REGINALD MENGI SASA VITA RASMI NA SOSPETER MUHONGO KUPITIA VYOMBO VYAKE VYA VYA HABAR
Habari za jumatatu wadau.
Leo ukurasa wa mbele kabisa wa *gazeti la NIPASHE umepambwa na picha kubwa ya Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Sospeter Muhongo huku kukiwa na kichwa cha habari kinachosomeka "WANAOMTETEA PROF. MUHONGO WAJIBU HAYA"
1.ametajwa kuwa dalali uchotwaji wafedhaza ESCROW
2. Chini ya utawala wake deni la TANESCO limepaa maradufu kufikia bi.456
3. Umeme bado hautabiriki, unakatika kila uchwao
4.mikatab ya Madini haijapitiwa kama alivyoahidi
Ndugu wapendwa ni dhahiri hayo yanatokana na ripoti ya PAC bungeni kuhusiana na fedha za Tegeta ESCROW.
Lakini pia kujikumbushe kuwa kwa takribani kipindi chote baada ya ripoti ya PAC bungeni kumekuwepo na mijadala kwenye mitandao ya kijamii na hata nje ya mitandao ya kijamii kuwa Mfanyabiashara, REGINALD MENGI yuko nyuma ya sakata la tuhuma dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Sospeter Muhongo la kutaka aondolewe kwenye nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini *kwa kile kinachosemekana ni kuchukizwa na kauli ya Waziri Muhongo Bungeni kuwa wanaosema wananyiwa kuwekeza kwenye vitalu vya gesi kama wazawa ni hawana uwezo kwa kuwekeza bali ni MADALALI ili wachukue vitalu na kuwaita wageni waje kuwekeza.
Swali la kujiuliza hapa. KWA NINI Mh. MUHONGO aitwe DALALI kwenye pesa za TEGETA ESCROW *baada ya kutoa kauli ya UDALALI Bungeni?*
Kuna kila sababu ya kuamini kuwa kitendo la Muhongo kuitwa DALALI na maneno haya kuonekana tena na tena kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na REGINALG MENGI likiwemo gazeti la NIPASHE toleo la leo *ni kutaka tu kutusahaulisha maelezo ya mh. WAZIRI kuwa REGINALD MENGI ni DALALI katika suala zima uwekezaji.
Mwandishi wa NIPASHE anawataka wanomtetea Waziri Muhongo wajibu kwa nini kipindi chake deni la TANESCO limefikia bil.456. Lakini mwandishi amesahau kujiuliza kabla ya hapo deni la TANESCO lilikuwa dogo kwa sababu gani na sasa ni kubwa kwa sababu gani?
Niainishe machache ambayo yanaweza kuwa sababu za deni kuongezeka lakini kwa manufaa ya wananchi
1. Ni kipindi cha Muhongo, gharama za kuwaunganishia wateja umeme zimepungua, lakini kupungua kwa gaharama kuwaunganishia wateja umeme hakupunguzi gharama za kuendeha shirika la TANESCO, ni wazi gharama zilizokuwa zikibebwa na wananchi sasa zinabebwa na shirika.
2.Waziri wakati akijibu hoja za ripoti ya PAC kuhusu pesa za ESCROW alisema kuna mwanasheria alikuwa amelipwa shilingi bil.62 katika kesi yaTANESCO na IPTL.kabla hajaamua shirika lisitishe mkataba na mwanasheria huyo ambaye alikuwa analigharimu shirika pesa nyingi, si ajabu hizi pesa bil.62 ni sababu ya deni la TANESCO kupaa.
3. Ni kipindi cha Waziri Muhongo Umeme umesambazwa katika vijiji vingi nchini(siyo rahisi vijiji vyote tanzania kufikiwa na umeme kwa wakati mmoja) na kama tunavyofahamu mara zote bajeti ya Serikali imekuwa haitoshelezi siyo kwa Wizara ya Nishati na Madini pekee bali Wizara zote.
Jamani eti hata suala la *Umeme kukatika nalo linakuwa sababu ya kumuondoa Muhongo kwenye uwaziri, kweli? Mbona mwandishi hatuambii umeme hautabiriki ukilinganisha na kipindi cha Waziri gani?. Tukumbuke huko nyuma siyo kwamba umeme ulikuwa unakatika tu, la hasha.Kulikuwa na *mgawo wa umeme. REGINALD MENGI anasahau kuwa kipindi cha nyuma(kabla ya MUHONGO), kuna wakati ITV walikuwa wanasitisha kurusha matangazo kutokana na mgawo wa umeme na kupelekea kushindwa kumudu gharama za mafuta ya genereta. Lakini pia tukumbuke kwamba sasa hivi TANESCO wanabadilisha mifumo yao ya mitambo kutoka ya zamani kwenda ya kisasa, hivyo inawezekana kabisa matatizo ya kukatika kwa umeme kunatokana na matengeenezo na siyo kutokuwepo kwa umeme.
Eti wananchi wanena! Akina nani hao? DEVID SILINDE? mwandishi alitaka awe kinyume na bosi wake ambaye anayetumiwa na MENGI ili awatumie vijana wake kama SILINDE kumchafua Mujongo? Hakipendi kibarua chake au *hapendi kionekana ili naye awe kama akina Mnyika, LISSU na wengine ndani ya chama?
Katika hotuba yake wakati wa kuchangia ripoti ya PAC , mbunge wa Muleba , Charles Mwijage ni miongoni mwa Wabunge waliomtetea sana Muhongo hasa akirejea kazi kubwa aliyoifanya ya kupeleka Umeme vijijini, leo tunapoambiwa kuwa amemponda Waziri Muhongo, napata mashaka kama hii habari iliyoandikwa na gazeti hili ni ya kweli au basi tu ni VITA YA *MANENO ambayo MENGI ameamua kuifanya kupitia vyombo vyake.
EZEKIEL MAIGE , aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ni mmoja wa Wahanga wa siasa nchini na asipokuwa na moyo wa uvumilivu wa majeraha aliyoyapata angefurahi kuona wenzake nao wanajeruhiwa ili ule msemo wa waswahili wa KIFO CHA WENGI NI HARUSI uweze kutimia.*
Vivyo hivyo kwa Prof. KITILA MKUMBO, mpaka sasa kilichoko mbele yake kisiasa ni giza nene. Zile ndoto za ZITTO KABWE kuwa nao kule ACT- TANZANIA ndiyo hivyo zinafifia. ZTTO ametumia vizuri turufu ya TEGETA ESCROW na pasi na shaka msaliti huyo atarejea kwa wahafidhina. HIVYO MKUMBO ni lazima sasa awe na maneno malaini ili naye arushe karata yake kama ZITTO KABWE.
Nimalizie tu kusema SOSEPETER MUHONGO NI DALALI KWA SABABU ALIMWAMBIA REGINALD MENGI NI DALALI NA SIYO VINGINEVYO
QUOTE=SELFISH;11343241]1) Hivi dalali hua hapati pesa, mbona yeye hajatajwa?
2) Mnashangaa kwa nini deni limeongezeka, mbona hamshangai kusambaa kwa nguzo nchi nzima au mlijua anatoa pesa mfukoni kwake?[/QUOTE]