Wanaosali Jumuiya vs wacheza pool table, kuna tofauti?

Wanaosali Jumuiya vs wacheza pool table, kuna tofauti?

BW SALARY SLIP; nimeona unamawazo mazuri. Ila pengine ungeongeza hivi. Endapo katika mtaa ambao waumini wanajumika kwa sala kipindi fulani, basi kama kuna jambo la kijumia la kiserikali au mtaa linaweza kujadiliwa ktk mkusanyiko huo. Ni jukumu la uongozi wa Serikali ya mtaa kutumia mkusanyiko huo, tena bila malipo yeyote ya kikoa kufanikisha na kusambaza maelekezo na maagizo ya Serikali. Hilo hufanyika hata makanisani. Mfano, mnaweza kutaangaziwa ujio wa viongozi, kazi za kujitolea za maendeleo nk nk. MKUSANYIKO WA WANANCHI AU WAUMINI NI FURSA KWA VIINGOZI WETU.WA MTAA. Tuutumia kuwasiliana na wananchi kwa mambo ya maendeleo.
 
Ndugu nakupongeza kwa mawazo yako binafsi, ila napenda kuchangia pia, mawazo yangu;
1. Kwa dini ambazo zinasali weekend, wengi wanasali asubuhi sana, anzia kumi na mbili na saa moja na nusu huwa wamemaliza na wanakwenda kweny shughuli za kuwaingizia vipato. Sasa mlinganisho wa hapo na wacheza pool naona kama hauna uwiano. Pia, dini zote zinavyo vibali rasmi kwa shughuli zote zenye maslahi yao, na shughuli hizi huwa ni rasmi, na haziingilii muda wa kazi.
Pia, kama umewahi kuhudhulia hizi jumuia, kuna mambo mengi tu ya kijamii yanajadiliwa na kuwekwa sawa kuwasaidia wahusika kiimani na kimaisha tu; kwa maneno yako inawezekana ukaenda na kushauri vitu kama ibada za ndoa ambazo hufungwa siku yoyote ya juma kwa dini mbalimbali nazo zisiwepo, chukua tahadhali katika unayofikiria.

2. Wazo la kwamba watu hawahudhulii mikutani ya wanamamlaka; vijiji, vitongoji n.k, linazo pande mbili; kwanza, mikutano hii kwa muda mrefu imekuwa na mrengo wa kichama, wengi wanaitana kwa kufanana itikadi, na kuvaa mavazi yanayooshabikiana na chama fulani. Hapa kuna udhaifu wa viongozi kutambua kwamba mamlaka haipaswi kuwatenga wenye itikadi tofauti, na suluhisho lake ni kama mkuu wa mkoa alivyojiainisha, tunatumaini litabadilika.
Pili; Nguvu ya hawa watu, uelewa wao na uwezo wa kuwaunganisha watu wote bila kujali maslahi ya itikadi husika unatia mashaka, kwa hivo mtu akielewa tofauti, na akihisi atapotezewa muda kwani watu wataanza na salamu (slogan) za kiitikadi inakuwa ngumu kupata heshima wanayostahili. Halafu, hata utendaji wao hauakisi matakwa mapana ya wanajumuia ( tofautisha na jumuia za kidini) au jamii kwa wakati na mahala husika.

Sasa kwa kuhitimisha, ni kwamba ili heshima ya hizi mamlaka zirudi, ni lazima kujitambua kwa mapana ya uwajibikaji, mkuu wa mkoa amehimiza kuorodhesha wanajamii wa mitaa husika kutoka katika kila kaya, hili ni wazo mtambuka kabisa.

Lakini wewe, yapasa ufanye maamuzi binafsi, sidhani kama unalazimishwa kwenda jumuia, na kama huendi, jichunguze utambue ni kwa nini unakereka na mambo yasiyo kuhusu?
 
Mikutano ya mitaa/vijiji hamshiriki ila Jumuiya ndio muhimu zaidi huku kila siku tukilia umasikini.Tutafika?Kwanini hizi Jumuiya zisifanywe kimtaa wala mara moja kwa wiki kuliko kuzunguka nyumba hadi nyumba kila week-end?Tujali muda.
Mkuu
Huo ni utaratibu wa Kanisa.
Kumbuka kuwa Kanisani hauwezi kupata huduma yeyote pasi kupitia kwenye Jumuiya.
Mfano ubatizo,Ndoa etc.
Mkuu hili ni Suala la kiimani na watu wanaenda kusali (Kumuomba Mungu wao) na sio kucheza Kamali ama Pool table.
Kufananisha Kusali Jumuiya na kucheza Pool table ni Dhambi kubwa sana unefanya Mkuu na unahitaji toba kama ni m Kristu.
Pia kumbuka kuwa kuna watawa ambao muda wao karibu wote wanautumia kusali kufunga na kuomba,hawa utasema wanapoteza Muda ?

Salary Slip leo umeongea kipuuzi sana kama yale ma Nyumbu ya Lumumba
 
Mkuu
Huo ni utaratibu wa Kanisa.
Kumbuka kuwa Kanisani hauwezi kupata huduma yeyote pasi kupitia kwenye Jumuiya.
Mfano ubatizo,Ndoa etc.
Mkuu hili ni Suala la kiimani na watu wanaenda kusali (Kumuomba Mungu wao) na sio kucheza Kamali ama Pool table.
Kufananisha Kusali Jumuiya na kucheza Pool table ni Dhambi kubwa sana unefanya Mkuu na unahitaji toba kama ni m Kristu.
Pia kumbuka kuwa kuna watawa ambao muda wao karibu wote wanautumia kusali kufunga na kuomba,hawa utasema wanapoteza Muda ?

Salary Slip leo umeongea kipuuzi sana kama yale ma Nyumbu ya Lumumba
Linapokuja swala la imani watu huwa mbogo lakini kiukweli nyinyi binadamu ni wanafiki wakubwa.Hakuna atakaenda mbinguni kwa kutetea imani yake bali kwa kwa kuheshimu maelekezo ya mwenyezi mungu.

Tunaojifanya kutetea imani zetu ndio wazinzi wakubwa,ndio vinara wa kusaliti ndoa zatu,ndio wezi na mafisadi katika ofisi za umma,ndio wanaotumia imani hizi kuibia waumini wao,ndio wauza madawa ya kulevya n.k.

Huu utaratibu wa kusali kila week-end nyumbani kwa mtu mmoja umepitwa na wakati na ni bora kuwa na utaratibu wa kutenga eneo moja katika mtaa kwa ajili hiyo na iwe mara moja,mbili au tatu kwa mwezi na inatosha kabisa.Tuache kuishi kwa mazoea na kupoteza muda wa kufanya kazi.
 
kweli wewe ni Salary Slip!
wapo wanaoshinda ktk makanisa ya upako na mengineyo kila siku kuanzia jumatatu hadi ijumaa ajabu ni kwamba JUMAPILI yanafungwa!/
 
we acha tu kuwa unaendaa thawa ila siku mkipata msiba au shughuli kama harusi n.k palee kanisa litakapo susia shughuli au ibada kwa marehemu ndo utaelewaa umuhimu wakee...afu nmennusa kitu ww inawezekana hata misibani huendagiii , ungekuwa kule kwa babu yangu kanda ya ziwa tungekutenga kijiji kizima mpaka utoee faini ya ng'ombe mmoja, mbuzi ,bata mzinga na mayai ya mbunii..ntaanzisha thread ya kukutenga hapa jf ili ukomeee
 
Siamini kama mtu na akili zake anaweza leta mada kama hii
 
Huyu mtoa post ana PEPO,, kama sio jini ambalo linamtesa akisikia watu wanalitaja jina la YESU karibu na makazi yke,, au yeye ni mchawi misukule yke inashindwa kumfanyia kazi zke pale jirani zake wanaposali,,

Kwa kifupi wakristo tumeambiwa ,, tuombe bila kukochoka maana hatujui siku wa saa ambayo bwana atakuja,,

Hata hiyo siku moja pia haitoshi ilitakiwa iwe kila sk .
 
Niambienii kuna nini cha maana tunacho-achieve kama jamiii ambacho bila kukaa katija hizo Jumuiya kingeshindikana?

Nijibuni sio kutoka povu.
Hazina maana ni upotezaji wa muda tu
 
Mtoa mada kwa vyovyote yeye siyo mtu wa dini au madhehebu yanayosali jumuiya. Ukiongea hivyo maana yake hata wanaohudhuria ibada mara tano kwa siku wakamatwe
 
...Huu utaratibu wa kusali kila week-end nyumbani kwa mtu mmoja umepitwa na wakati na ni bora kuwa na utaratibu wa kutenga eneo moja katika mtaa kwa ajili hiyo na iwe mara moja,mbili au tatu kwa mwezi na inatosha kabisa.Tuache kuishi kwa mazoea na kupoteza muda wa kufanya kazi.
We jamaa wewe! Tumsifu Yesu Kristo......itikia "Milele, Amina"...kisha tafakari.

Lakini yote kwa yote, heri ya pasaka na Mungu akubariki sana.
 
Mada mzuri mkuu ila tatizo wanaoenda jumuiya ni wavivu na wana IQ ndogo na ndio hawa wanaokushambulia hizo jumuiya zipigwe tu marufuku
IQ ndogo? Kws hiyo ww unajihisi huko timamu?
 
Mikutano ya mitaa/vijiji hamshiriki ila Jumuiya ndio muhimu zaidi huku kila siku tukilia umasikini.Tutafika?Kwanini hizi Jumuiya zisifanywe kimtaa wala mara moja kwa wiki kuliko kuzunguka nyumba hadi nyumba kila week-end?Tujali muda.
Halafu ni mwanachadema wewe. Mmeingiwa na kitu gani nyinyi? Unalinganishaje wanaoenda kuabudu asbh saa12 na wacheza pool? Hopeless kabisa wewe
 
Kijana wa Bavicha una matatizo kwenye ubongo wako .
Ulilalamika azana za misikitini Leo unakalamikia watu kusali jumuiya.
mngepata nchi mngepiga marufuku watu kuabudu ,mngetaka watanzania wote wasiwe na dini kama mwanachama wenu Kingunge.
 
1.Jumuiya zinaimarisha sana umoja miongoni mwa waumini.
2.Jumuiya zinarahisisha sana ustawi wa imani kwa kuwajumuisha waumini wake pamoja na kuwajengea watoto utaratibu wa kusali kwa pamoja.
3.Jumuiya zinaleta ibada karibu na wasio na uwezo wa kufika kanisani kama wazee na vilema.
4.Jumuiya zinaleta mashirikiano ya kijamii kama misiba na sherehe.
5.Jumuiya zinaleta utambuzi wa raia pahala pa serikali

NB:
1.Kila taasisi inapaswa kujiimarisha kwenye misingi kama kanisa ili iwe imara zaidi.
2.Serikali ina taratibu zake na kanisa nalo linataratibu zake.

Mkuu leo umeniangusha kuliko unavyoniangushaga kwa jinsi unavyomshambuliaga Dr.Slaa.
Nahisi mada yako hii inatoa mwanya juu ya chuki yako dhidi ya Padre Dr.Slaa
 
Back
Top Bottom