Mnaopinga na mnaounga mkono mmeusoma mkataba?

mrdocumentor

Member
Nov 27, 2021
43
53
Bandari imetawanya watanzania katika makundi tofauti tofauti, kuhusu bandari mambo mengi yameibuka Kama siasa, udini, na muungano pia umehatarishwa katika suala hili la bandari.

Na sio watu wote waliogawanyika wanafahamu chochote kuhusu mkataba husika kuna wale akina sisi ambao huwa tumezoea kukuza kila kitu kinachozungumzwa kwa ubaya kuhusu viongozi lakini pia wapo wale ambao wamezoea kusifia kila kitu kinachohusu viongozi.

Hapa ndipo pale utawapata watu ambao hata serikali ikisema tunawaletea dawa za kuua mbu watasema "serikali imepata njia ya kusambaza magonjwa kwa watu wake" Lakini pia hapa ndipo utapata wale watu ambao Hata Msigwa apost goli la msuva atasema "anamaliza Bando la serikali tu wakati bandari inauzwa"

Lakini hapo ndipo utapata watu ambao hata ngedere wapungue shambani watasema "Asante viongozi wetu"

Hawa wote wapo sahihi kwa mujibu wa namna walivyokuzwa na asili zao pia.

Ebu tuache hayo turudi kwenye hoja ya msingi.

Tumeusoma mkataba?

Uwiano kati wanaopinga na wanaounga mkono mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari yetu na hoja wanazotoa haulingani kabisa.

OPPOSERS
Wanaopinga mkataba ni wachache wanapinga kwa hoja uku wafuasi wao wakitembea na zile hoja bila kujua kama anaepinga aidha ana maslahi na kupinga kule au ni mzalendo kweli? Ili kupata jibu la swali hili lipo kwenye mkataba Je, Unapinga umeusoma huo Mkataba?

PROPOSERS
Wanaounga mkono kwa asilimia ni wachache sana na wana wafuasi wachache sana ila bahati mbaya au nzuri wana nguvu na mamlaka lakini pia wanapinga kwa hoja lakini kadri wanavyojitahidi kutumia nguvu kuwaelekeza watu ili waelewe wanachotaka ndivyo wananchi wanavyozidi kukaa mbali na wao kwa kuamini kuwa "wamehongwa ndo mana wanatumia nguvu kubwa".

Nani anajua kama madai hayo ni kweli au laah? HAKUNA!! Hapo ndo utagundua kuna haja ya wewe mwenyewe kuusoma mkataba ili ujue unasimama wapi Je, Umeusoma huo Mkataba?

Ni mawazo tu ambayo nmejarbu kuwaza na nmeona ili usitekwe na hili joto la upande wowote kati ya hizo pande mbili Aidha ujitoe kabisa uache liende au tafuta vyanzo vya kueleweka upate knowledge yako alafu tulia nayo baki na msimamo wako kwa sababu sauti yako haina nguvu ya kuba
dilisha hali iliyopo.
 
Back
Top Bottom