Wanaotaka maridhiano ya kitaifa tukutane hapa

Wanaotaka maridhiano ya kitaifa tukutane hapa

ong'wafaza

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
262
Reaction score
115
Kwa muda sasa kumekuwa na maoni mbalimbali kuhusukufanyika kwa maridhiano ya kitaifa kufutia matukio ya baada. ya uchaguzi mkuu wa mwaka Jana.Kuna wanaotaka maridiano ili kuliponya taifa kufuatia maumivu yaliyolikumba taifa kabla na baada ya uchaguzi,na engine wakiona maridhiano hayo ni kupiteza muda wa kufanya mambo engine ambayo kwao ni muhimu zaidi.
Binafsi naona kabla ya kulijadili hili,tujiulize maswali yafutayo:-
1.Maridhiano ni nini?
Tafsiri nyingi zimetolewa kwa lengo la kujibu swali hili.
Kwa muktadha wa mada hii,itoshe kusema kwamba maridhiano ni majadiliano yanayolenga kupatanisha jamii iliyohitilafiana na kugawanyika pande mbili juu ya Jambo/mambo Fulani linalowahusu wote.
Sasa hapa ndipo mjadala katika mada hii unapoanzia.
Kumbe kuna JAMII ILIYOHITILAFIANA NA KUGAWANYIKA PANDE MBILI na pia kuna JAMBO/MAMBO .
Hapa sasa yanazaliwa maswali mawili:
Kwanza jamii imehitilafiana na kugawanyika pande mobili:ni zipi hizo?
Kwa maoni yangu,jamii iliyohitilafiana Kwa mkutadha wa mada hii ni Wananchi Kwa mana ya Watanzania (Watawala na Watawaliwa) Kwa pamoja.
Pande mbili zilizohitilafiana,Kwa maoni yangu ni Watawala kama kundi moja,na Watawaliwa kama kundi jingine.
Kwa mantiki hii,ninaweza kusema bila kumumunya maneno kwamba,Watanzania wamegawanyika katika makundi makubwa mawili ya WATAWALA kwa upande mmoja na WATAWALIWA kwa upande mainline.
Swali linalobaki kujibiwa ni Je, haya makundi yamehitilafiana kwa JAMBO/MAMBO gani?
Mengi yamesemwa kuhusu hili.Binafsi naona Jambo Hilo ni mfumo wa namna ya kujitawala.
Hii inajumuisha mambo mengi ikiwemo mifumo ya kupatikana viongozi na ukiukwaji wa sheria na taratibu za kiutawala tulizojiwekea.
Itakumbukwa kwamba kuna mate do mengi yanayodhihirisha ukweli huo ambayo hata tume ya Raisi aliyoiunda kuchunguza matukio ya tarehe 29 october na siku kadhaa baadaye chini ya Jaji Chande ilibainisha hivyo.
Pengine Mtu anaweza kudhani. kwamba kuhitilafiana kwenye mambo haya kumesababishwa na Watawala pekee,la hasha.
Kuna baadhi pia ya Watawaliwa hawakutimiza wajibu wao ipadavyo.
Kwa mktadha wa mada hii,sitaingia Kwa undani zaidi kufafanua hitilafu za kila upande.
Itoshe kusema kwamba JAMBO/MAMBO yanayosababisha jamii yeti (Watanzania) kuhitilafiana na kugawanyika linatokana na mfumo mbaya wa Utawala.
2.Nini kifanyike?
Baada ya kuifahamu dhana nzima ya maridhiano,no muhimu sasa kujua ni nini cha kufanya ili kufikia maridhiano ya kweli.
Kwa maoni yangu,njia sahihi ya kufikia maridhiano ya kweli ni kukaa pamoja na kuzungumza.
Pengine hapa linaweza kujitokeza swali:
Inawezekana vipi jamii ya watu. zaidi ya millioni sitini wakakaa pamoja na kuzungumza na hatimaye kufikia muafaka wa kitaifa?
Mwingine anaweza kuuliza kuwa inawezekanaje pande mobility zilizohitilafiana zikakaa meza moja bila mpatanishi?
Pia wengine wanaweza kuhoji kuwa ni Nani atakayeitisha hiyo meza ya mazungumzo?
Maswali ni mengi lakini Kwa maoni yangu,ni mhimu Kwa Watawala kusikiliza na kufanyia KAZI maoni ya walio wengi ili kufanikisha maridhiano ya kweli.
Na hapa nasisitiza busara zaidi itumike ili kufanya mazungumzo haya yafanyike bila kuacha kundi lite nje ya majadiliano.

Majadiliano shirikishi ndiyo yatakayoleta maridhiano ya kweli na hatimaye kuliponya Taiga letu.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.Karibuni Kwa mjadala.
 
Back
Top Bottom