Moshi: Askari atoa majibu ya yasiyoridhisha mbele ya Mkuu wa Wilaya

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Siku ya Jumatatu saa sita kamili nilifanikiwa kuwa miongoni mwa wananchi wa Kata ya Shimbwe kwenye kikao cha Mkuu wa wilaya na wananchi

Huyu si mwingine ni mkuu wa Wilaya Moshi, lazima nikiri na niwe muwazi mkuu wa Wilaya ya Moshi ni miongoni mwa wakuu wa wilaya wenye Busara, hekima nina imani na elimu yake lakini zaidi nina imani hata experience yake ni kubwa katika utumishi wa Umma.

Sambamba na busara za Mkuu huyu wa Wilaya lazima tukili yakuwa ni mpole sanaa lakini pia ana upungufimu mkubwa sanaaa wa wataalamu wenye weredi kwenye wilaya yake kwa ujumla
Kwa kuwa leo nimeanza kuandika moja baada ya jingind naomba leo nigusie mapungufu makubwa niliyoyaona kwa idara kubwa mbili.

MOSI;
Nimeamini Mkuu wa Wilaya hana mapungufu ya katika idara ya usalama wa taifa wa wilaya.

Nijuavyo mimi nikuwa inapotokea mkuu wa kata mathalani mkuu wa nchi yaani Rais,mkuu wa Mkoa au hata Mkuu wa Wilaya anaenda sehemu kwa ajili ya ziara ya kikazi watu pekee wanao takiwa kutangulia eneo la tukio ni hawa niliowataja kwa lengo kwanza kuhakiki usalama,pili uwa ni kupeleleza changamoto zote zilizopo eneo ilo na kuziwaslisha kwa Mkuu kabla ya kukanyaga eneo la Tukio , ili sikuliona kwa mkuu wa wilaya ya moshi vijijini badala aliambatana na kundi la watu ajabu walio jiita wataalamu uku wakiwa na majibu ya ovyo ovyo ovyo sana mathalani Polisi Kata ya shimbe, Afisa Ardhi kichomi,Afisa Ushirika ovyo ovyo kabisa,Afisa kilimo aliyekuwa tungi uku akigeuza kikao cha mkuu wa wilaya kuwa mkutano wake na nk.

SIKITIKO;Busara za mkuu wa wilaya zilimuongoza asikilize kero tu na kutafuta suluhu la hapo kwa hapo pongezi kwake ni kuwa alibaini ameanmnbatana na wataalamu wa muchongo akaona bora abebe kero na kuondoka nazo

Kimsingi idara ilitakiwa itangulie ichunguze kero ishauri suluhisho mkuu akifika anaonekana ni mfatiliaji hapa siwezi lalamika ninafahamu vibwengo wengi mliopanngwa wilaya ya moshi ni walaibu tu hakuna mnachokifanya.

Nitaelezea uozo wa kila mtaalamu aliyekuja hapo kwenye kikao wakiwemo Tarula,Tanesco nk ila leo ni vyombo hivi kwanza.

PILI POLISI HAPA NAANZA NA OCD WILAYA YA MOSHI NI AIBU.

Naomba nieleweke kidogo hapa kwenye kikao kile ocd hakuwepo ila aliwasilishwa na POLISI KATA MWENYE NYOTA MOJA NA ALIJITAMBULISHA KWA CHEO CHA MKAGUZI.

(alikumbusha rafiki yangu mmoja nilitambulishwa yakuwa ni mkaguzi aliyemtambulisha hakujua yakiwa mim nimjua zaidi yule bwana na hata kidato cha kwanza mpaka cha nne tulisoma pamoja na alipata division ZIRO SIKU HIYO ALIITWA AJE KUNISUTA AHAHAA jamaa aliona aibu ila nilipotoka nje akaanza kunongona na boss wake yakuwa mimi sio kitu).

inapotokea mwakilishi wa mtu akawa ovyo tunapata picha yakuwa hata anae wakilishwa nae yupo hivyo.

Wananchi mbele ya mkuu wa wilaya walikuja na hoja tatu.
Mosi MAUAJI

Aliyeleta concern hii ni mtumishi wa Umma kwa maana ya mtendaji alilalamika mauaji yanatokea sana kata ya shimbwe na moja ya watu walio Uawa ni mwana mama mmoja na ushahidi yeye kama mtendaji na mwenyekiti wake wa kijiji walienda polisi wakaripoti tukio na ushahidi wa wazi wazi kabisa. Ila watuhumiwa walikamatwa na kurudishwa mtahani siku ya tatu

Swali anaulizwa Askari kata(anae uliza ni mkuu wa wilaya,je hayo amuaji anayajua na yamefikia wapi?

JIBU; SIKUWEPO SIKU HIYO NILIKUWA NA KAZI MAALUMU ila nawambia ndugu wananchi mnashitakiana muwe tayari kuleta ushahidi sio mnashitaki na kukimbia.

Hahahahahahah

Yaani aliyepeleka taarifa ni mtendaji wa kijiji kwa kushirikiana na mwenyekiti wake na mpka leo hii wapo na watuhumiwa wapo mitaani unasemaje wamekimbia waleta ushahidi?(tulio somea investigation tuliliona ilo afande ni boya tu).

Kesi iko kituoni tangu mwaka jana,usalama wa taifa mpo,polisi wapo na watuhumiwa wapo mtaani.


MAUAJI YA PILI YA KIJANA MWAKA HUU,

Mkuu wa wilaya anauliza tena je haya nayo wayajua

Majibu ya Afande mwakilishi wa OCD Wilaya.

Heeee nayajua mchakato unaendelea tunaomba sana mnaposhitaki mje mlete ushahidi.

Hahahahahaha hahshs jamaaa anajibu swali uku ameweka mkono mmoja mfukoni akiwatizama wananchi,mkuu wa wilaya anaona na sisi wapita njia tunaona.


KITUO KIPYA CHA POLISI

anasimama mh Diwani anaelelezea yakuwa jengo la kituo limeisha kamilika ni bora kifunguliwe.

MKUU WA WILAYA ANAMNYANYUA TENA AFANDE MWAKILISHI WA OCD

KWANINI KITUO AKIFUNGULIWI?

Mh Dc kituo hakina benderA,akijipigwa rangi ya jeshi la polisi,hakina viti na Umeme.(MAJIBU HAYA YAZINGATIE YAKUWA KITUO KIMENJENGWA NA NGUVU ZA WANANCHI HAKUNA MIA YA JESHI LA POLISI WALA SERIKALI LAKINI MAJIBU YA AFANDE.).

Mkuu wa wilaya anagundua kasoro za askari huyo na majibu yake anamua kusema ilo nalo analibeba .

TATU(HAPA AFANDE NDO ANA PUUZA KAISA AMRI YA MKUU WA WILAYA.).

Anatokea mwananchi analalamika kuna saccos yao imefungwa kwa uzembe wa viongozi na watu kula pesa zao mkuu wa wilaya anaita viongozi wa saccos anabaini hawapo kwenye kikao chake na waliakwa.

Anamwelekeza yule Afande awatafte waandike maelezo kwa nini hawataki kutoa ushirikiano ili hizo fedha zirudi, ikumbukwe sio kuwaweka ndani ni kutoa maelezo ni ya kwanini hawatoi ushirikiano.

Yule Afande ananyanyuka na kubana makalio na kupiga saluti kumwoneshaa ametii kumbe,kimoyo moyo alikuwa akimtukana yakuwa ni fala wewe.

Baada ga kikao Afande anapanda gari na kusepa hana time mpaka wa leo.

Hii ni sehemu ya kwanza kesho ntakuja na MAJIBU YA AFISA Aridhi mcheke mfeeeeeeeeee.
 
hoja ya afande kufeli form 4 achana nayo,inaweza sababisha ukaonekana una vita naye binafsi ya kuporwa demu ama shamba sehemu.

halafu kama afande alimtukana kimoyomoyo wewe ulisikiaje mkuu???

jenge hoja katika weledi wake,lakini pia nikukumbushe,polisi hajapewa mamlaka yeyote ya kumpeleka mtu jela kwa hisia au utashi wake,isipokuwa kwa ushahidi uliotosha kumkuta mtuhumiwa na hatia mahakamani,yeye kazi yake ni kukamatana kupeleka mahakamani.mtu asipokutwa na hatia akatoka ni hatari hata kwa usalama wake maana inaweza tafsiriwa na mhusika ilikuwa ni jaribio la kumharibia future mhusika.
vibaka wengi wanaachiwa polisi na kuendelea kusumbua sababu hiyo hiyo hapo juu,anakosekana shahidi au mlalamikaji wa msingi tok mwanzo wa kesi mpaka mwisho mahakamani,mtuhumiwa anaachiaa kwa dhamana.
 
Boss ! Kwa heshima . Kindly, edit your work ili tupate flow nzuri Kuna typos nyingi, natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom