Wanaomnanga jkikwete............mazishi ya madiba, kidedea!

Moony

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,595
1,195
Afrika ya Kusini, Africa nzima ikiwakilishwa na Dr Kenneth Kaunda wamempa leo JK stahili yake.
Amepewa heshima kubwa katika nafasi ya waalikwa na familia na serikali ya RSA.

Kwa kweli speech yake yenye maneno mazito yamekonga nyoyo za watu wote waliomsikiliza. Ameiwakisha Tanzania na watanzania vilivyo, ameitangaza Tanzania, amemuenzi MWALIMU, walokuwa hawajui ROLE ya Mwalimu na Tanzania iliyoplay katika harakati za ukombozi wa kusini mwa Afrika, leo wamejua, waliokuwa hawajui Uhusiano wa wa tangu zama zile wa Mandela na Mwalimu na Tanganyika hata wewe mwana JF ukiwa mmoja wao tumefunguka macho. Kwa kweli it was a touching moment to hear our President speaking.
Japo wana JF wengi kwa niaba ya makundi yenu mmezoea kumponda, kumnanga, kama unakosoa serikali.. RUKSA! lakini ujijumuishe na wewe, badala ya kulalama na kutukana, provide solutions ama mikakati.
Nadhani kwa kumuenzi Mandela, tu reconcile na Rais wetu, tumtie moyo amalize awamu yake kwa amani. Hongera na Asante KIKWETE leo umetuinua juu sisi Watanzania na Nchi yako Tanzania.
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,531
2,000
Unajua watz ndo maana tunadharaulika sana...watu wanadhabikia utumbo sijui kwa nini..ss jk alichofanya cha ajabu nini...? Hotuba mbovu kabisa imejaa kujidai kwingi wala haijamuenzi mandela...unaongea ooh tulimpa passport so what?
 

Moony

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,595
1,195
Unajua watz ndo maana tunadharaulika sana...watu wanadhabikia utumbo sijui kwa nini..ss jk alichofanya cha ajabu nini...? Hotuba mbovu kabisa imejaa kujidai kwingi wala haijamuenzi mandela...unaongea ooh tulimpa passport so what?

Peleka pepo lako huko; ulaaniwe
 

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,311
2,000
Unajua watz ndo maana tunadharaulika sana...watu wanadhabikia utumbo sijui kwa nini..ss jk alichofanya cha ajabu nini...? Hotuba mbovu kabisa imejaa kujidai kwingi wala haijamuenzi mandela...unaongea ooh tulimpa passport so what?

Natamani nikujibu.........nimeamua kukuignore
 

manjumkuu

Member
Nov 22, 2013
5
0
Rais wetu ametuwakilisha vizuri sana. Ile speech ilikuwa re conciliatory kama Madiba alivyokuwa. Unajua kule South kuna issue ya ku sideline waafrika wahamiaji. Ni issue kubwa kwa wanaoenda kutafuta maisha kule. Vijana wengi wenyeji wanawaona immigrants kama tishio katika fursa za ajira. Hivyo kuna chuki dhidi ya wahamiaji. Speech ya JK imelenga kuwajulisha hao vijana namna watanzania tulivyojitolea kutafuta uhuru wa nchi yao. Ile ilikuwa forum nzuri kufikisha ujumbe na naamini ujumbe utafanya kazi. Angalao vijana wasiojua historia kule South watakuwa wamefunguka. The speech was pure economic diplomacy. Big up JK
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,101
2,000
Yeah..ilikua nzuri..lakini kama tujuavyo huwezi kumfurahisha kila mtu..
 

SUKAH

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
714
500
Ingetokea JK ndio rais wa kwanza Tz halafu akae uongozin zaid ya miaka 20 kama babaake Makongoro hii nchi tusingekuwa tunazubaazubaa hapa tulipo.

Maana jamaa naona ndio kama anaanza kuijenga nchi upya.
 

made

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
814
500
Leo dunia nadhani hata wale wa SOUTH AFRICA wanaowanyanyasa wageni watakuwa wamejifunza kama historia hiyo ilifunikwa huko kwao na hapo Mugabe hakualikwa najua alikuwa na mengi sana.
 

Kiwa

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,106
1,250
kwan JK alipewa chance kuongea kuhusu nini?
-jinsi tanzania ilivyomsaidia madiba katika mapambano?
-jinsi tanzania tunavyomchukulia madiba?
-au vitu alivyofanya madiba ambavyo vinabidi vienziwe?
-alitakiwa aongelee uhusiano wa TZ na SA?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom