Wananchi Wilaya ya Serengeti watoa ushuhuda hadharani ndugu zao kuuliwa na Askari Nyamapori Serengeti

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wananchi wilayani Serengeti watoa ushuhuda hadharani jinsi ndugu zao waliovyouliwa na Askari Nyamapori. Hili lilifanyika katika mkutano wa hadhara uliofanyika Serengeti ambapo Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA, Catherine Ruge aliwapa kipaza sauti wananchi hao kuelezea jinsi ndugu zao walivyopotea.

Baada ya mkutano huo Catherine, watu waliotoa ushuhuda na baadhi ya wanachama wa CHADEMA walikamatwa na polisi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Mugumu mjini, ambapo walioachiwa baada ya kutoa maelezo.

 
Watu wanatoa taarifa halafu wanakamatwa na polisi?

Kutoa taarifa siku hizi limekuwa kosa?

Wanataka uhalifu uongezeke mitaani, tunatawaliwa na wajinga kila idara ya serikali.
 
Watu wanatoa taarifa halafu wanakamatwa na polisi?

Kutoa taarifa siku hizi limekuwa kosa?

Wanataka uhalifu uongezeke mitaani, tunatawaliwa na wajinga kila idara ya serikali.
Hapo sasa, badala ya kufanyia kazi malalamiko wanakata watu
 
Back
Top Bottom