Wanaotaka Muungano Uvunjike watoke kwanza Bungeni na BLW | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaotaka Muungano Uvunjike watoke kwanza Bungeni na BLW

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 12, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna Wawakilishi na Wabunge ambao wamekuwa wakitoa lugha ya kuonesha kuchoshwa na Muungano na bila ya shaka wanazo sababu ambazo wanaamini zinawapa haki ya kutoa hisia hizo. Lakini wapo wengine kati ya hao ambao wanatoa matamshi yenye kuashiria kupigania kuvunjwa kwa Muungano. Wapo wawakilishi wa vyama vyote ambao wamekuwa na kauli hizo za kutishia kuvunja Muungano hasa katika Bunge lililopita na hili la sasa. Ndugu zangu, hawa wawakilishi hawawezi kutoa kauli za kutaka kuvunja Muungano na wakabakia wawakilishi halali wa wananchi kwani kwa kutoa kauli za kuvunja Muungano wanavunja Katiba iliyowaweka hapo.

  1. Wawakilishi wote hawa walisimamishwa kugombea nafasi zao au kupata nafasi zao kwa kudhaminiwa na vyama vya siasa ambavyo viliandikishwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria ya Vyama Vingi. Katiba na Sheria zinakataza kabisa kuandikishwa chama chochote ambacho kinapigania kuvunja Muungano. Hivyo, wote walisimamishwa na vyama visivyopigania kuvunjwa kwa Muungano.

  2. Kutokana na hilo la kwanza, hakuna Mbunge au Mwakilishi ambaye wakati anagombea aliwaahidi wananchi kuwa ataenda kupigania kuvunja Muungano kwa sababu au kisingizio chochote kile. Wasingeweza kufanya hivyo wakati wa kampeni kwa sababu Katiba inawakataza na Sheria ya Uchaguzi ingewabana na kuwaengua mara moja. Kama hakuna chama kilichoandikishwa kwa ajili ya kuvunja Muungano hawa wawakilishi wanapata wapi mandate ya kutoa hoja za kuvunja Muungano?

  3. Waliposhinda uchaguzi au kupewa ushindi wa chee waliingia Bungeni/BLW na kabla ya kuanza majukumu yao walishika misahafu na kuapa. Waliapa kwanza kabisa "kulinda, kutetea na kuihifadhi Katiba Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Ninataka kuamini kuwa walimaanisha viapo vyao. Kama walimaanisha walijifunga kuulinda Muungano siyo kuuvunja. Hivyo, kauli zozote za kutishia kuvunja Muungano au hata kuashiria kuwa "muungano uvunjike" ni kinyume na kiapo chao na hivyo ni kosa tosha kabisa la kumfanya Msajili aidha kukifuta chama cha siasa au kumtangaza huyo Mbunge/Mwakilishi kuwa amepoteza sifa za kuwa mwakilishi. Huwezi kuapa kulinda Katiba halafu ukasimama kutangaza kutaka kuivunja!

  4. Kama 1,2 na 3 ni kweli basi Wabunge na Wawakilishi walioko kwenye nafasi zao sasa hawana haki, uwezo, madaraka wala mamlaka ya kuzungumzia kuvunja Muungano. Yote wanayoweza kufanya ni kuutetea na kuuenzi na kuulinda.

  5. Kwa vile Katiba imeweka toka mwanzo kabisa (Ibara ya 1,2) kuwa Tanzania ni nchi moja na eneo lake ni eneo lolote la Tanzania Bara na Tanzania Visiwani na kuwa katika nchi hii moja kuna vyombo viwili vya utendaji yaani Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kauli zozote za kubadilisha serikali hizi mbili aidha kwenda serikali moja au serikali tatu nayo ni kinyume na Katiba! Wabunge hawawezi na hawapaswi kuzungumzia kubadilisha Muungano kwani Katiba Inawakataza isipokuwa kama wametekeleza utaratibu wa Katiba wa kubadili Muungano. Wameapa kulinda Nchi Moja, Serikali Mbili! Ndio maana wengine tulipuuzia na kubeza kauli ya Rais Kikwete kuwa Zanzibar ni "nchi ndani ya nchi" kwani haina mantiki na ni kinyume cha Katiba!

  6. Kama 1, 2, 3, 4 na 5 ni kweli basi wabunge na wawakilishi wetu wanaachiwa uchaguzi mmoja tu nao ni kutatua kero za Muungano, kuondoa matatizo yaliyopo na kuboresha ili kuufanya Muungano uzidi kuimarika. Hawapaswi kuudhoofisha wala kutoa kauli za kuwachochea watu kuchukua msimamo wa kuuvunja. Siyo wabunge tu wale wote walioapa kulinda Katiba na hivyo kulinda Muungano wanalazimishwa na Katiba hiyo kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote.

  Hii ina maana gani?
  Kwamba, kama kuna Mbunge au Mwakilishi ambaye anaona kuwa Muungano haufai na hataki uwepo anaachiwa uamuzi wa kutakiwa kutoka Bungeni (ili asibanwe na kiapo) na kwenda kuanzisha harakati za kuvunja Muungano. Na kama kundi hili linaweza kupata wafuasi basi ni jukumu lao kutumia nguvu zao zote (na hapa neno ZOTE nalimaanisha) kupigania kuvunja Muungano na kwa kufanya hivyo wajue wameamkua kupambana na vyombo vilivyopo vyenye kulinda Muungano. Kama hoja yao inaweza kuwa na nguvu sana na kupata wafuasi wanaweza kujikuta hatimaye wanalazimisha Muungano kuvunjika aidha kwa njia ya amani au kwa vurugu. Kwa vile Muungano wetu haukuwa wa ku-annex Zanzibar ni wazi unaweza kuvunjwa kwa njia ya amani kabisa. Muungano wetu siyo kama ilivyokuwa Ethiopia na Eritrea au Sudan na Sudan Kusini au Russia na Georgia au Ukraine au zilizokuwa Jamhuri za Yugoslavia. Tanganyika haikuivamia Zanzibar na kuichukua kwa nguvu. Ulikuwa ni Muungano wa Hiari ambayo kusema ukweli ni vigumu sana kuuvunja licha ya majaribio ya baadhi ya watu kujaribu kuwafanya Watanganyika wajisikie kama waliivamia Zanzibar. Ni vigumu kuvunja Muungano wa hiari.

  Hivyo, wale walioapa kulinda Katiba na Muungano na sasa wanataka kuvunja Muungano huo hawalindwi na kinga za Bunge wala Uhuru wa Mawazo kwani mwanafamilia hawezi kuja na dumu la mafuta ya petroli na kiberiti mkononi na kuanza kudai kuwa pale Nyumbani watu hawampendi na hawamjali na hivyo ameamua kuichoma nyumba moto na watu wasema ati "ni uhuru wa maoni". Pale Bungeni Mbunge hawezi kusimama na kupiga kelele "moto moto" halafu watu wakikurupuka kukimbia asema "analindwa na haki na kinga za Bunge kusema lolote Bungeni".

  Waondoke kwanza Bungeni na BLW ili waanzishe hoja za kuvunja Muungano; hawawezii kufanya hivyo wakiwa bado wamefungwa na viapo vya kuulinda Muungano huo.
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mwanakijiji hapo umepotoka kwasababu mwakilishi anaposimama ndani ya bunge na kutaka kuvunja muungano haina maana ya yeye kutokuwepo ndani ya bunge bali ni yeye kuwasilisha mawazo wanajamii fulani ya kuwa wamechoka muungano. sasa kama ni mwakilishi wa watu au jamii fulani basi anatakiwa kuleta hoja bungeni ili wawalishi wa wananchi wa makundi mengine wajadili hija hii na watoe mawazo na ikibidi kuwe na upigaji kura katika bunge. na si hivyo tu bali wanaodai muungano uvunjike ingawa wanaweza kuwa wachache lakini hati wa muungano ilionyesha kuwa baada ya miaka 12 toka siku ya muungano kutakuwa na upigaji kura kuchagua kama wananchi wa pande hizi wanapenda kuendelea na muungano au lah,

  cha msingi ni kuanza kujiuliza nini tatizo la watu wanaodai muungano uvunjike , kwani bila shaka watakuwa na kitu au imani wanayoifuata , la sivyo inawezekana ni uroho au ukichaa. lakini tusifike wakati tukakataa kusikiliza mawazo ya watu fulani kwa kuwahukumu kuwa wao wamekosea kabla ya kujua misingi yao.

  Wengi wa watanzania tunapend muungano lakini wachache wanaonekana kuchoka muungano, basi ni wakati wa kuwasikiliza wachache na kutatua matatizo yao , kama tatizo ni vyeo basi tuwasaidie kuwashauri ni njia gani ya kuvipata pasipo kuvunja muungano na kama tatizo ni akili zao basi tuwatafutie dawa ya kuwatibu.

  Mwanakijiji punguza jazba juu ya maoni ya wawakilishi wanaotaka muungano uvunjike, tumia muda mwingi kuwaelimisha mafanikio na mazuri ya muungano na jinsi gani ya kutatua kasoro zao, isije ikafika wakati kuwatenga na kuzuia sauti zao kusikika kwani tusije kufika wakati mawe yakawasaidia kusema na wasijue cha kufanya na nchi ikatikisika
   
 3. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna wakutoka hapo hawa ni njaa tupu, Mh Sita kamwaga kila kitu na kuwaeleza hizo kelo ambazo hazina msingi badala yake Jusa badalka ya kumjibu Sita bungeni eti kaenda kuitisha mkutano Unguja anamjibu Sita. Huu si uanajike huu mwanaume ankuambieni kama hamtaki tuvunje, sasa si ndo kila siku mnatka sasa mnataka nini? Tulikuwa hatui na kuwa kumbe ni serikali ya mapinduzi ililemewa swala la elimu ya juu, ikamba serikali ya muungano ilichukue. Sasa wanataka nini hawa?

  Hata hao wawakilishi uelewa wa Zanzibar ni mdogo saana, ndo maana mtu anayedhani Zanzibar kuwa Singapore huyo anaota simulizi za kungwi, kwa kichwa kipi kutoka Zanzibar?
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Mwanakijiji, labda wabunge/wawakilishi hao wameona ni bora kupigana wakiwa ndani ya uwanja wa mpira kuliko kuangalia Luninga.

  Pili, kama mwakilishi ametumwa na wapiga kura wake atoe hoja hizo, je afanyaje? akae kimya? Na kwa uelewa wangu ni kwamba wananchi wengi na wawakilishi wao hawakatai Muungano, wanachotaka kirekebeshwe ni 'muundo/aina' ya Muungano. Sasa ni mahala gani muafaka kutoa hoja kama hizo kama sio Bungeni?

  In my view, status-quo is not an option hasa baada ya serikali ya umoja wa kitaifa maana kwa sasa hakuna 'distraction'.
   
 5. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji upo sawa. Maana ya kiapo cha kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano maana yake ni kuyalinda, kuyatetea na kuyahifadhi yote yaliyomo ndani ya katiba hiyo. Muungano umo ndani ya katiba. Mbunge ama Mwakilishi ukitoa matamshi ya kuulani Muungano maana yake unailaani katiba uliyoapa kuilinda, ni kosa kubwa kukiuka kiapo cha utiifu.

  Ukiwa ndani ya bunge ama BLW unapoteza kikatiba haki ya kutaka kuvunja kitu kilichomo ndani ya katiba uliyoapa kuilinda. Hata Kikwete alivunja katiba kusema Zenji ni nchi ndani ya nchi. Msimamo wa Pinda ulikuwa sawia tukirejea hata kwenye hukumu ya rufaa kwenye kesi ya SMZ V Seif na wenzake. Mahakama ililitafsiri hilo kwa kirefu na ufafanuzi kisheria.
   
 6. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Nafikiri hapa kuna utata, ni katika mazingira gani wabunge wanaweza kujadili mabadiliko yoyote ya kikatiba (likiwano hili la muungano) bila kukiuka kiapo cha kuilinda katiba yenyewe?!
   
 7. G

  Godwine JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  usichanganye vitu mjumbe mbona ata vifungu vya katiba vinaweza kubadilisha na bunge na hoja inajadiliwa bungeni iweje kuhoji muungano ndio sheria izuie. mbunge ana kinga ya kuzungumza huru mawazo ya watu wake japo si lazima yaendane na wengi
   
 8. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu heshima mbele,
  Kwa maoni yangu si sahihi kuwaambia wanaopigania kuvunjika kwa muungano wafanye hivyo wakiwa nje. Mi nadhani hayo ni maoni yao na wanapaswa kusikilizwa, na mojawapo ya sehemu ambayo kuna nafasi nzuri ya kutoa maoni na ukasikika ni kupitia bunge ama BLW hivyo tusiwabeze.
  Ni sawa tu na mtu ambaye ameomba kazi kwa unyenyekevu na akakubaliana na vipengele vyote vya mkataba, baadaye atakapoanza kudai maslahi ambayo awali alikubaliana nayo, je itakuwa ni sahihi kumwambia kuwa una haki kwa sababu mwanzo ulikubali hivyo jiuzuru kwanza ili ukadai maslahi mazuri ukiwa njeya ajira?

  Kiujumla Muungano una makosa/matatizo/kero/mapungufu mengi mno. Nadhani si busara kuyafichaficha na kuyafunika mambo haya na badala yake tujikite katika kutafuta suluhu za matatizo haya. Na hii ni kwa pande zote.
   
 9. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,074
  Likes Received: 7,562
  Trophy Points: 280
  The hard way is the only way.......serikali yetu haina tabia ya kuwasikiliza wananchi wake, hivyo njia pekee ya kupambana na kulazimishwa kusikilizwa ni kwa wananchi kujipenyeza katika mihimili ya dola na kuendesha vita wakiwa humo ndani....the better way to win this war is to fight from inside
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wanaweza kujadiliana kero za Muungano na wanaweza hata wakipenda kuzungumzia jinsi ya Kubadilisha Katiba; lakini hawawezi kuzungumzia "kuvunja Muungano". Hakuna mtu aliyetumwa kwenda kupelekea hoja ya kuvunja Muungano maana kama yupo alipoteza hilo pale aliposhika Katiba na kuapa kulinda. Na naweza kusema ni makosa makubwa kwa Maspika wetu kuwapa wawakilishi hao jukwaa la kuzungumzia kuvunja Muungano. Wanatakiwa kuwauliza kwanza:

  a. Uliapa kuilinda Katiba Mheshimiwa fulani?
  b. Ulimaanisha kiapo chako au uliapa tu ili uingie Bungeni?
  c. Kama ulimaanisha iweje uzungumzie kuvunja Muungano?
  d. Chama chako kina sera ya kuvunja Muungano?
  e. Ulipofanya kampeni uliwaahidi wananchi kuwa utapigania kuvunja Muungano?

  Haya ni maswali rahisi; wale wanaotaka kuvunja Muungano hawawezi kuwa wale wale walioapa kuulinda! Hili mbona si gumu sana kulielewa. Ni sawasawa na mtu asimame na kusema "mimi siupendi kabisa ukatoliki na laiti ungefutiliwa mbali" halafu mtu huyo huyo ameshika rozali na kumpanga mstari kwenda kupokea Komunyo baada ya kusali sala ya "Nasadiki kwa Kanisa Katoliki". Au mtu mwingine ajitokeza na kuseme "Siamini kabisa katika Uislamu na misikiti yote ivunjwe" halafu huyo huyo akasimama na kusema shahda na akawa wa kwanza kutoa fedha za kujenga na kusaidia misikiti. Haiwezekani.

  Aidha unamaanisha unachosema au humaanishi. Kama unamaanisha huwezi kumaanisha halafu ukafanya jitihada ya kwenda kinyume cha kule kumaanisha kwako. Wanataka kuvunja Muungano watoke kwanza Bungeni na kwenye BLW ili wafanye yale ambayo wanaamini ni sawa.
   
 11. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  I do not give a damn na hawa wavivu wa kupindukia.
  Wanaweza kusepa na sisi tukajiendea kivyetu
  Kwamba wanatabia za kulelewa na kupewa vya bure kama mabibi ni dhahiri.
  Kama wana ungangari wowote waondoke tu katika muungano wakati huu dunia inapowaona bungeni Dodoma.
  They have no balls
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa Baraza la Wawakilishi ni wanafiki tu. Wanasema hivyo ili wapate mgawo mkubwa zaidi wa keki ili wapoe. Wakiwekwa kiti moto sawa sawa kuwa au wanyamaze au waondoke bungeni na kwenda kugombea kwa ujumbe wa kuvunja Muungano, utaona watakavyonywea.

  Huyu Dr Hamad tulimuona na vijembe vyake. Alipokwama kila upande ndiyo akaja na porojo za nia njema kujiunga na Chadema.

  Nakubaliana na Tundu Lissu kuwa mafuta tuwaachie Wazenji wachimbe maana jamaa ni wavivu kufanya kazi na masikini wa Mungu sana na hasa wale ambao hawakusoma na hawana ka damu ka Uarabu (Wanaitwa Wanyamwezi, P*mbavu sana, kwani Mnyamwezi ni mtumwa? Mie ni Mtumwa?). Hawa ndugu zangu Wanyamwezi watabaki kuwa na hali mbaya sana labda Zanzibar kweli wawe na mafuta ili kipato kiwe kikubwa kwa wote.

  Utaona wakisikia mkwara wa Serikali tatu watakavyoanza kuchanganyikiwa maana ulaji utakwisha.

  Yetu macho.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Mwanakijiji, watoa hoja wengi bungeni (kama si wote) wanataka 'ku-renovate'. Na wanataka kufanya hivyo ili kujinusuri na kile wanachoona hatari ya kuangukiwa na ukuta maana nyufa zimekuwa kubwa! Na nionavyo mimi bora liongelewe bungeni huku mtaani is 'worse'.
   
 14. P

  Paul S.S Verified User

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu sijakupata vizuri hapa unamaanisha nini?
  Hivi kwa mfano mbunge akidai raisi apunguziwe madaraka aliyonayo kikatiba anakuwa anavunja katiba aliyoapa atailinda?
  Je mbunge kudai jambo lolote lililopo kwenye katiba ni kuisaliti katiba hiyo? kwamba mbunge hana haki kuwa against na katiba aliyoapia hata kama
  inamapungufu kiasi gani?,
  Sidhani kama katiba ni msaafu usio hitaji kuhojiwwa na wabunge pale unapokuwa ni kwa maslahi ya wananchi
   
 15. G

  Godwine JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  a. katiba sio kitu kisichobadilika ndio maana kukitokea na mabadiliko bado yatamuhusu katiba ni dynamic na si mgando kwa hiyo ata tukisema katiba tuweke mambo mengine bado muwakilishi huyu atahusika na mabadiliko haya sio kwamba mbunge akiapa na katiba ya mwaka fulani ikibadilika basi haimuhusu.

  b.watu kuapa hakuna maana ya kuwa ni kutii bila kuhoji mambo yaliyo ndani ya katiba kwa mfano kama katiba ingeweka kifungu kibovu kinachoruhusu wizi wa rasilimali zetu basi mbunge hasihoji kwasababu ameapa kuitumikia

  c.hati ya muungano yenyewe imeweka wazi namna ya kuvunja muungano kwani walisema baada ya muda fulani wapige kura ya maoni kuona kama muungano unahitajika kuendelea au lah. kama tuendelee ni kwa mfumo gani, basi tusije dhani waliounganisha mungano hawakudhani unaweza kuja kuwa na matatizo bali walipenda matatizo yaje yatatuliwe kwa amani na si kutisha na kufunga hisia za watu,

  d. mbunge si muwakilishi wa chama bali ni muwakilishi wa wananchi kwahiyo awezi kusukumwa na sera za chama pekee bali ni mahitaji ya wananchi anaowawakilisha

  e. wengi tunachanganya tunadhani mbunge anatakiwa kutoa ahadi nyingi kuwa atafanya nini, bali mbunge anatakiwa kutuambia ya kuwa atakuwa tayari kutuwakilishia mawazo yetu na si mawazo yake. na ni kosa mbunge kusema atafanya kitu gani kwani mbunge si mtendaji bali ni mwakilishi wa jamii husika, mbunge hatakiwai kujenga visima bali anatakiwa kulisemea tatizo hili mpaka watendaji wakalitatua,


  kwahiyo mwakilishi anaposimama bungeni na kueleza mambo yasichukuliwe ni mawazo yake au yeye kavunja kiapo bali ni mawazo ya wananchi anaowawakilisha na kusiwe na hukumu juu yake kwa mawazo ya wanajamii anaowawakilisha
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ninavyowasoma ndio ninaona tuna tatizo kubwa; mtu ameapa kufanya kitu hafanyi kwa sababu zake halafu tunashindwa kumbana kwa sababu tunafikiria kuwa ana uhuru wa kutokufanya. Viapo (oaths) ni vitu vizito sana. Tukikubali wabunge waape kulinda Katiba halafu tukasema wasisimamie kiapo chao kwanini tuamini watu wanaoitwa mahakamani na kulishwa kiapo watarajiwe kusema kweli kama hawamaanishi kiapo chao?

  Rais amekula kiapo cha kazi ya Urais na ndani ya kiapo hicho cha kwanza ni kulinda Katiba. Sasa Rais huyo huyo akianza kuvunja Katiba kwa kisingizio cha "maoni tofauti" ataweza vipi kuendelea kuwa Rais? Kama tunamkubalia avunje kiapo chake kwenye jambo moja kwanini tusimkubalie kwenye mambo mengine? Wabunge wamekula kiapo kulinda Katiba, sasa wasipoilinda tusiwaulize? Maana kama viapo havina maana ni bora kutokuvishika, sivyo?

  Au tuwape uchaguzi wanapokula viapo - wachague ni mambo gani wataapa kuyalinda ili tusipate shida ya kuwaliza. Kwa mfano, wabunge wanapoapa wasema "Naapa isipokuwa kwenye kulinda Muungano"...
   
 17. G

  Godwine JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  @mwanakijiji
  usichanganye kulinda hakuna maana kutohoji kitu chochote bali ni kutekeleza mpaka pale mambo yanpobadilika na si kuwa usiwe sehemu ya mabadiliko hayo. kutii ni kuiheshimu mpaka pale kutapokuwa na badiliko na unabadili misingi toka kuheshimu ya zamani mpaka mpya. bila ya kuhoji basi hakuna haja ya kuwa na wawakilishi wa kutunga sheria na kuchomoa baadhi ya vifungu vilivyo ndani ya katiba
   
 18. P

  Paul S.S Verified User

  #18
  Jul 13, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu is this came from you au kuna mtu kaiba password yako?
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ahaa haa umenikumbusha mchezo wetu wa kitoto.

  Tema, ni teme chakula?
  Meza, nimeze moto?

  Sasa utafanyaje? nitamung'unya tu!

  Sasa, Mwanakijiji wakiwa nje ya bunge watapata wapi nguvu ya kusikilizwa na kutekeleza matarajio yao? na je wanaapa kulinda katiba au kulinda Muungano? kama wanaapishwa hivyo basi kuupinga ni uhani, na hivyo walipashwa kuomba kubadilishwa aina ya kiapo. Kama wakina Marando walipoingia Bunge la mwanzo walifanikiwa kubadili kiapo cha wabunge kwa kukataa kuapa kumtii rais wa Jamhuri ya Muungano mpaka kiapo kilibadilishwa na kutoa hilo neno.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nadhani labda imekuwa vigumu kueleweka. Hakuna tatizo kujadili hoja na kero za Muungano; hakuna tatizo kwa wabunge kutaka kubadilisha mambo fulani fulani na hata kutunga sheria za kuboresha mambo fulani. Kama kuna tatizo wana uwezo wa kufanya mabadiliko ya Katiba kama yanahitajika. Hayo yote hayana tatizo kwani ni ndani ya wajibu wao kama unavyoashiria. Kitu ambacho hawawezi ni kusimama na kusema "tuvunje Muungano". Hili haliwezekani. Kwa sababu, waliapa kuulinda na kuuboresha na Katiba inawapa jukumu la kufanya majadiliano yoyote kwa msingi wa "umoja wa Taifa" na Taifa na nchi ni moja yaani Tanzania.

  Mbunge au Mwakilishi hawezi na hapaswi kusimama na kusema "mambo ni magumu tuvunje Muungano" hawezi kwa sababu hapo hatoi ushauri, hajaribi kupendekeza sheria wala nini anasimamia na kupigania kuvunja Muungano.
   
Loading...