Wanaorusha Video YouTube, Facebook, Periscope n.k Wawe na Leseni Ati?

Wanaorusha Video YouTube, Facebook, Periscope n.k Wawe na Leseni Ati?



Kuna taarifa zinasambaa kuwa TCRA imetaka kina Millard Ayo na Michuzi na bila ya shaka wengine ambao wanarusha video mbalimbali ambazo zinaonekana kama habari au produced kama habari wawe ne leseni za kutangaza.

Hivi ni genius gani huko ndani amekuja na wazo muflisi kama hili? Na wanaotumiana video wenyew kwa wenyewe au kuonekana "live" siyo kwambba watatakiwa wawe na leseni? au wanaotumia mitandao kurusha "live" training kutoka sehemu moja kwenda nyingine nao watatakiwa wawe na leseni?

Ni wakati gani mawasiliano yatachukuliwa kama yako kwenye "private" realm na siyo "public" realm? Je, watu wote walioko Tanzania wanaoposti vitu mbalimbali (ambavyo vinaweza kuangukia kwenye 'electronic communication') watahitaji kuanzia sasa kuwa na leseni? Hii ikiwemo ni wanamuziki, bloggers n.k?

Wewe Mzee kama siyo Mlozi basi Mchawi.
 
  • Thanks
Reactions: 999
Ccm wanatakutuletea figisu figisu la mtawala kambarage kutunyima TV na uhuru mzima wa habari enzi hizoooo! Na baadae tutaambiwa tumuimbe zidumu Fikra za mwenyekiti jpm..
 
  • Thanks
Reactions: 999
Ingekuwa mihimili 3 inafanya kazi tungepata msaada toka mhimili wa pili na wa tatu. lkn bahati mbaya sana mihimili mingine iko mfukoni mwa pilato. anaamua na kufanya anacho taka.

wabunge baada ya bunge kuwa gizani walirusha video za hoja zao ili wananchi tuzione. sasa hatutawaona tena. Dk Tulia atawapiga mpk makofi.
 
Ukiweka video za mahojiano ya Wema kuhusu mapedeshee yenya hela hawatakugusa, kimbembe uweke video za toto tundu Lisu akiponda gavumenti, hapo lazima rungu likushukie!!!
 
Watu kwa kupinga pinga tu nawapa crown. Hivi huo muda mnaoutumia kupinga si mngeutumia katika kutafuta sababu za kufungiwa? Vipi kama walikua wanatoa huduma bila ya kibali? Msiwe watu wa kupinga kila jambo.
 
Kama kuna taasisi zinaongoza kwa vilaza Tanzania ya kwanza ni TCRA, imejaa wazee wasiojielewa, taasisi ya pili bila shaka tunaijua imekua inapiga headline sana siku hizi kwa kuitaita watu polisi daily bila mpangilio.

Yaani wanataka watu wajiajiri ila wanaamua kuweka barrier ya mtu kutengeneza hadi YouTube videos???????????????
People can't be this stupid, huu ujinga umepitiliza, China wana-filter sana mambo online lakini hata wao hawana muda na watu wanaofungua online video channels, wanachofanya ni kukusanya kodi tu. Sasa tumeanza kuiga filtering ila tunaifanya ka vilaza. Any online business ilitakiwa iwe na very low barrier to entry ili watu wengi wajihusishe, yaani ilitakiwa hata isihitaji registration hadi pale ambapo mtu ameanza kukua na kuingiza pesa, ndivyo nchi ZOTE ambazo zinaongoza kula pesa online zinafanya.

Hivi Tz inategemea itaendelea kwa style ipi? Ambaye anahisi bado tupo kwenye mstari anajidanganya, bila kureplace vilaza wote wa TCRA tutegemee kusubiri makampuni ya nje ndiyo yaje kuoperate nchini maana mtanzania wa kawaida piga ua hana pesa ya kuregister business bongo.

Sasa FB, Instagram, Whatsapp, Uber, zote tunatumia za wamarekani kwa kua TCRA wanabana kila kona badala ya wao kua wa kwanza kutoa support. I'm so disappointed in my country. Japan kila siku walikua na pitch za startups serikali imeondoa barrier zote hata registration walikua hawataki before startup imeanza kugrow, tume ikaundwa kuhakikisha wanasaka startup nchi nzima na kuzikuza, hata foreigners tulikua tunaitwa na tunalipwa kabisa na kulishwa, tunaletewa na mentors ambao wamefungua successful companies, mwisho wa siku zimetokapo kampuni kama tano kubwa sana kwenye hiyo center moja tu ambazo ziko valued at more than $1Billion combined. Hivyo ndivyo serikali inayojua biashara inatakiwa kuoperate sio vilaza hawa ambao kila kitu ni kupiga ban tu, hatuna online companies kabisa bongo ila wanaojaribu kujihusisha ndio hawa wanapigwa ban na kuanza kuwekewa sheria za kijinga, alafu Google wakija tunakua wa kwanza kuwakaribisha waje wabebe hela yote wapeleke nje. Stupid Africans.

Endeleeni kujipendekeza kwa mkuu maana mmejua anapenda kusikia watu wanapigwa ban mnaona mumfurahishe kidogo, ila mnasahau kua yeye sio mjua vyote, hajui how online businesses operate, how startups operate, kama mnataka kumfurahisha badala ya ban mngekua mstari wa mbele kusaidia tukuze kampuni zetu wenyewe, hapo angekuja personally kuwapa pongezi.
 
Mkuu uliwashawishi Watu wengi sana kuiunga mkono CCM ktk Uchaguzi Mkuu uliopita ,sasa haya ndio moja ya matatizo ya mfumo ulioupigania na kutuachia sisi huku Tz tukisomeshwa namba kwa lazima..
Grow up. Kama alishawishi watu kuichagua CCM ndio imnyime uhuru wa kuikosoa serikali? Kuna wapuuzi kama wewe ambao bado mpo kwenye election mode. Mbona nanyi mlimwita Lowassa fisadi tangu 2006 lakini ghafla dakoka za majeruhi kabla ya uchaguzi mkui 2015 mkamteua kuwa mgombea wenu...na hatuwakumbushi.
 
Mbona hii habari haijakamilika...
Wamepigwa marufuku ya nini, na kwa sababu gani?

Kama umefuatilia vizuri, AyoTV amekua akiripoti matukio mengi nafikiri lililotibua zaidi ni hili la jinsi Gwajima na Manji walivyoondolewa kimtindo na Gari jeupe pale central.

Michuzi Kama sio danganya Toto, huenda na yeye picha zake na habari zake zinaleta mijadala Sana mtaani. Ikumbukwe huyu ni mpiga Picha wa serikali na Mara nyingi ikulu.

Sasa Kama sheria ya vyombo vya habari na makosa ya mtandao ipo na inafanya kazi, hili agizo lina mahusia nayo au hiii bi amri mpya?

Hii yote ni kukomesha kuandika andika na kusema sema.
 
Inaonekana kuna shinikizo kutoka kwenye mashirika ya TV nchini. Hii ni baada ya Millard Ayo kuanza kuweka matangazo ya biashara.
Na hizi online tv imekuwa sources za Breaking News na watumiaji wake wamekuwa wengi sana.
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV, AYO TV na Global TV kusitisha huduma zao za TV mtandaoni hadi hapo kanuni za usajili rasmi ambazo mamlaka hiyo imesema inaandaa kwa huduma hizo zitapokuwa tayari.

Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James Kilaba tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa sana nchini na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.

“Kwa mujibu wa section 13 (1) of the electronic and postal communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma zozote za aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano,” imesema barua hiyo.

Wamiliki wa mitandao hiyo Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi na Abdallah Mrisho wameeleza kushtushwa kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati hata kanuni zenyewe hazijawekwa.
“Global TV ipo tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili kama zingekuwepo na kwa sababu bado kukamilika tunaomba kupewa muda zaidi chini ya uangalizi wakati tunasubiria kanuni hizo mpya,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja Mkuu wa Global Publishers.

Ankal Michuzi na Millard Ayo waliunga mkono kauli hiyo na kwa pamoja watatu hao wameomba kuonana na mkurugenzi wa TCRA ili kuwasilisha maombi rasmi ya kuruhisiwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wakati kanuni zikisubiriwa.

Bahati mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa kushughuliwa ataporejea wiki ijayo.

“Ukizingatia kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na haijulikani kanuni zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya kufanya ili wananchi wanaotutegemea sana wasikose huduma hii,” alisema Ankal. Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mchakato wa TV mtandao.

Ayo TV, Michuzi TV na Global TV ambazo zina watazamaji wengi ndani na nje ya nchi, ni TV mtandao pekee zilizoitikia mwito wa TCRA kati ya vituo mtandao takriban 51 vilivyopata barua hiyo.

Nini maoni yako??
Screenshot_2017-02-10-05-28-11.png
 
Back
Top Bottom