Shame article,unatumia vyombo vyako vya habari kusambaza ujinga. Na wewe jibu maswali haya:-
1. Hasara ya mabilioni umeyaona kwa Tanesco. Ok je Tanesco ilikuwa na mapato kiasi gani huko nyuma? Ainisha na miaka kama ulivyoainisha hasara.
2. waliopata umeme toka Muhongo hajawa madarakani mpaka amekuwa waziri wa wizara hiyo ni wangapi? Tanesco miaka yote ilikuwa inaenda kwa hasara kwa wateja kidogo walionao,sasa kwa miaka hiyo uliyoitaja ya hasara kama wateja wameongezeka ulitegemea hasara itapungua itazidi? Kama kipindi cha Muhongo hakukuwa na mgao unategemea nini si lazima hasara iongezeke maana huduma inapatikana kwa wingi na hasara lazima iongezeke tu,kwani toka mwanzo wakiwa na wateja kidogo ni hasara,tuchukulie wakati wa mgao tanesco ilikuwa inanunua lita 100 za mafuta na wakati hakuna mgao inabidi wanunue mafuta lita 1000 hapa unategemea nini? Kwa nini hasara isiongezeke,tukumbuke hapa shirika haliendeshwi kibiashara
3.Mikataba ya migodi imepitiwa msipotoshe watu,ila tunataka maboresho zaidi na udhibiti zaidi. Tukumbuke Nyerere alipotaifisha mali za watu alitaifisha za wazawa pia,maana aliamini bepari ni bepari tu awe mzungu,mswahili au mhindi,kwa hiyo tusichukulie kuwa mzawa una haki zote kumiliki wewe na ndugu zako migodi ya geita na kufanya unavyotaka. Tanesco na wizara hizo Muhongo kazikuta za hovyo hivyo basi kipindi hicho kifupi kafanya mageuzi mengi tu na hawezi kumaliza mambo yote kwa mara moja.
4. Umeme unakatikakatika mara kwa mara,ok. Ni sawa na mgao uliokuwepo? Na ukatikaji wa mara kwa mara ni hujuma mlizokuwa mnamfanyia kwa kushirikiana na makampuni mengine ya umeme ili ashindwe kutekeleza azma yake ya mgao ubaki historia tu.
5. Ni lini au ni waziri yupi aliyeshika wizara hiyo na kuwadhibiti Tanesco kama Waziri Muhongo? Imefika Tanesco wanakupigia simu saa Fulani tunakuja kuweka umeme nyumbani kwako,toka uhuru imewahi kutokea? Waziri Muhongo kakata mirija Tanesco hivyo maadui walikuwa wengi tu na sasa kila mfanyakazi Tanesco meno njia wanajua ulaji umerudi. Na katika mirija aliyoikata ipo pia kina Zitto na Mkono waliokuwa wakishirikiana na Mkurugenzi wa zamani wa Tanesco kwenye ulaji wa shirika hilo,je Muhongo atakuwa salama?
Mheshimiwa Muhongo unafaa hata kuwa Rais wan chi hii,maana nchi kwa sasa inataka mtu jeuri na dikteta na anayetoa amri na msimamo usioyumba. Kwa kazi hakuna waziri yeyote toka uhuru mpaka sasa aliyeimudu wizara kama wewe,ni siasa za chuki na ulaji ndio zilizokuchafua,ati wanakuita dalali, wamekosa cha kuwathibitishia umma kama ulipata mgao,mbona wengine wameweza kwa nini wewe washindwe? Siasa chafu tu hizo,mbona wamemsitiri kiongozi wa upinzani ili upinzani usiabike na kusambaratika na ndio gia anayoingilia Zitto sasa kutaka kurudi Chadema. Unafikiri watamkataa wakati kamfinika mkuu nguo?
KAMA HASARA YA TANESCO IMETOKANA NA KUTOKOSEKANA KWA MGAO HIYO SIYO HASARA NI FAIDA KUBWA