Kuna Wawakilishi na Wabunge ambao wamekuwa wakitoa lugha ya kuonesha kuchoshwa na Muungano na bila ya shaka wanazo sababu ambazo wanaamini zinawapa haki ya kutoa hisia hizo. Lakini wapo wengine kati ya hao ambao wanatoa matamshi yenye kuashiria kupigania kuvunjwa kwa Muungano. Wapo wawakilishi wa vyama vyote ambao wamekuwa na kauli hizo za kutishia kuvunja Muungano hasa katika Bunge lililopita na hili la sasa. Ndugu zangu, hawa wawakilishi hawawezi kutoa kauli za kutaka kuvunja Muungano na wakabakia wawakilishi halali wa wananchi kwani kwa kutoa kauli za kuvunja Muungano wanavunja Katiba iliyowaweka hapo.
1. Wawakilishi wote hawa walisimamishwa kugombea nafasi zao au kupata nafasi zao kwa kudhaminiwa na vyama vya siasa ambavyo viliandikishwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria ya Vyama Vingi. Katiba na Sheria zinakataza kabisa kuandikishwa chama chochote ambacho kinapigania kuvunja Muungano. Hivyo, wote walisimamishwa na vyama visivyopigania kuvunjwa kwa Muungano.
2. Kutokana na hilo la kwanza, hakuna Mbunge au Mwakilishi ambaye wakati anagombea aliwaahidi wananchi kuwa ataenda kupigania kuvunja Muungano kwa sababu au kisingizio chochote kile. Wasingeweza kufanya hivyo wakati wa kampeni kwa sababu Katiba inawakataza na Sheria ya Uchaguzi ingewabana na kuwaengua mara moja. Kama hakuna chama kilichoandikishwa kwa ajili ya kuvunja Muungano hawa wawakilishi wanapata wapi mandate ya kutoa hoja za kuvunja Muungano?
3. Waliposhinda uchaguzi au kupewa ushindi wa chee waliingia Bungeni/BLW na kabla ya kuanza majukumu yao walishika misahafu na kuapa. Waliapa kwanza kabisa "kulinda, kutetea na kuihifadhi Katiba Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Ninataka kuamini kuwa walimaanisha viapo vyao. Kama walimaanisha walijifunga kuulinda Muungano siyo kuuvunja. Hivyo, kauli zozote za kutishia kuvunja Muungano au hata kuashiria kuwa "muungano uvunjike" ni kinyume na kiapo chao na hivyo ni kosa tosha kabisa la kumfanya Msajili aidha kukifuta chama cha siasa au kumtangaza huyo Mbunge/Mwakilishi kuwa amepoteza sifa za kuwa mwakilishi. Huwezi kuapa kulinda Katiba halafu ukasimama kutangaza kutaka kuivunja!
4. Kama 1,2 na 3 ni kweli basi Wabunge na Wawakilishi walioko kwenye nafasi zao sasa hawana haki, uwezo, madaraka wala mamlaka ya kuzungumzia kuvunja Muungano. Yote wanayoweza kufanya ni kuutetea na kuuenzi na kuulinda.
5. Kwa vile Katiba imeweka toka mwanzo kabisa (Ibara ya 1,2) kuwa Tanzania ni nchi moja na eneo lake ni eneo lolote la Tanzania Bara na Tanzania Visiwani na kuwa katika nchi hii moja kuna vyombo viwili vya utendaji yaani Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kauli zozote za kubadilisha serikali hizi mbili aidha kwenda serikali moja au serikali tatu nayo ni kinyume na Katiba! Wabunge hawawezi na hawapaswi kuzungumzia kubadilisha Muungano kwani Katiba Inawakataza isipokuwa kama wametekeleza utaratibu wa Katiba wa kubadili Muungano. Wameapa kulinda Nchi Moja, Serikali Mbili! Ndio maana wengine tulipuuzia na kubeza kauli ya Rais Kikwete kuwa Zanzibar ni "nchi ndani ya nchi" kwani haina mantiki na ni kinyume cha Katiba!
6. Kama 1, 2, 3, 4 na 5 ni kweli basi wabunge na wawakilishi wetu wanaachiwa uchaguzi mmoja tu nao ni kutatua kero za Muungano, kuondoa matatizo yaliyopo na kuboresha ili kuufanya Muungano uzidi kuimarika. Hawapaswi kuudhoofisha wala kutoa kauli za kuwachochea watu kuchukua msimamo wa kuuvunja. Siyo wabunge tu wale wote walioapa kulinda Katiba na hivyo kulinda Muungano wanalazimishwa na Katiba hiyo kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote.
Hii ina maana gani?
Kwamba, kama kuna Mbunge au Mwakilishi ambaye anaona kuwa Muungano haufai na hataki uwepo anaachiwa uamuzi wa kutakiwa kutoka Bungeni (ili asibanwe na kiapo) na kwenda kuanzisha harakati za kuvunja Muungano. Na kama kundi hili linaweza kupata wafuasi basi ni jukumu lao kutumia nguvu zao zote (na hapa neno ZOTE nalimaanisha) kupigania kuvunja Muungano na kwa kufanya hivyo wajue wameamkua kupambana na vyombo vilivyopo vyenye kulinda Muungano. Kama hoja yao inaweza kuwa na nguvu sana na kupata wafuasi wanaweza kujikuta hatimaye wanalazimisha Muungano kuvunjika aidha kwa njia ya amani au kwa vurugu. Kwa vile Muungano wetu haukuwa wa ku-annex Zanzibar ni wazi unaweza kuvunjwa kwa njia ya amani kabisa. Muungano wetu siyo kama ilivyokuwa Ethiopia na Eritrea au Sudan na Sudan Kusini au Russia na Georgia au Ukraine au zilizokuwa Jamhuri za Yugoslavia. Tanganyika haikuivamia Zanzibar na kuichukua kwa nguvu. Ulikuwa ni Muungano wa Hiari ambayo kusema ukweli ni vigumu sana kuuvunja licha ya majaribio ya baadhi ya watu kujaribu kuwafanya Watanganyika wajisikie kama waliivamia Zanzibar. Ni vigumu kuvunja Muungano wa hiari.
Hivyo, wale walioapa kulinda Katiba na Muungano na sasa wanataka kuvunja Muungano huo hawalindwi na kinga za Bunge wala Uhuru wa Mawazo kwani mwanafamilia hawezi kuja na dumu la mafuta ya petroli na kiberiti mkononi na kuanza kudai kuwa pale Nyumbani watu hawampendi na hawamjali na hivyo ameamua kuichoma nyumba moto na watu wasema ati "ni uhuru wa maoni". Pale Bungeni Mbunge hawezi kusimama na kupiga kelele "moto moto" halafu watu wakikurupuka kukimbia asema "analindwa na haki na kinga za Bunge kusema lolote Bungeni".
Waondoke kwanza Bungeni na BLW ili waanzishe hoja za kuvunja Muungano; hawawezii kufanya hivyo wakiwa bado wamefungwa na viapo vya kuulinda Muungano huo.
Katika sheria kila muungano unavunjika, hakuna muungano usiovunjika, labda ukose mwanasheria mbishi uzuri.
Hata hizo atoms zinazounganishwa kwa nuclear force naturally zinavunjika katika radioactivity, itakuwa hizi artificial man made entities ?
Cha kufanya hapa ni kuitisha country wide referrendum, ili muungano uendelee inabidi upate baraka za at least a simple majority kote bara na visiwani. Hili litakata mzizi wa fitina, watakaoutetea muungano watasema wanautetea kutokana na mandate ya watu.
Muungano uliopo umekuwa shoved down peopl'e throat, hakuna Mtanzania aliyeupigia kura au ku u endorse directly.
Hata kama mtu alikubali muungano, hili halina maana kwamba hana haki ya kubadili mawazo yake.
absolutely.. hii hapa si hoja; hoja siyo kama Muungano uvunjie au usivunjike au hata uhalali wa Muungano. Hoja ni kuwa waliapa kuulinda - tena hata leo Mbunge mwingine kazungumza hivyo hivyo Bungeni kusema "wakati umefika" Muungano uvunjwe. Well.. aidha walimaanisha walichoapa au hawakumaanisha. Rais wa Marekani kwa mfano au seneta wa marekani hawezi kuzungumzia "lets break up the union" na akaachwa hivi hivi.
Nadhani Kila mmoja wetu anafahamu swala la muungano limekuwa likiisumbua serikali zote Nne zilizowai kuwa madarakani na kama mnakumbuka G7!n.k.Lakini huu muungano siyo maisha ya watanzania Bara wala siyo maisha ya Wazanzibar,bali Muungano nikitu tu kipo ambacho kiliwekwa kwa ajili ya kuunganisha tamaduni zetu baina ya Bara na Visiwani,Lakini ukiangalia kwa umbali utaona tangu Muungano huu uwepo kumekuwepo na kasoro nyingi japo zimekuwa zikirekebishwa!Nazote zimekuwa zinarekebishwa kwa ajili ya kusaidia upande mmoja wa Visiwani!Kwa maana hiyo siku zote Hawajaridhika na marekebisho hayo! nakumbuka sisi tulikuwa tukienda Zanzibar na Passpoort,lakini wao wanakuja huku bila hata karatasi ya mjumbe!.Matokeo yake wamekuwa wakilalama na kutukebei juu ya Muungano wetu ulio anzishwa na Na wa asisi wa nchi hizi mbili Tanganyika na Zanzibar leo Tanzania!Kwa kasumba ya Wazanzibar hata mngewafanyiwa nini hawawezi kuridhika na kwakuwa wao ni wabinafsi ndiyo maana leo wewe toka hapa Tanzania bara nenda Tanzania visiwani huwezi kubata hata nyumba ya kupanga achilia kiwanja!.Mimi naona wauvunje huu Muungano hauitajiki kwa wa Zanzibar lakini wanasahau kama wao ndiyo wanaofaidika na Muungano huu! Kuanzia Kodi mpaka vyeo!Hivyo tusiendelee kukumbatia Nyuki wakati tuanaumia!!. Nasema Serikali ijue inaweza ikautaliki Muungano Tuachane na mabo haya alianzisha fulani hiyo nikudumisha Fkira za mwenyekiti ni mambo yaliyopitwa na wakati!!!
absolutely.. hii hapa si hoja; hoja siyo kama Muungano uvunjie au usivunjike au hata uhalali wa Muungano. Hoja ni kuwa waliapa kuulinda - tena hata leo Mbunge mwingine kazungumza hivyo hivyo Bungeni kusema "wakati umefika" Muungano uvunjwe. Well.. aidha walimaanisha walichoapa au hawakumaanisha. Rais wa Marekani kwa mfano au seneta wa marekani hawezi kuzungumzia "lets break up the union" na akaachwa hivi hivi.
Kiapo nacho ni muungano, kinamuunga mtu na principle fulani.
Kama muungano unavyoweza kuvunjwa kwa sababu ni man made, kiapo nacho kinaweza kuwa nullified based on new info.
Swala ni kuuliza basis yao ku nullify kiapo. Mtu anaweza kusema ana nullify kiapo chake kwa sababu misingi ya muungano imekiukwa, nchi imeoza, etc.
Ni kama mtu aliyetoa confession kituo cha polisi, akatia saini, anaweza kwenda mahakamani akadai kwamba alitia saini under pressure.
Kwa hiyo kiapo si deal.
Kama kiapo si deal watu wasingekuwa wanashtakiwa kwa perjury or "lying under oath". Na kiapo cha ofisi ni tofauti na kiapo cha ushuhuda kwani kiapo cha ushuhuda kinahusiana na kusema kile ulichoshuhudia kwa ukweli wote. Kiapo cha ofisi kinahusiana na kukubali wajibu, madaraka, haki na kazi zinazotokana na kiapo hicho. Hivyo, kama Rais anakula kiapo cha ofisi ya Urais au Mbunge cha Ubunge maana yake hawa wote wanakubali majukumu yanayotokana na kiapo hicho.
Kiapo hicho cha kazi kinaitwa "Kiapo cha Uaminifu" na mtu kama Rais au Jaji anakula pia kiapo cha ofisi yake. Ndio maana basi kiapo hicho kinasema (as far as I can remember):
''Mimi (Mbunge atataja jina lake), naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote, na kwamba nitaihifadhi, nitailinda na nitaitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyowekwa kwa mujibu wa sheria. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.''
(Msisitizo wa kwangu)
Haya maneno yanaweza yasiwe na uzito au yakawa na maana na watu wakachukulia kirahisi rahisi tu; lakini ukiyaangalia yanafuta kabisa uwezekano wa mbunge huyo kutaka Muungano uvunje.
Kiapo kimetolewa kwa misingi fulani, ukiweza kutoa argument kwamba misingi ya kiapo imevunjwa, kwa mfano nchi haifuati katiba, unaweza kuvunja kiapo.
Ndiyo maana nikasema kitu muhimu ni basis yao ya kutaka kuvunja kiapo/ muungano.
Hata ndoa ina legal na religious grounds for divorce.
Wewe unaongelea utakatifu wa kiapo? Kuna watu wana debate legitimacy ya idea nzima ya nchi -nchi yeyote ile-, achilia mbali muungano wa Tanzania na viapo vyake.
But that's a totally separate ballgame.
Hoja ya legitimacy haipo; ndio maana hata sijaribu kuiangalia kwa sababu argument inayotolewa kuhoji legitimacy yake haina mshiko. Hata hivyo kama hao wabunge wangekuwa wanahoji "legitimacy" ya Muungano wasingeapa kuwa waaminifu kwa muungano huo. Kwa kukubali kula kiapo cha kuwa waaminifu kwa "jamhuri ya Muungano wa Tanzania" wameondoa uwezo wote wa kuhoji legitimacy yake.
Lakini hata kama kungekuwa na hoja ya legitimacy, bado kunaleta shida. Kwanini waliapa kuwa waaminifu kwa kitu ambacho wanamashaka na uhalali wake?
In both counts, hawa walioapa hawawezi kuwa wao ndio wanasimama na kusema tuvunje. Walioapa kulinda na kuhifadhi na kuwa waaminifu wanatarajiwa kusimamia kile walichoapa kukifanya.
Kama wanaona kuwa hawawezi kuendelea (katika dhamira safi) na bona fide basi wajitoe kwanza Bungeni au BlW ili waweze kusema kweli wana matatizo na Muungano. As long as they are sworn to be faithful to the United Republic of Tanzania, the people have to hold them accountable to that oath. Shouldn't they?
Mwanakijiji nadhani kusema wabunge wanaotaka muudo tofauti ya muungano watoke ni sawa na majibu ya ndugagai alimwambia Halima mdee kuwa zile posho za wabunge zilivyopitishwa hakuwepo na ka kama hawazitaki basi warudishe zote.
Mbunge sio Rais.. Angekuwa ni Rais au Waziri naweza kukuelewa lakini kwa mbunge hana ulazima wa kuachia ubunge ili atetee muundo wa serikali ulio swa kwa mtazamo wake au wananchi anaowakilisha.
Sababu tunategemea wabunge waheshimu kanuni za bunge zikiwemo na kanuni za posho zilizopitshwa kihalali na bunge. Lakini kwa mbunge kuhoji na kukataa uhalai wa oposho haina maana anavunja kanuni za bunge.
Tunategemea wabunge wawe na uwezo wa kuichallenge hata katiba kama ni kwa maslahi ya wananchi.
Yesterday I took an oath. I swore that as President of the Republic of Tanganyika I would to my duty and carry out my work without fear or favor, affection or ill will towards anyone. That was no hollow formula, to be spoken and forgotten. It was a most solemn promise, made before Almighty God, that with His help I shall prove myself worthy of the responsibility which you- the people of Tanganyika - have entrusted me; that I shall strive to fufill the task laid upon me without permitting myself to be of my comfort or convenience. I say "I' sore, but in actual fact it is true say that "we" swore; for I took that oath on your behalf. Every citizen of Tanganyika, whether he be the President, or a politician, a civil servant, a farmer, a teacher, or the lowest -paid worker in the land, every single one of us has an equal duty to give of his best. Every one of us has an equal duty to do the work entrusted to him - whatever that work may be - as if he too had taken a solemn oath to devote himself, without thought for his own advantage, to building our new Republic of Tanganyika".
Ninavyowasoma ndio ninaona tuna tatizo kubwa; mtu ameapa kufanya kitu hafanyi kwa sababu zake halafu tunashindwa kumbana kwa sababu tunafikiria kuwa ana uhuru wa kutokufanya. Viapo (oaths) ni vitu vizito sana. Tukikubali wabunge waape kulinda Katiba halafu tukasema wasisimamie kiapo chao kwanini tuamini watu wanaoitwa mahakamani na kulishwa kiapo watarajiwe kusema kweli kama hawamaanishi kiapo chao?
Rais amekula kiapo cha kazi ya Urais na ndani ya kiapo hicho cha kwanza ni kulinda Katiba. Sasa Rais huyo huyo akianza kuvunja Katiba kwa kisingizio cha "maoni tofauti" ataweza vipi kuendelea kuwa Rais? Kama tunamkubalia avunje kiapo chake kwenye jambo moja kwanini tusimkubalie kwenye mambo mengine? Wabunge wamekula kiapo kulinda Katiba, sasa wasipoilinda tusiwaulize? Maana kama viapo havina maana ni bora kutokuvishika, sivyo?
Au tuwape uchaguzi wanapokula viapo - wachague ni mambo gani wataapa kuyalinda ili tusipate shida ya kuwaliza. Kwa mfano, wabunge wanapoapa wasema "Naapa isipokuwa kwenye kulinda Muungano"...