Wananchi inabidi muelewe migomo ya wafanya biashara

sney

Member
Jan 21, 2014
13
2
Migomo hii si kwa faida ya wafanya biashara tuu ila bali ni kwa wananchi kwasababu jiulize mfanya biashara anamuuzia nani kama sio mwananchi, that means kila kitu kitapanda bei ujenzi, uvaaji, vipodozi, simu vyote vitakuwa juu, wananchi amke jamani open your eyes and see, kila kitu kinapanda mnakaa kimya maisha yatakuwa magumu wa hali ya chini tutazidi kudidimizwa wake up Tanzania together we can
 
Mkuu acha kuwashawishi Wanainchi bila kuwa na ufahamu na unachowashauri. VAT ni kodi inayolipwa na mtumiaji wa Huduma, ama na Mnunuzi wa bidhaa. Nafasi ya Mfanyabiashara kwa kodi hii ni kuwa WAKALA wa kukusanya na kuwasiliaha TRA kila mwisho wa mwezi kiasi kamili cha Fedha zilizokusanywa. Wafanyabiashara hawataki kwa makusudi tu kutumia EFD's kwa sababu wanafahamu kuwa fedha walizokuwa wanazichukua kama VAT walikuwa hawaziwakilishi kwa usahihi na walikuwa wanajitajirisha kwa fedha haramu! Wnachotakiwa kufanya ni kuzikubali na kuendelea na maisha kama kawaida.
 
Migomo hii si kwa faida ya wafanya biashara tuu ila bali ni kwa wananchi kwasababu jiulize mfanya biashara anamuuzia nani kama sio mwananchi, that means kila kitu kitapanda bei ujenzi, uvaaji, vipodozi, simu vyote vitakuwa juu, wananchi amke jamani open your eyes and see, kila kitu kinapanda mnakaa kimya maisha yatakuwa magumu wa hali ya chini tutazidi kudidimizwa wake up Tanzania together we can

Mleta mada, maana yake unataka kuniambia mimi kama mwananchi na mnunuzi nihalalishe wizi unaofanywa na wafanyabiashara kwa kutuuzia vitu kwa bei iliyojumlishwa na kodi huku wao wakiacha kupeleka makusanyo ya kodi TRA?
 
kiukweli umeweka hoja yenye maana, mgomo huu ulitakiwa ufanywe na wananchi badala ya wafanyabiashara lkn kwakua serikali inajua inaongoza wadanganyika lolote wanaweza wakafanya bila ya kutokea chochote kwa wananchi. asilimia 18 kila kwenye mia inatoka kwa mwananchi anayenunua bidhaa yoyote kwenye 100. kwaiyo kwanza TRA wanachukua pacent kubwa kuliko faida ya mfanyabiashara. Tatizo la Tanzania wananchi wamelala fofofo, hata Kenya wananchi walipiga kelele sana mpk kodi imeshushwa.
 
Inabidi mchukue muda mrefu kuwashawish watz kuwa mnachogomea kina maslahi kwenu ama kwao; ninachojua ni kwamba waligomea bei kubwa ya kununulia machine hizo, sasa swala la bei ya mashine halitoshi kumwambia mwananchi agome labda umshawishi sana. Lakini tumeona mengi ambayo kimsingi yangepaswa kugomewa na wananchi, mfano ongezeko la bei ya umeme, huduma duni za kijamii; kumbuka mgomo wa madaktari wananchi ndio walipaswa kuona tatizo mana ndo walengwa. Watz ni watu wanaoamini kuwa amani ni hali ya kuwa mbumbumbu na kutouliza jambo la msingi linalokuhusu hata kama umelikosa kwa uzembe wa mtu mmoja. Siku asilimia 20 ya watanzania wakijua haki zao za msingi viongozi wa nchi hawatalala usingizi bila kutumia dawa za kulazimisha ubongo kulala
 
Yaani wewe hata huna uliloongea hapo.., porojo tu.., mwone kwanza. SEMA clearly.., mnachogoma ni nini hasa; je bei za mashine ni kubwa?, au ni kwamba ile asilimia 18 mliyokuwa mnakusanya mlikuwa hamuiwakilishi ipasavyo sasa hizi mashine zinawabana ndio mnagoma..???! nyie mlikuwa mnaiibia nchi.., sasa mtawakilisha 18% bila ubabaishaji.., wezi kabisa..!!
 
Balaki, we don't need kumshawishi mwananchi a strike, cos for mfanya biashara ataongeza price to cover up the 18% but the problem comes wateja watatoka wapi, coz bandari kwa kuongeza ushuru tulipoteza wateja wa nchi za jirani that means tumebakiwa na internal market which is not good for the country, zamani tulikuwa tunafanya vizuri ila tunarudisha maendeleo nyuma huku mkizani mnamkomesha mfanya biashara, we are doing this for our country. Mungu ibariki kariakoo Mungu ibariki Tanzania yetu we all love our green land
 
kiukweli umeweka hoja yenye maana, mgomo huu ulitakiwa ufanywe na wananchi badala ya wafanyabiashara lkn kwakua serikali inajua inaongoza wadanganyika lolote wanaweza wakafanya bila ya kutokea chochote kwa wananchi. asilimia 18 kila kwenye mia inatoka kwa mwananchi anayenunua bidhaa yoyote kwenye 100. kwaiyo kwanza TRA wanachukua pacent kubwa kuliko faida ya mfanyabiashara. Tatizo la Tanzania wananchi wamelala fofofo, hata Kenya wananchi walipiga kelele sana mpk kodi imeshushwa.

Una uhakika na unachomaanisha??? Kila kona ya dunia watu wanalipa kodi, sasa udanganyika unayika wapi ukitakiwa kulipa kodi???
 
ww kama kweli unaijua dunia nipe data za kodi inayolipwa UK kila kwenye bidhaa inayonunuliwa? nataka kukwambia kukwepa kulipa kodi ni ujinga lkn ukiona wafanyabiashara wanagoma ujue hakuna mpangilio mzuri na hakuna faida ya Kofi inachofanya. ukienda nchi za wenzetu unalipa bila ya kuhimizwa na kila mmoja anajua wajibu wake. hapa kwetu kodi zinaishia matumboni kwa wakubwa tuu
 
Sasa hapo unalinganisha tembo na panya.
 
Inabidi mchukue muda mrefu kuwashawish watz kuwa mnachogomea kina maslahi kwenu ama kwao; ninachojua ni kwamba waligomea bei kubwa ya kununulia machine hizo, sasa swala la bei ya mashine halitoshi kumwambia mwananchi agome labda umshawishi sana. Lakini tumeona mengi ambayo kimsingi yangepaswa kugomewa na wananchi, mfano ongezeko la bei ya umeme, huduma duni za kijamii; kumbuka mgomo wa madaktari wananchi ndio walipaswa kuona tatizo mana ndo walengwa. Watz ni watu wanaoamini kuwa amani ni hali ya kuwa mbumbumbu na kutouliza jambo la msingi linalokuhusu hata kama umelikosa kwa uzembe wa mtu mmoja. Siku asilimia 20 ya watanzania wakijua haki zao za msingi viongozi wa nchi hawatalala usingizi bila kutumia dawa za kulazimisha ubongo kulala

mkuu umeandika mambo ya msingi sana
 
Hivi we unaona sis wananchi ni wajinga sana.Yaani ninyi wafanyabiashara ambao kimsingi hata kodi hiyo kiduchu mnayolipa Serikalini tunaolipa ni sisi walaji eti tupinge mashine!!Kwanza Serikali hii haikusanyi kodi ipasavyo,wafanyabiashara hamlipi kodi ipasavyo,mnatuuzia vitu bei ghali halafu fedha nyingi mnatia mfukoni-Serikalini mnapeleka kiduchu!!
Namuomba Mungu CDM iingie madarakaniili ikusanye kodi ipasavyo sio CCM inawalambalamba.Mfano unakuta vitu vya kichina visivyo na ubora wowote )mnavinunua kwa bei ya chini halafu mnauza mara nne ya bei ya manunuzi;huu ni ushenzi kabisa.
Serikali kama inanisikia mlipe tena mashine mzinunue kwa bei ileile ya mwanzo 'no compromise'.Na mfanyabiashara anayekataa anyang'anywe leseni"FULL STOP"
 
Back
Top Bottom