Inabidi mchukue muda mrefu kuwashawish watz kuwa mnachogomea kina maslahi kwenu ama kwao; ninachojua ni kwamba waligomea bei kubwa ya kununulia machine hizo, sasa swala la bei ya mashine halitoshi kumwambia mwananchi agome labda umshawishi sana. Lakini tumeona mengi ambayo kimsingi yangepaswa kugomewa na wananchi, mfano ongezeko la bei ya umeme, huduma duni za kijamii; kumbuka mgomo wa madaktari wananchi ndio walipaswa kuona tatizo mana ndo walengwa. Watz ni watu wanaoamini kuwa amani ni hali ya kuwa mbumbumbu na kutouliza jambo la msingi linalokuhusu hata kama umelikosa kwa uzembe wa mtu mmoja. Siku asilimia 20 ya watanzania wakijua haki zao za msingi viongozi wa nchi hawatalala usingizi bila kutumia dawa za kulazimisha ubongo kulala