Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 8,194
- 11,623
Kwa upendo wa wazi na wa dhati walionao wa Tanzania dhidi ya kiongozi huyu mkuu wa nchi, wanatamani aiongoze Tanzania bila ukomo, lakini ndio hivyo tena anaheshimu na kuitii katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, dhidi ya utaratibu ukomo wa uongozi.
Na kwahivyo baada ya ngwe zake kwisha atawaachia wengine waendelee pia.
Kiongozi huyu shupavu, madhubuti na mwenye mipango ya kuwaletea wananchi maendeleo, yuko imara hayumbishwi na chochote anachapa kazi kwa bidii, weledi, umahiri na umakini mkubwa kwa maslahi mapana ya waTanzania wote.
Anachapa kazi akiwa ndani ya nchi, anachapa kazi akiwa nje ya nchi. Tanzania ni tulivu, ulinzi na usalama watu na mali zao ni shwari na wa uhakika.
Maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi yanavyoshamiri nchini ndicho hasa kinachofanya wananchi wampende sana na kumuamini kiongozi huyu mkuu wa nchi.
Kwasababu wananchi wanafaidika na kunufaika na maboresho ya huduma zinazogusa maisha yao halisi mathalalani, katika sekta ya afya, Elimu, maji, kilimo, biashara, ufugaji , barabara, usafirishaji, usafiri wa anga na majini, uvuvi, ulinzi na usalama, uhuru wa maoni, uwazi serikalini, uwajibikaji kwa uchache sana.....
Masuala ya rushwa na utovu wa maadili katika utumishi wa umma yanashughulikiwa ipasavyo na hatua zinachukuliwa dhidi ya wahusika bila huruma wala upendeleo na wahusika wanawajibika vilivyo kwa makosa yao.
Nionavyo mie, katika uchaguzi ujao wa 2025, endapo atagombea Urais, basi ni dhahiri atashinda kirahisi sana na kwa kishindo kikubwa mno hapajawahi kutokea. Rekodi ya utendaji wenye weledi, tija na matokeo kwenye maisha ya waTz inambeba.
Atashindana na nani sasa kwa mfano humu nchini? Kwa kweli hakuna, ila bila shaka kutakua na wasindikizaji.
Mungu Ibariki Tanzania.