Nampongeza rais kikwete kwa uongozi bora
Wakuu hatuna kipengele cha kumpa nafasi nyingine rais baada ya kustaafu hatuna katiba inayotaka hivyo.
Umeshasahau kuwa uchaguzi uliopita tu "alikula ngwala" mpaka akampigia magoti muumini mwenzie Lipumba "aokoe" jahazi.Akigombea 2015 itabidi atembee na mtungi wa hewa ya oxygen,maana itakuwa sio zomeazomea hiyo!!!!Maoni ya kwenye Dala dala la vibarua hayaakisi mawazo ya watanzania! Kama mnadhani kachokwa turuhusu agombee tena chini ya hii katiba mpya muone watavokula za uso wale watu wenu, jakaya kachokwa Jf sio mtaani, kuna watu wanadhan mawazo ya multiple ID ya jf ndo ya watanzania.
Kikwete ni mtu wa watu na ni rais bora sema katiba yetu haitoi fursa ya mtu kuongezewa muda wa urais.
Leo tukiwa tunaenda job asubuhi kwa gari lakzini ( Staff bus) tukawa tunasikiliza dondoo za magazeti mara kikasomwa kichwa cha habari katika gazeti la Raia Mwema chenye muundo wa swali kuwa "JK Kuongezewa muda?" watu karibu wote basi zima wakaguna na kusema "mmmh tena? inatosha!" Mara ukaibuka mjadala humo ndani huku watu wengi wakisema hawataki kusikia hiyo habari.
Swali ni kwamba ni kweli wananchi wamemchoka mheshimiwa kiasi hicho? Na je hali ikoje katika eneo ulilopo?
Kiongozi yeyote unayemfahamu ni chguo la Mungu ndiyo maana Mungu amesema Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.Kwenye gari mliokuwemo wala amzidi 20 halafu mnataka kuwasemea Watanzania zaidi ya milioni 40. JK chaguo la Mungu, Askofu Kilaini.
Kikwete ni mtu wa watu na ni rais bora sema katiba yetu haitoi fursa ya mtu kuongezewa muda wa urais.