduzi ililemewa swala la elimu ya juu, ikamba serikali ya muungano ilichukue. Sasa wanataka nini hawa?

Hata hao wawakilishi uelewa wa Zanzibar ni mdogo saana, ndo maana mtu anayedhani Zanzibar kuwa Singapore huyo anaota simulizi za kungwi, kwa kichwa kipi kutoka Zanzibar?

Kujadiliana na wewe ni kazi sana maana hata Kiswahili hujui. Isitoshe huna hoja ya maana na ndio maana unakimbilia matusi.

Kwa taarifa yako, nyinyi ndio mnaolazimisha huu "muungano" kwa kuweka majeshi yenu ya uvamizi Zanzibar.

Jussa akajibu wapi, kwani yeye Mbunge?

Wacha hizo bana.
 
Umewahi kufukiria hili? Mtu Mme na mtu Mke wananfunga ndoa kwa hiari kisha wanajaliwa mtoto Mwanamme. Baada ya muda Mtoto anaamua kuoana na mama yake na kwapamoja wanampeleka kusikojulikana baba wa mtoto ili mama na mwanae waponde raha!!! Asubuhi imefika Watanganyika. Amekeni msisinzie.
 
Nadhani labda imekuwa vigumu kueleweka. Hakuna tatizo kujadili hoja na kero za Muungano; hakuna tatizo kwa wabunge kutaka kubadilisha mambo fulani fulani na hata kutunga sheria za kuboresha mambo fulani. Kama kuna tatizo wana uwezo wa kufanya mabadiliko ya Katiba kama yanahitajika. Hayo yote hayana tatizo kwani ni ndani ya wajibu wao kama unavyoashiria. Kitu ambacho hawawezi ni kusimama na kusema "tuvunje Muungano". Hili haliwezekani. Kwa sababu, waliapa kuulinda na kuuboresha na Katiba inawapa jukumu la kufanya majadiliano yoyote kwa msingi wa "umoja wa Taifa" na Taifa na nchi ni moja yaani Tanzania.

Mbunge au Mwakilishi hawezi na hapaswi kusimama na kusema "mambo ni magumu tuvunje Muungano" hawezi kwa sababu hapo hatoi ushauri, hajaribi kupendekeza sheria wala nini anasimamia na kupigania kuvunja Muungano.

Salaam MKJJ,
Ni dhahiri kwamba wewe binafsi ni mtu mwenye 'Ethics' makini na unaamini katika hizo hupendi kuyumbishwa, Ni kweli hayo yote uliyoyasema yanatakiwa kuwa applicable, lakini, kama kiongozi anaweza kupinga ukweli ndani ya bunge 'mfano; Taarifa za ufisadi mfano wa rada ambazo zilipingwa kwa nguvu zote ndani ya hicho chombo (bunge) na wale wote walikula kiapo cha kutetea maslahi ya taifa kwa uwezo wao wote, na wanaoamini waliomba Mungu awasaidie, na bado wamepata aibu na sasa wanatumana kuomba chenji ije mifukoni mwao. Vivyo hivyo kashfa zote walizikanusha (walisema uongo bungeni) sasa kaka hawa hawajavunja katiba? Well, lets get back to the subject, Personally, may be sina ueleo mpana nahitaji msaada, can somebody tell beyond doubt, Muungano unafaida gani kwa hii pande ya pili? maake kuna nchi tayari inaitwa Zanzibar inawasilisha maombi UN kuhitaji kujitawala kama South Sudan! ile nchi ya pili kwenye muungano ni ipi?????? na inapata faida gani hizo (within the box ati ni nyingi na kubwa mno?) hebu nisaidie kufungua hiyo black box iitwayo Muungano, i am well capable of understanding clearly stated materials.

Another thing is, wale walioingia mkataba wa kirafiki, it is obvious they did not define what was within, mkataba ni nini? Well hawa ndugu wawili hawakuwa na common understanding that is JK the master, the teacher the civilised and everything you can say being flattered but upande wa pili Karume the 'kuli' who was scared of being turned down!

Hebu zungumza huku ukiwa na uamininwako wote kichwani if you could look at my eyes and tell me it is true muungano huu una faida yoyote kwetu, kama siyo wao tu 'Wavivu' {umeme bure, kodi hawataki kulipa} the list is inconclusive!

Wanatupotezea muda tu kwa kushika ghost positions {makamu wa rais, waziri wa mambo ya ndani, makatibu wakuu kibao, wafanyakazi kibao serikalini, mabalozi and so for} wote wanaziba nafasi zetu na za watoto wetu, mpaka kwenye nafasi za kusoma, mikopo ya elimu ya juu man etc, please nawaomba waungwana mtulie halafu tuuzungumze huo muungano, ni wa nchi zipi? na utachangiwa vipi, tusiogope serikali tatu au moja au serikali ya Tanganyika ninayoipenda pekee! miungano iko mingi Mbona hatuna namna ingine kama EA community ambayo nayo ilivunjika na sasa inataka kuungana tena? lets disolve within ourselves, digest the issue as a whole, and then decide, kama tunavyofanya EAC, mbona Rwanda, Burundi, uganda, Kenya, Mozambique, Congo DRC, Malawi, Zambia jamani all these countries have roots with Tanzania, ila tunapotaka kuungana, ni lazima tuuelewe huo muungano tunao uingia ama sivyo we are just scared to death imagining 'muungano' huu galasa utakapovunjika, STARTING WITH AN IMAGINATION OF THE TANGANYIKA COUNTRY, ambayo pia tutapenda tuigawe katika majimbo na muundo wa nchi hautaregea don't quote me wrong, nchi hii malalamiko yatapungua saana. look at the resources and imagine all are used to compete one another (majimbo) and then endeleza nchi, Wa-unguja do not even perceive muungano utakapovunjika itakuwaje, i tell you Tanganyika is a well developed country in the right imagination., nijibu MKJJ na unikaribishe!
 
Muungano upo kisheria na unaweza kuvunjwa Kisheria, na itatakiwa wabunge wawemo bungeni ili sheria ya kuuvunja ipite

Technically Muungano unaweza kuvunjwa kwa baraza la wawakilishi kupitisha kifungu cha kuvunja muungano ndani ya katiba yao, kwa kuwa katiba yao ni sehemu ya katiba ya Jamhuri wa Muungano basi iwapo watafanya hivyo kutakuwa na "clause" ya kutokuwepo muungano ndani ya katiba ya Jamhuri ya muungano.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Taasisi, na ni wananchi ndo wenye kauli ya mwisho juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa Taasisi hii, kwa maana hiyo wananchi wanaweza kuamua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ivunjike zibaki nchi za awali, au Iungane na nchi nyingine yoyote, au wanaweza kuamua kuipa Autonomy Kagera ikawa na Shilingi yake, bendera yake n.k, kiufupi katiba ni mtumishi wa watu wakiamua wanaweza kuiondoa hata hiyo katiba iliyopo wakatengeneza nyingine.

Kwa kuwa kuapa kuilinda katiba hakumaanishi kutokuweza kubadirisha vifungu mbalimbali vya katiba, basi kifungu kinachohusu Muungano kinaweza kubadirishwa pia na hivyo kuuvunja au kuunda mwingine na nchi nyinginezo.
hicho kifungu kipya mathalani kinaweza kusomeka hivi, " Kutakuwa na mchakato wa mpito wa kuunda serikali ya Tanganyika na Zanzibar ndani ya miaka 10 tangu kipengele hiki kilipopitishwa na Bunge hili, ndani ya wakati huo Bunge Maalum la Kujadili hatima ya muungano litaketi, baada ya mjadala kufanyika kura zitapigwa, iwapo theluthi mbili ya wajumbe kutoka majimbo ya Tanzania bara na Theluthi mbili kutoka majimbo ya Zanzibar wataunga mkono Kuvunjika basi itatangazwa kuvunjika kwa muungano".

My point is, Njia iliyotumika kuunda huo muungano ndiyo hiyohiyo inayoweza kutumika kuuvunja!

Njia iliotumika ni tofauti sana na kile ulichopendekeza huko juu Mkuu.

Muungano umekosa uhalali wa kisiasa na kikatiba.

Wakati wa kuunganishwa nchi mbili huru hizi hakuna kura ya maoni iliopigwa kuulizwa iwapo tunaridhia au la.

Sasa tupige kura ya nini tukitaka kurudi katika hali yu kama zamani?

Mkuu "muungano" huu ni bomu, uvunjie tu.
 
Mwandishi wetu, Dodoma

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameendelea kuuchokonoa Muungano na safari hii mbunge wa Viti Maalum, Mwanamrisho Abama (CHADEMA), ametaka uvunjwe kwa kufuata kauli ya Rais wa Zanzibar, hayati Abeid Karume.

Mbunge huyo alisema ni wakati muafaka sasa na kufuata kauli ya hayati Karume kuwa Muungano ni kama koti, hivyo linapokubana unalivua.

"Hayati Karume alishawahi kusema kuwa Muungano ni kama koti, likikubana unaweza kulivua, je Mheshimiwa Waziri Mkuu huoni huu ni muda muafaka wa kufuata kauli hiyo kwa kuuvunja Muungano kutokana na kero zilizopo?" alipoji mbunge huyo alipokuwa akiumuuliza Waziri Mkuu swali wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo.

Alishauri pia wananchi wa pande zote, Tanzania Bara na visiwani kupewa fursa ya kupiga kura ya kutoa maoni kuhusu suala hilo.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu, alisema kero zilizopo katika Muungano hazitofautiani na zilizopo katika nchi nyingine zilizoungana.

"Sidhani kama ni jambo la busara kuuvunja Muungano. Jambo hili tusilione jepesi, kwani Muungano umetujengea heshima na matatizo yaliyopo tutaendelea kuyamaliza siku hadi siku," alisema.

Pinda alisema kuwa anapata faraja kuona Wazanzibari wamejenga nyumba Tanzania Bara na wanaishi kwa amani na kuongeza kuwa pamoja na kero zilizopo, njia muafaka ni kujadili namna ya kuyamaliza matatizo yalipo

"Pinda alisema kuwa anapata faraja kuona Wazanzibari wamejenga nyumba Tanzania Bara na wanaishi kwa amani na kuongeza kuwa pamoja na kero zilizopo"
Na vipi wabara kujenga nyumba Zanzibar & Pemba? Hawafai?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom