William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Mwishoni mwa miaka ya sabini zile bend kebekebe za Verkys zilipormoka ghafla huko Zaire ambapo kati ya wananmuziki wakuu walioondoka Zaire wakati huo ni pampja na Sam Mangwana aliyekwenda Kameron na Assosa aliyekuja Tanzania kujiunga na Mzee Makassy
Mkuu Kichuguu,
Heshima mbele, Assosa alitoka Orch. Kamale ambako alishirki nao kwene album yao ya misho yenye nyimbo kama "Assana Mwana Maua", "Andoya", na "Aidjo"
-Assosa, alikuja bongo na bendi ya Orch. Fuka Fuka kwa mara ya kwanza, na wimbo wake wa kwanza alioutunga kwa kiswahili na bendi hiyo akiw bongo unaitwa "Baba Isaya", baadaye bendi hiyo iliamua kwenda kuhamia Nairobi, yeye na mpiga drums wake Micky wakamua kubaki bongo na bendi ya Makassy, wimbo wake kwanza akiwa na Makassy, ilkuwa unaitwa "Mambo Bado" na mtindo wa "Disco Agwaya",
-Baadaye Makassy, alimleta mtoto wake anayeitwa Munsemba na kumuingiza kwenye bendi hiyo, lakini hawakuelewana na Assosa, ndipo Assosa akaingia Marquis na wimbo wake wa kwanza ulikuwa ni Huba Wangu, ninaamini kuwa mpaka leo bado yuko na Marquis.
baada ya Lemmy kuhamana Makassy na kuwenda Songea kuongoza bendi ya Mzee Matimila.
Remmy Ongara, alihama Makassy na kuingia Bendi ya Matimila, ya Mzee Matimila na Mwingira, iliyokuwa na makao mkuu yake kwenye Bar maarufu ya Ruvuma Mpaka Maputo, ilyokuwepo kwenye kona ya njia ya kutoka au kwenda Dar Airport.
Hawa wanamuziki wawili pamoja na Nyboma ndio waliokuwa mwagiji wa nyimbo maarufu kama "Moni Afinda" na "Masua" ndiyo maana kwenye ule wimbo wa Moni Afinda Asosa anatajwa wazi wazi wakisema "Asosa mama." Asosa aliletwa Tanzania na Mzee Makassy alipoanzisha mtindo wake wa Agwaya. Leo hii ni zaidi ya miaka 30 tangu Assosa alipokuja Tanzania, je kuna aliyewahi kufuatilia kama jamaa huyu alikuja kihalali na anaishi nchini kihalali pia?
1. Moni ya Finda ni wimbo ulioimbwa na bendi moja ya Verkyis, inayoitwa Orch. Kiam, na mpigaji wake alikuwa ni Muzola Ngunga akishirikiana na Memi.
2. Massua, ni wimbo uliopigwa na Orch. Kamale kwenye album ya Abissina , naona hapa mkuu umechanganya madawa kidogo maneno ya "assosa mama" yanasemwa kwenye wimbo wa Orch. Veve uitwao, Mikolo Milengi Mingi .
3. Assosa, aliondoka Zaire akiwa a big star kwa hiyo kila kitu kilikuwa taen care hata kabla hajaja na since then amekuwa star pa hata bongo, ndio nimesema kuwa wapiga muziki wa caliber yake hata siku moja hawajawahi kuulizwa haya maswali.