Wanaotaka Muungano Uvunjike watoke kwanza Bungeni na BLW

Mkuu Mwanakijiji.

Muungano ni off-limit katika siasa za Tanzania?
Je Muungano wa Tanzania unatoa nafasi kwa nchi nyengine zinazotaka kujiunga nasi kuweza kufanya hivyo?

Kama muungano uliundwa kwa nini usiweze kuvunjwa vilevile?

Nani mwenye haki ya kuuvunja muungano?
Ili uvunjwe hatua zipi inapasa zichukuliwe?

Mikataba ya kimataifa huwa na exit- clause... je huu Muungano wetu hauna kipengele hiki? Kama hauna huoni ni mapunguvu makubwa hayo?

Je huu Muungano wa Tanzania utakuwa muungano wa kwanza duniani kuvunjika? Mbona miungano mengine ilikuwepo na imevunjika?
Senegambia ni mmoja wapo!
Hata nchi moja inagawanyika...mfano Sudan..sasa zipo Sudan mbili.

Kama sheria ya usajili wa vyama hairuhusu chama kupinga muungano au kutaka kuvunja muungano.
Ni njia ipi itumike kuvunja Muungano...ipiganwe vita kama Sudan? au maandamano ya wananchi (uprising)?

Kwa nini iwe marufuku kuujadili muungano wa Tanzania? Na wanaoleta mjadala wa Muungano waonekane wamepotoka?

Katiba yenyewe " bomu"..ni katiba ya mfumo wa chama kimoja,chama cha magamba.

Tushukuru kuwa wananchi wameonesha ustahamilivu wa hali ya juu na siasa za mazingaombwe za Tanzania. Tumeona katika nchi nyengine ni vita tu.

Tukumbuke hakuna marefu yasiyo na ncha! Mtanzania zilizokuwa zimelala zinaanza kuamka kidogo kidogo!

mwanzoni watu wamezungumzia kero za Muungano ambazo hazitatuliwi na wala hazitatuki...sasa Muungano wenyewe ndio umekuwa kero.

Nyumba yenye nyufa nyingi iko siku itabomoka tu. Muungano wenye faida kwa pande zote ungekuwa na malalamiko machache. Huu wa kwetu malalamiko yanazidi kila jua linapochomoza na chuki inajengeka katika jamii.
 
Sie mbona hatujawasikia hao wabunge wa kufirika kama wewe umewasikia wataje majina.
 
Ahaa haa umenikumbusha mchezo wetu wa kitoto.

Tema, ni teme chakula?
Meza, nimeze moto?

Sasa utafanyaje? nitamung'unya tu!

Sasa, Mwanakijiji wakiwa nje ya bunge watapata wapi nguvu ya kusikilizwa na kutekeleza matarajio yao? na je wanaapa kulinda katiba au kulinda Muungano? kama wanaapishwa hivyo basi kuupinga ni uhani, na hivyo walipashwa kuomba kubadilishwa aina ya kiapo. Kama wakina Marando walipoingia Bunge la mwanzo walifanikiwa kubadili kiapo cha wabunge kwa kukataa kuapa kumtii rais wa Jamhuri ya Muungano mpaka kiapo kilibadilishwa na kutoa hilo neno.

Yeah.. ndiyo ninachokisema. Rais, Mbunge au Waziri (wa Muungano au Zanzibar) hawezi kuapa kulinda na kutetea halafu akasimama kutaka kuvunja!
 
Yeah.. ndiyo ninachokisema. Rais, Mbunge au Waziri (wa Muungano au Zanzibar) hawezi kuapa kulinda na kutetea halafu akasimama kutaka kuvunja!

Hawa Wabunge na viongozi tuliona hao hawawezi kuuvunja Muungano wanautaka na wanauthamani, tatizo walilonalo ni uwezo wao wakuwaelimisha wananchni wao juu ya nini umuhimu wa Muungano na kuutetea adharani, mtu aliyekuwa na ubavu huo alishakufa.

Pili tuna aina ya wanasiasa ambao mimi nawaita wanafki, yaani wanasikiliza wananchni wanaongea nini na wao wanatumia hayo mambo ambayo wananchni wanayalilia kuwaadaha kupata kura hata kama anajuwa kuwa hataweza kuyatekeleza, na hawana ubavu wa kuwaeleza wananchni kuwa mimi Mr. so and so naombeni ubunge, na kuhusu ndoto zetu nyie wananchni wa unguja wa kujitenga na Muungano mimi siungi mkono kwasababu ina madhara kadha wa kadha na muungano ina faida nyingi kama zifuatazo: --.......... na hivyo tuutete sote....

Hivyo ukiona wanaongea na kufanya chokochoko lengo lao siyo kuvunja bali ni kuendeleza ile adahaa yao iliaonekane yeye ndio anafaha zaidi huku akijua anatwanga maji na kuwaadaha wapiga kura wake, Hao ndugu zetu ndio wanaofahidi kila kitu hapa Bara na wanajuwa fika kuwa wananchni wao wanaupofu juu ya ukweli ila hawataki na wanaogopa kuwaeleza ukweli siku zote. Wavunje Muungano wataenda kuishi wapi na kumiliki wapi ardhi hekari zote wanazo miliki bara, na nyumba za serikali za bure na nafasi kibao za ubunge wanazopata kutokana na Muungano watazitowa wapi maana hadi kata zina wabunge ukilinganisha ukubwa na wingi wa watu.
 
Mkuu Mwanakijiji.

Muungano ni off-limit katika siasa za Tanzania?

maswali yako yote ni mazuri kweli na majibu yake bila shaka yako wazi. Hata hivyo hayagusi tatizo lililopo. Wameapa kulinda Muungano vipi watake kuuvunja au kuashiria kuwa "uvunjwe"? Huwezi kuapa kulinda kuku halafu uwe wa kwanza kutaka kuwachinja!
 
Yeah.. ndiyo ninachokisema. Rais, Mbunge au Waziri (wa Muungano au Zanzibar) hawezi kuapa kulinda na kutetea halafu akasimama kutaka kuvunja!
Alafu akitoka so what? ndio katiba inamruhusu? whatever it can be, issue itazunguka na mwisho wa siku lazima hao walioapa kuulinda muungano ndio watatoa maamuzi ya kuuvunja pia.
Mkuu ukileta hiyo theory yako hakuna kitu kitafanyika kwa mgongo huo wa kukiuka kiapo.
Sijui kwa zanzibar lakini kwa bara hakuna anayetamka au kupigania muungano uvunjwe zaidi ya kutaka kero za muungano zishughulikiwe
 
Hivyo ukiona wanaongea na kufanya chokochoko lengo lao siyo kuvunja bali ni kuendeleza ile adahaa yao iliaonekane yeye ndio anafaha zaidi huku akijua anatwanga maji na kuwaadaha wapiga kura wake, Hao ndugu zetu ndio wanaofahidi kila kitu hapa Bara na wanajuwa fika kuwa wananchni wao wanaupofu juu ya ukweli ila hawataki na wanaogopa kuwaeleza ukweli siku zote. Wavunje Muungano wataenda kuishi wapi na kumiliki wapi ardhi hekari zote wanazo miliki bara, na nyumba za serikali za bure na nafasi kibao za ubunge wanazopata kutokana na Muungano watazitowa wapi maana hadi kata zina wabunge ukilinganisha ukubwa na wingi wa watu.

of course najua hivyo; ndio maana nataka tuwawajibishe ili waonekane kweli wanasimamia wanachoamini na wasitumie hadaa. Kama kweli wanataka Muungano uvunjwe si lazima wawe Bungeni - mahali ambapo waliapa kuulinda. Kama hicho wanachokisema ndicho wanachokiamini warudi mitaani na kuanza harakati za kuvunja Muungano bila kufungwa na kiapo cha kuulinda.
 
a. Uliapa kuilinda Katiba Mheshimiwa fulani?
Naam niliapa kuilinda lakini sikuapa kutoibadirisha au kutunga mpya
b. Ulimaanisha kiapo chako au uliapa tu ili uingie Bungeni?
Kabisa Mh Spika, nilimaanisha nilichoapa
c. Kama ulimaanisha iweje uzungumzie kuvunja Muungano?
Haya nizungumzayo siyo yangu mheshimiwa Spika bali wananchi ninaowawakilisha hapa Bungeni
d. Chama chako kina sera ya kuvunja Muungano?
Chama changu hakina sera ya kuvunja Muungano, isipokuwa wananchi wa jimbo langu wenye vyama na wasio na vyama wengi wanataka muungano uvunjike, na sitegemei mheshimiwa Spika kuwakilisha ilani ya Chama Changu humu bungeni bali maoni ya wananchi walionituma.
e. Ulipofanya kampeni uliwaahidi wananchi kuwa utapigania kuvunja Muungano?
Wala sijawahi kuzungumzia suala la muungano katika kampeni zangu Mheshimiwa Spika, hata hivyo hii hainizuii kuwakilisha maoni ya wananchi wa jimbo langu.

MY TAKE:
Wale waliounda Muungano mwaka 1964 eti hawakuvunja katiba kwa Kuiua TANGANYIKA waliopa kuilinda hapo awali, lakini eti hawa wa leo wahesabiwe kuivunja katiba walioapa kuilinda kwa Kwa kuivunja TANZANIA.

Mwanakijiji hebu yageuze maswali yako kwa Raisi na wabunge wa Mwaka 1964 pale walipofanya muungano uone yatajibiwa vipi?
 
Naam niliapa kuilinda lakini sikuapa kutoibadirisha au kutunga mpyaKabisa Mh Spika, nilimaanisha nilichoapaHaya nizungumzayo siyo yangu mheshimiwa Spika bali wananchi ninaowawakilisha hapa BungeniChama changu hakina sera ya kuvunja Muungano, isipokuwa wananchi wa jimbo langu wenye vyama na wasio na vyama wengi wanataka muungano uvunjike, na sitegemei mheshimiwa Spika kuwakilisha ilani ya Chama Changu humu bungeni bali maoni ya wananchi walionituma.Wala sijawahi kuzungumzia suala la muungano katika kampeni zangu Mheshimiwa Spika, hata hivyo hii hainizuii kuwakilisha maoni ya wananchi wa jimbo langu.MY TAKE:Wale waliounda Muungano mwaka 1964 eti hawakuvunja katiba kwa Kuiua TANGANYIKA waliopa kuilinda hapo awali, lakini eti hawa wa leo wahesabiwe kuivunja katiba walioapa kuilinda kwa Kwa kuivunja TANZANIA.Mwanakijiji hebu yageuze maswali yako kwa Raisi na wabunge wa Mwaka 1964 pale walipofanya muungano uone yatajibiwa vipi?
Atachakachuwa, si ndio wale wale!
 
Mwanakijiji

Nakupa heko

Big UP

These dudes just do not know what they are discussing about
 
ngoja niseme tena...kile kiapo cha 'naahidi kuilinda, kuitetea na kuihifadhi katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania' kiliboreshwa mwaka 1995 kwenye mabadiliko ya katiba. Maana yake nini? Kulikuwa na wasiwasi upande mmoja wa muungano ungeangukia kwa wapinzani na pengine wangetaka kuuvunja muungano. Kiapo kile kiliwekwa kama kitanzi.
 
Mzee Mwanakijiji,
Kama sijakusoma vizuri naomba unisahihishe lakini nadhani unakosea unaposema wanaotaka muungano uvunjike watoke kwanza Bungeni. Hoja hii haina mshiko kwa sababu wabunge ni wawakilishi wa wananchi na kama wametumwa kufikisha hizo salamu sidhani kama wakiondoka Bungeni ndio Bunge litafikiria kuuvunja muungano.

Labda nishereheshe tu kwa kusema vyama vya Upinzani pamoja na wabunge wote sii lazima wakubaliane na kila kitu ktk katiba iliyopo na hakuna wakati mzuri wa kuwakilisha pingamizi zao zaidi ya bungeni ambako naweza kusema hata hao wabunge wanaopinga katiba iliyopo au Posho basi wajiondoe Bungeni au Chadema inayotaka Wabunge wasiwe mawaziri wajiondoe Bungeni au wale wanaodai serikali tatu waondoke bungeni. Tukifanya hivyo sidhani kama tutaweza kufanikisha lolote isipokuwa cha msingi ni kwamba Wazanzibar wanashindwa kuuza hoja hii kwa wananchi badala yake wanaitumia hoja ya Muungano kujenga uhasama baina ya bara na visiwani.

Na kisiasa haya ni makosa makubwa sana kama alivyofanya Malecela wakati wa mwalimu kwani kosa halikuwa hoja ya kuwepo na serikali tatu bali ni kulazimisha mgawanyiko pasipo kuuza hoja kwa wananchi na ukapata support yao kama mtumwa kinyume cha hapo inakuwa kama ni mpango wa Mapinduzi baridi..

Waache Wabunge wa Zanzibar waendelee kudai kuvunja Muungano lakini waje na hoja za msingi na sii kujenga uhasama ambao hauwezi kuwasaidia kwani ni wao waliobadilisha katiba tena kwa majivuno wakijipangia nyadhifa zinazowastahili. Wameshindwa vipi kudai referundum kwanza ili wapate kuona wanaungwa mkono kiasi gani? hiki ndio kipimo kizuri ambacho hakika ubishi.

Muafaka wa CUF na CCM ulikuwa game changer kwao, na tuliosema hapa JF wakatuona wana Chadema tunalia CUF kutuacha solemba. Leo wamerudi ktk hoja ile ile ya kutaka serikali tatu au laa Muungano uvunjike hali wamekwisha kula yamini ya udugu na CCM ktk Utawala wa Zanzibar. Hata mwaka haujapita, wanafiki wa Muungano wameanza kulialia tena maana wengine walitegemea kupata nafasi za uongozi ktk shre power hiyo hawakupata.

Kwa mantiki ya hoja yako ni kweli hao wabunge mawaziri kama kweli wanataka kuvunja Muungano wajitoe bungeni na kuachia ngazi za uwaziri maanake ktk majukwaa ya Kitaifa utawasikia wakisema wanaopinga Muungano ni wasaliti hali wakiwa na wananchi mitaani hubeza Mapinduzi yenyewe. Na kama umegundua kitu kimoja wale waliopigwa chini ktk chaguzi mbali mbali za madaraka iwe kamati za bunge au serikali kuu ndio wanapiga makelele zaidi, lakini ndio hao hao walishangilia muafaka hadi jino la mwisho. Sijui Karume na Seif waliwaahidi kipi na hakika katika sifa za Makamba hili linatangulia kwani ni ushindi mkubwa kwa CCM.
 
Mzee Mwanakijiji,
Kama sijakusoma vizuri naomba unisahihishe lakini nadhani unakosea unaposema wanaotaka muungano uvunjike watoke kwanza Bungeni. Hoja hii haina mshiko kwa sababu wabunge ni wawakilishi wa wananchi na kama wametumwa kufikisha hizo salamu sidhani kama wakiondoka Bungeni ndio Bunge litafikiria kuuvunja muungano. .

Mzee, wananchi hawawezi kumtuma Mbunge kwenda kuvunja sheria naye katika akili timamu akakubali kwenda kuvunja sheria kwa kisingizio kuwa "wapiga kura wangu wamenituma". Hivi hao wananchi wakimtuma Mbunge aende Bungeni kuhalalisha kusema wanaobaka wasiadhibiwe kwani wananchi wake ndio wanataka hivyo tunaweza kumkubalia kwa sababu "wananchi wake wamemtuma hivyo"? Hawa wabunge ndio wawakilishi wa wananchi lakini siyo kasuku wa wananchi. Wanatakiwa kusema wazi kuwa "hilo siwezi kulisimamia kwa sababu ni kinyume na sheria". Mbunge anayekubali kutumwa kuvunja Katiba au sheria na wananchi wake anatakiwa atoke Bungeni kwanza ili aende kufanya huo uvunjaji wa Katiba nje ya bunge.

Narudia tena mzee mwenzangu, Wabunge hawawezi kutumwa na wananchi kwenda kuvunja Katiba; tukikubali inawezekana tutakubali mteremko mmoja wa hatari sana.
 
Kuitetea katiba haimaanishi usiweze kuibadili penye mapungufu.

Wasio itetea katiba ni wale wanaotaka iundwe mpya. Makes more sense.

Muungano unafaida gani kwetu? Faida ya muungano ni moja tu. Crusade.
 
Mkuu nitakujibu tu hoja yako.
kama wananchi hao walikuwa na utamaduni wa kubaka kisha ktk kuingia sheria mpya wamelazimishwa kuacha utamaduni huo - Jibu ni Yes, wanaweza wakilishwa na mbunge wao akasema kwa niaba yao hata kama wewe na mimi tunaona ni uncivilised. Hata kuleta hoja ya kudai Katiba mpya dhidi ya ile waliyo apa kuilinda ni kinyume cha sheria lakini madai yako bungeni na JK kayapokea..Marekani wapo wabunge wanaotaka bangi ihalalishwe wakati imeharamishwa kisheria.

Tatizo linakuja pale unaposhindwa kuwakilisha hoja kimsingi isipokuwa kudai kuvunja Muungano baada ya kufikia muafaka. Kwa maana kwamba kero za Muungano zilipatiwa dawa ya kuunda muafaka baina ya CUF na CCM kiutawala ili Wazanzibar wapate uwakilishi zaidi ktk Muungano na kwa amani Wazanzibar waliipigia kura kinyume cha sheria ama katiba yenyewe na kupitisha muafaka huo kwa kura nyingi (demokrasia). Sasa wanapokuja na madai mengine baada ya kuafikiana ndipo naposhindwa kuelewa Wazanzibar wanataka nini haswa! Kama Muungano hauna faida walipopiga kura hawakuyajua haya?
 
Muhimu Katiba itetewe.

Kuna zoezi la kuandika katiba mpya; wanaweza kupeleka huko. for now, the status quo applies.

I would not call it crusade; hizo ndio stereotype

Kuitetea katiba haimaanishi usiweze kuibadili penye mapungufu.

Wasio itetea katiba ni wale wanaotaka iundwe mpya. Makes more sense.

Muungano unafaida gani kwetu? Faida ya muungano ni moja tu. Crusade.
 
Mkuu nitakujibu tu hoja yako.
kama wananchi hao walikuwa na utamaduni wa kubaka kisha ktk kuingia sheria mpya wamelazimishwa kuacha utamaduni huo - Jibu ni Yes, wanaweza wakilishwa na mbunge wao akasema kwa niaba yao hata kama wewe na mimi tunaona ni uncivilised. Hata kuleta hoja ya kudai Katiba mpya dhidi ya ile waliyo apa kuilinda ni kinyume cha sheria lakini madai yako bungeni na JK kayapokea..Marekani wapo wabunge wanaotaka bangi ihalalishwe wakati imeharamishwa kisheria.

Wabunge hao wanakosoa sheria iliyopo lakini hawasemi "njooni tuvute Bangi" wakati wanajua sheria inakataza na wakivuta au wakikutwa nazo haijalishi kama wanaona ni halali watatiwa pingu tu. Mbunge hawezi kusimama Bungeni (hapa Marekani kwa mfano) na kuwataka watu wavunje sheria.
 
ndio maana nikasema labda sikukusoma vizuri.

Kwani hao wabunge wa Zanzibar wanasema njooni tuvunje muungano? na kwa matendo gani waloyafanya ambayo yanavunja Muungano maana wako bungeni ambako wewe unawataka watoke kama vile wanavuta bangi kinyume cha sheria zilizopo. Utaratibu wa bunge ni kuleta hoja na na kama kawaida yangu nasema wenye kiburi cha kusema hivyo wamekuwa na uthubutu wa hata kuhoji Mapinduzi na hati za muungano.

Ila sijasikia Mbunge yeyote akiwataka wananchi wauvunje Muungano bali kulitaka bunge lipitishe maamuzi ya kuuvunja. sasa kama kuna mtu kasema hivyo ndio nawaita wanafiki na ndio nikasema (soma paragraph ya mwisho) una point unapowataka wabunge mawaziri (CCM -Z) wajiuzuru nafasi zao kwanza kwa maana watakuwa wanavunja Muafaka kisha hapo ndipo tutajua kweli wanasimamia maagizo ya wananchi wao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom