Wanaorusha Video YouTube, Facebook, Periscope n.k Wawe na Leseni Ati?

Wanaorusha Video YouTube, Facebook, Periscope n.k Wawe na Leseni Ati?

Kuna mambo yanaumiza moyo sana katika nchi yetu hata ukijaribu kuipenda utaumizwa tu anyway inauma sana kunyimwa habari inauma zaidi kulazimishwa kusikiliza ya wenye mamlaka inauma mno kwakweli haya yanayofanya nchi iendeshwe kipolisi yanaumiza sana kiufupi maamuzi mengine yanayofanywa na mamlaka yanampandisha chati jk mnooo huku mitaani kuliko mnavyofikiria
Jk aliharibu sana mpk watu walimchukia yeye na chama kwa ujumla ila kwa haya maamuzi mengine yanampandisha chati mno mno mno kitu ambacho hastahili mh wetu wa sasa anafanya mambo yanayoonyesha uzalendo kweli ila naamini kwa maamuzi ya serikali yetu yanafanya uma umuone jk ni mzuri Mara dufu kitu ambacho c kweli

Tcra msiirudishe nchi miaka ya 80 mmeiharibu TBC tuliyoiamini sasa mnataka kuharibu hata vyanzo vinavyoaminika sasa haya ni kwa maslahi ya taifa kweli?
Fufueni TBC kwanza iwe yenye kujiamini mkiirudisha TBC ya enzi za tido mhando futeni vituo vyote vya televisheni tutaridhika

[HASHTAG]#Harsh[/HASHTAG] tag #rudishenitbcyatido#
 
sasa hapa si wangetunga tu hizo sheria na taratibu halaf wangewaambia hao jamaa wajisajili kupitiataratibu hizo!!! kwan wao TCRA wana haraka gani?? watu wamejiajiri na hawajavunja sheria yoyote TCRA kama serikali ingewatungia sheria za kuwaongoza ili kusaport kazi za hawa watanzania na c kuwacimamisha kwa mda hata usiojulikana wakati hawajafanya kosa lolote hii nchi cjui ni namna gani eti!! watu waoga wa media hawa haijapata kutokea
 
afu kesho mtu anasimama anatuimbia ooh tunataka vjana wetu wawe wabunifu
 
Wanaacha vitu kwa muda mrefu halafu wanakuja kutoa taarifa wakati ambapo tayari wananchi wamezoea..!
 
Wansataka waipe kazi TBC maana inaelekea KUFA..!?
 
Unafiki mbaya sana na ndio umekuwa adui zetu watanzania.

Adui wa mtanzania ni mtanzania mwenyewe, kuna wakati mtu anajinafkia mpaka yeye mwenyewe personal.

Kipindi kile cha uchaguzi ulikuwa kiherere mandazi sana kwa kutetea upande wa bwana yule. Ila kwa sasa umegeuka na kutaka kurudi upande uliokwisha kunyea kambi.

Wakati mwingine muwe na aibu ata kidogo jamani.

Zungumza kama mtu mwenye akili siyo vipepeo; unafikiri kweli kabisa angeingia mgombea yule Tanzania ndio ingekuwa tofauti; mko tayari kuendelea na ufisadi ili muishi bila kunung'unika? tuliikataa hiyo gharama kuilipa sisi wengine.. haya mengine ni siasa za kawaida tu
 
Kila kitu kitakabidhiwa kwa Jeshi...you know what am saying. Hakuna kuongea ongea wala kuandika andika!
 
operesheni zinduka ndiyo hii .... combustion chamber .... backfired .... blue litmus red .... Isaac Newton third law of motion ..... no success without sangoma
Operesheni Zinduka mbona imefanikiwa sana; kuzuia mafuriko feki usidhani mchezo. Hakuna majuto katika hilo. Na ukiniambia baada ya haya yote yanayotokea sasa na kumchagua mgombea yule nichague nini; bado uamuzi wangu wa kumkataa ungedumu.
 
Hii serikali ina uoga mkubwa sana, sijui kwanini
 
Huyu ndiye Mzee Mwanakijiji !Hata hajui anatetea nini. Si unyamaze upige box maana mtu uliyempigia debe kapita. Hata nusu ya uongozi wake hajafikia unalalamika. Kisa kagusa maslahi yako. Ila akimwadhibu Sumaye, Lowasa au Mbowe anakuwa powa. Tulia unyolewe mzee.

Bahati mbaya hajagusa malsahi yangu; miye napostia vitu vyangu Marekani mambo yenu ya leseni za youtube wala hayanihusu. Ninachofanya ni ukosoaji wa sera tu na mipango (kama ni ya kweli) haihusiani na maslahi binafsi. Ukosoaji huu ningeufanya hata kama nisingemuunga mkono Magufuli.
 
Magufuli akishinda 2020 nitaamini kweli CCM haina mpinzani
 
Bahati mbaya hajagusa malsahi yangu; miye napostia vitu vyangu Marekani mambo yenu ya leseni za youtube wala hayanihusu. Ninachofanya ni ukosoaji wa sera tu na mipango (kama ni ya kweli) haihusiani na maslahi binafsi. Ukosoaji huu ningeufanya hata kama nisingemuunga mkono Magufuli.

Really?, kwamba it is our bussiness kudeal na hii ishu, na kwamba wewe haikuhusu saaana kwa vile uko Marekani?. Hii yote ni kwa sababu unaogopa kusema wazi kwa msisitizo zaidi kuwa katika hili serikali imezingua!

Ungekuwa utawala wa JK ndo umefanya haya, sijui urefu wa makala yako ungekuwaje!

Shame on you brother!
 
Je wasanii kuweka video zao mitandaoni hii imekaaje? Maana kuonyesha video za muziki ni mojawapo ya huduma za TV
 
Back
Top Bottom