The Next MP
Member
- Nov 15, 2023
- 38
- 45
Tufaidishane pengine tukaokoa watu wengi kutotapeliwa au kuingiza faida.
Kuna namba ilinitumia message telegram wakidai wao ni kampuni ya marketing za online ambapo wanafanya media buy wakishirikiana na makampuni mbalimbali. Wanachofanya ni ku-recruit watu kufanya kazi ya ziada binafsi walinipa link nikawa na access ya kuona kinachoendelea kwenye group la telegram lenye wafuasi zaidi ya elfu 8. Kila baada ya dakika 20 wanaweka link unaenda ku-like na ku- subscribe, unascreenshot unamtumia alokuunganisha. kila action moja ya hivo unapata elfu moja.
Wiki iliyopita sikuwa biz kwahiyo kila link nilifanikiwa kufanya hivyo na nikatumiwa 27,000. nikafanya kwa siku 5 kila siku nikawa napata hicho kiasi. Hiyo kazi inabidi uwe na bando na muda wa kutosha kuchungulia kila mara kama kwenye group kuna link. Hizi link ni za makampuni na taasisi mbalimbali pamoja na wasanii wakubwa.
Kwenye group naona kinachoendelea na link zilikuwa zinatumwa mle lakini sina access ya ku-comment. Sasa kilichonishtua ni kwamba kuna wakati wanatoa orodha ya viwango vya pesa vya ku-invest yaani mtu anatuma pesa ndani ya dakika 30 anarudishiwa na kamisheni ya 9% mfano ukituma 30,000 anarudishiwa 39,000. wanajaribu kunishawishi lakini hii binafsi naona wazi wanataka kunipiga kwasababu kwa upande wangu mtu akishaingia hatua ya mimi kutuma pesa huwa naamini tayari huu ni utapeli. So naomba yeyote anayejua haya mambo tujuzane mimi huwa napenda kujifunza JF kabla ya kufanya kitu maana ni moja ya kuchunguza haya mambo. Karibuni wadau.