Wanaohamia CCM kutoka upinzani wanafanya hivyo kutafuta vyeo na masilahi mengine, wakiyakosa wataendelea kubaki?

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,386
73,980
Nipe historia ya KANU, UNIP ya Kaunda etc! Historia ni mwalimu mzuri. CCM imesismama (kama kweli imesimama) kwa vile inapendwa na wanaohamia au ni kwa vile kuna "marupurupu" yanafuatwa?

Kwangu mimi CHADEMA imesismama pamoja na kutokuwa na nguvu ya dola kwa vile walioko wana nia ya dhati na malengo yake.

CHADEMA iko mioyoni mwa watu na si kwa vile kuna manufaa yanapatikana kutokana na upendeleo wa kidola unaofanywa na Magufuli!

Askofu Bagonza amesema namnukuu "Umaskini wa fikra unazitafuna siasa (na soka la) Tanzania. Kuna siku mtamsingizia tasa kuwa ana mimba (na mwenye mimba kuwa tasa).!
 
Umasikini, majukumu ya kifamilia,ukosefu wa ajira na watu kulinda masilahi yao waliyoyapata kabla ya kujitoa CCM na kujiunga upinzani, kwangu mimi ndizo hasa sababu kubwwa za wanasiasa kuhama upinzani na kujiunga CCM.

kuna wanaohama kwa kuahidiwa vyeo,matumaini ya kupata vyeo,kutafuta ajira,kutafuta fursa za kupitishwa na CCM kugombea katika uchaguzi mkuu wa baadae mwaka huu,n.k.

Lakini pia wapo wanaoamua kwenda CCM kutokana na sisi kama nchi kutokuwa na tume huru ya uchaguzi hivyo kugombea kupitia upinzani kwa sasa ni kama kupoteza muda kwani teyari kuna mtu anatuhumiwa kuwatisha watakaotangaza wapinzani washindi na tumeona yaliyotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni.

Ni wazi,CCM hii ingekuwa inafanya vizuri,basi hata wananchi wa kawaida tungewaona kwa mamia au maelefu wakijiunga CCM jambo ambalo halipo na CCM kwa kujua ukweli huu,ndio maana swala la tume huru wanalipinga.

Swali ni je,wanasiasa hawa wanaokimbilia CCM kwa masilahi yao binafsi wakikosa wanachokitarajia huko CCM,wataendelea kubaki huko na kuwa waaminifu?

Tukumbuke teyari kuna ambao walihamia huko na kupewa vyeo na wengine wanaendelea kuhamia huku kuna wana-CCM ambao nao wanasubiri uteuzi,n.k.

Swali ni je,itawezekana kuwaridhisha wote hawa?

Kwa mfano,watakaotoswa baada ya uchaguzi mkuu,wataendelea kubaki CCM?

Na wakibaki,hawatakuwa na vinyongo?

Je,political migration hii si hatari kwa CCM katika siku zijazo?

Je,huku sio kutengeneza "time bomb"?

Kuhama huku kunaisadia CCM kujiimarisha kisiasa au kuna fanya wananchi wapuuze siasa na wanasiasa wakiwemo wanasiasa wa CCM na chama chao chote kwa ujumla?

Time will tell.
 
Hao wanaoingia CCM wameshapimwa kwamba hawatakuwa 'threat' kwa maneno na matendo na hii inatokana na CCM kuwa na mfumo imara sana.
 
Hao wanaoingia CCM wameshapimwa kwamba hawatakuwa 'threat' kwa maneno na matendo na hii inatokana na CCM kuwa na mfumo imara sana.
Kama kina Sumaye na Lowassa waliikacha CCM baada ya kukatwa,hao wanashindwa nini kuondoka kama watakosa nafasi?Umakini wa CCM haukuwaona akina Lowassa na Sumaye kuwa watakuja kuwa tishio?
 
Huyu kawa mkweli familia inaitaji kula
mashinji.PNG
 
Vyama vingi vya upinzani vinatatizo kubwa sana la uongozi, wanachama wengi wana pata ghadhabu wakitaka kuleta idea mpya kwenye chama wanajikuta wako kwenye kundi la waovu.

Mashinji amepambana na mengi sana ndani ya Chadema, amelalamika kwa muda mrefu bila kisikilizwa. Kama sio malumabo ya kifedha basi ni malumbano ya mweleko wa chama, kama sio maswala ya sera basi ni nani anastahili kupata nafasi ya uwongozi.

Vyama vyote vya upinzani ni vigumu kupishana kauli na kiongozi ukabaki salama.
 
Nipe historia ya KANU, UNIP ya Kaunda etc! Historia ni mwalimu mzuri. CCM imesismama (kama kweli imesimama) kwa vile inapendwa na wanaohamia au ni kwa vile kuna "marupurupu" yanafuatwa?
Wanaohamia CCM wamejitambua!, Chadema hakuna kitu!.

P
 
Nilishasema na wewe Mayalla, ukitaka kuwa betrayed weka kunji (sijui kama unaijua enzi hizo UDSM miaka ya 70_80)na msukuma, umekwisha!
Wanaohamia CCM wamejitambua!, Chadema hakuna kitu!.

P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Peleka idea kwa Magufuli ukirudi ni beep
Vyama vingi vya upinzani vinatatizo kubwa sana la uongozi, wanachama wengi wana pata ghadhabu wakitaka kuleta idea mpya kwenye chama wanajikuta wako kwenye kundi la waovu. Mashinji amepambana na mengi sana ndani ya Chadema, amelalalmika kwa muda mrefu bila kisikilizwa. Kama sio malumabo ya kifedha basi ni malumbano ya mweleko wa chama, kama sio maswala ya sera basi ni nani anastahili kupata nafasi ya uwongozi. Vyama vyote vya upinzani ni vigumu kupisha kauli na kiongozi ukabaki salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Peleka idea kwa Magufuli ukirudi ni beep

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo lenu hamuijuwi CCM, Magufuli ni mwenyekiti wa "vikao" vya chama na wala sio mwendeshaji wa kila siku wa chama. Tofauti na vyama vyenu wannabe ambapo mwenyekiti au kiongozi wa chma ndio katibu kuu, ndio mweka hazina, ndio mnadhimu mkuu na ndio mfadhili. Chama sio mali ya mtu mmoja, vyama vyote vya siasa Tanzania ni mali ya jamii.
 
Back
Top Bottom