Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,739
- 40,864
Kuna taarifa zinasambaa kuwa TCRA imetaka kina Millard Ayo na Michuzi na bila ya shaka wengine ambao wanarusha video mbalimbali ambazo zinaonekana kama habari au produced kama habari wawe ne leseni za kutangaza.
Hivi ni genius gani huko ndani amekuja na wazo muflisi kama hili? Na wanaotumiana video wenyew kwa wenyewe au kuonekana "live" siyo kwambba watatakiwa wawe na leseni? au wanaotumia mitandao kurusha "live" training kutoka sehemu moja kwenda nyingine nao watatakiwa wawe na leseni?
Ni wakati gani mawasiliano yatachukuliwa kama yako kwenye "private" realm na siyo "public" realm? Je, watu wote walioko Tanzania wanaoposti vitu mbalimbali (ambavyo vinaweza kuangukia kwenye 'electronic communication') watahitaji kuanzia sasa kuwa na leseni? Hii ikiwemo ni wanamuziki, bloggers n.k?
========
Barua iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba ya tarehe 30 Januari 2017, imevitaka vyombo hivyo kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.
“Kwa mujibu wa kifungu 13 (1) cha Electronic and Postal Communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma zozote za aina hiyo wawe leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano,” imesema barua hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Mamlaka ya Mawasiliano ilizitembelea Ofisi za kampuni hiyo mwishoni mwa mwaka jana(2016) ili kujiridhisha na Programu mpya ya JamiiLeo inayorushwa kwa mtindo wa Video katika YouTube, Instagram na Facebook kisha kuwekwa JamiiForums ikichambua habari kuu 3 za siku na maoni ya wananchi kutoka mitandaoni.